Zitto aibuka na mbinu ya kuing’oa CCM

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Messages
686
Points
1,000

Trust None

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2018
686 1,000
KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe aeleza mbinu zitakazotumiwa na chama hicho kukiondoa madarakani Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza katika ufunguzi wa Mkutano wa Halmashauri kuu ya chama hicho leo (jana) tarehe 29, Septemba 2019, amesema kuwa Serikali ya CCM kwa kipindi cha miaka minne hakikukidhi matakwa ya wananchi hususani katika uchumi.

“Uchaguzi wowote huhusu mambo ambayo yapo juu …unahusu mambo ambayo yapo chini...

wao wakija juu na ndege zao nyie nendeni chini na njaa za wananchi ambayo imesababishwa na sera za CCM,

Wakija juu na Reli zao nyie nende chini na hali ya elimu katika maeneo yao,

wakija juu na ‘stieglers gorge’ nyie nendeni chini kuangalia maelfu ya vijana ambao hawana ajira wanateseka,

wakija juu na lolote lao nyie angalie yanayowagusa wanachi moja kwa moja,” amesema Zitto.

Amesema kuwa ni watanzania wachache wanaoamini katika maendeleo ya vitu baadala ya watu kwa kuwa watu hawawezi kufanya shughuli za uchumi.

“Ni asilimia tano (5%) pekee ya Watanzania wanaopanda ndege, acheni wapigiwe kura na hiyo asilimia tano …hata hiyo tano hawatakuwa nayo yote, mimi napanda ndege na sitawapigia kura,” anesema Zitto.

Amewataka wanachama wa chama hiko kuwaendea wananchi na kuwapigania juu ya masuala yanayogusa maisha yao moja kwa moja ndipo watakapoeleweka.

Amesema kuwa ni watanzania wachache wanaoamini katika maendeleo ya vitu baadala ya watu kwa kuwa watu hawawezi kufanya shughuli za uchumi.

“Ni asilimia tano pekee ya Watanzania wanaopanda ndege acheni wapigiwe kura na hiyo asilimia tano …hata hiyo tano hawatakuwa nayo yote mimi napanda ndege na sitawapigia kura,” anesema Zitto.

Amewataka wanachama wa chama hicho kuwaendea wananchi na kuwapigania juu ya masuala yanayogusa maisha yao moja kwa moja ndipo watakapoeleweka.

-------
Je, CCM bila Polisi, Wakurugenzi na NEC watatoboa?
 
Barbarosa

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2015
Messages
20,093
Points
2,000

Barbarosa

JF-Expert Member
Joined Apr 16, 2015
20,093 2,000
Duh! Dunia ina maajabu, Mbunge ambaye Chama chake kina Mbunge mmoja anaongelea kukiondoa Madarakani Chama chenye Wabunge zaidi ya 200? Hivi tofauti ya Zito Kabwe na act yake na Cheyo na UDP yake ni ipi? Mimi nafikiri angejali kwanza kutetea kiti chake cha Ubunge kwa maana hata kama atarudi Bungeni, sijui.
 
LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2017
Messages
4,496
Points
2,000

LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Joined Oct 3, 2017
4,496 2,000
Duh Dunia ina maajabu, Mbunge ambaye Chama chake kina Mbunge mmoja anongelea kukiondoa Madarakani Chama chenye Wabunge zaidi ya 200? Hivi tofauti ya Zito Kabwe na act yake na Cheyo na UDP yake ni ipi?Mimi nafikiri angejali kwanza kutetea kiti chake cha Ubunge kwa maana hata kama atarudi Bungeni, sijui.
mkuu hizo Ni pumba, hakuna uhusiano wowote
 
mulaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2019
Messages
2,113
Points
2,000

mulaga

JF-Expert Member
Joined Sep 2, 2019
2,113 2,000
Duh! Dunia ina maajabu, Mbunge ambaye Chama chake kina Mbunge mmoja anaongelea kukiondoa Madarakani Chama chenye Wabunge zaidi ya 200? Hivi tofauti ya Zito Kabwe na act yake na Cheyo na UDP yake ni ipi? Mimi nafikiri angejali kwanza kutetea kiti chake cha Ubunge kwa maana hata kama atarudi Bungeni, sijui.
Wamezuiwa kufanya siasa huwezipata kipimo sahihi
 
moudgulf

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2017
Messages
67,791
Points
2,000

moudgulf

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2017
67,791 2,000
Inadaiwa kwamba hivi sasa makusanyo ya kodi ni makubwa kuliko hapo kabla, lakini jambo la kushangaza kwenye hospitali kubwa za Serikali tunalazimishwa kulipia huduma pamoja maiti wetu.
Kwakweli katika hilo ni lazima tuelewane
 
TsafuRD

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2013
Messages
1,781
Points
2,000

TsafuRD

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2013
1,781 2,000
Duh! Dunia ina maajabu, Mbunge ambaye Chama chake kina Mbunge mmoja anaongelea kukiondoa Madarakani Chama chenye Wabunge zaidi ya 200? Hivi tofauti ya Zito Kabwe na act yake na Cheyo na UDP yake ni ipi? Mimi nafikiri angejali kwanza kutetea kiti chake cha Ubunge kwa maana hata kama atarudi Bungeni, sijui.
kwa kweli. Zitto Kabwe ni msanii mnafiki bora wa karne hii.
 
ighaghe

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2013
Messages
1,360
Points
2,000

ighaghe

JF-Expert Member
Joined Mar 25, 2013
1,360 2,000
Duh! Dunia ina maajabu, Mbunge ambaye Chama chake kina Mbunge mmoja anaongelea kukiondoa Madarakani Chama chenye Wabunge zaidi ya 200? Hivi tofauti ya Zito Kabwe na act yake na Cheyo na UDP yake ni ipi? Mimi nafikiri angejali kwanza kutetea kiti chake cha Ubunge kwa maana hata kama atarudi Bungeni, sijui.
Signature yako ya life is suffering ni jibu la hii hoja yako.
 
mwakijembe

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2017
Messages
900
Points
1,000

mwakijembe

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2017
900 1,000
Ukifuata siasa za mtandaoni utachanganyikiwa kama Ruyagwa.
Huko nje ndio huko rais anatumia madaraka yake kuagiza vyombo viwahujumu wapinzani, na kwenye box la kura tunaona uhayawani wa wazi dhidi ya wapinzani ili ccm watangazwe washindi. Kwa maneno marahisi ccm haiko madarakani kwa ridhaa ya wananchi bali kwa mabavu ya vyombo vya dola.
 
mwakijembe

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2017
Messages
900
Points
1,000

mwakijembe

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2017
900 1,000
Hata ndoto za mchana nazo pia ni ndoto!

Alichokisema ni sawa na kusoma maneno yaliyoandikwa kwenye kanga!
Nikikumbuka nilivyoona mabox ya kura yakitolewa vituoni kwa uratibu wa jeshi la polisi ili kwenda kujaza kura za ccm, nikisikia mtu anasema ccm inashindana kwenye uchaguzi naona kinyaa.
 
Forum statistics

Threads 1,364,192
Members 520,667
Posts 33,307,961
Top