Zitto afunguka na kueleza hafanyi siasa za kufuata upepo, anasimamia kanuni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto afunguka na kueleza hafanyi siasa za kufuata upepo, anasimamia kanuni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nice 2, Jul 27, 2012.

 1. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hii ni sehemu ya majibu ya Zitto uko twitter:
  Aliambiwa: fredrooney: Zittokabwe my bro we need statement ukanushe hizi tuhuma kwamba ulipokea hongo kuwatetea mhando bungeni

  Akajibu: Zittokabwe: fredrooney sitatoa statement kwa mambo ya uzushi yanayosukumwa na agenda za kisiasa. Siku zote nasimamia ninayoamini. Sifuati upepo

  Akaambiwa: fredrooney: Zittokabwe ok nashukuru kwa msimamo wako lakini kwanini unadhani wanakuandama je ni nguvu yako kuelekea 2015

  Akajibu: Zittokabwe: fredrooney nadhani ni aina ya siasa zetu tu. siasa za kumaliza watu kwa kuzusha mambo yasiyo na ukweli. Hata hivyo "ukweli haufichiki"

  Akaendelea: Zittokabwe: AnnieTANZANIA walisema hivi hivi kwa CHC. Sitetei Mtu kwa kuhongwa. Natetea kanuni. And Mhando akikutwa na makosa, aadhibiwe fredrooney

  Amaa kweli nimekubali ZZK amekomaa kisiasa!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  hapo kwenye RED kakomaa wapi kama sio undumilakuwili?

  Who is Zitto? hivi unafikiri zitto anaweza kusadia nini?
   
 3. nice 2

  nice 2 JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 746
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Undumilakuwili kivipi mkuu? Tulia kwanza uongee taratibu... Zitto anaweza kusaidia nini katika nini?
   
 4. matumbo

  matumbo JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2012
  Joined: Jul 9, 2011
  Messages: 7,199
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  mkuu hii ishu ni ngumu sana...kama huijui vizuri ni bora utulie..ngoja tuendelee kusubiri huo ukweri lakini.
   
 5. Sober

  Sober JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 6, 2008
  Messages: 289
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ZZK mara nyingi namkubali kwa hoja zake, ila kwa hili nadhani na naamini amepotoka.

  Mi binafsi nilishangazwa sana kusikia kamati ya POAC ndiyo ya kwanza kutoa tamko la kutetea menejimenti ya TANESCO
  iliposimamishwa, hata kabla ya kamati ya Nishati na Madini. Lakini zaidi, kuona sasa hizi kamati zimekua kama sehemu ya watendaji wa serikali kwa kutaka kujihusisha kwenye kila uamuzi wa serikali, na hapohapo waje kuwasimamia bungeni. Nilihisi something is not right!

  Kusimamia kanuni BLINDLY hata pale ambapo maslahi ya nchi yanapobakwa hadharani, ni kukosa WELEDI na UZALENDO.

  Kama kweli anasimamia sheria na kanuni imekuaje juzi kwenye mjadala aliouzua Mh. Jaffo(Mb) wa sheria ya SSRA ya kuzuia fao la kujitoa aliunga mkono hoja, kutaka uamuzi wa SSRA upitiwe upya huku akijua SSRA ilikua inatimiza wajibu wake kwa kusimamia sheria, iliopitishwa na bunge hilihili.

  Busara ingekua akubali tu this time kachemka, we all make mistakes and learn from them!
   
 6. K

  KakindoMaster JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2012
  Joined: Dec 5, 2006
  Messages: 1,349
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  ZZK ni mkali kweli kweli nasmsifu
   
 7. Borat69

  Borat69 JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 2,536
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  Zitto ni MWANASIASA na sio KIONGOZI.
  Sifa moja ya MWANASIASA ni kuweka Maslahi yake mbele na kubadilika Kama kinyonga ili apate rizki yake.
  Kanuni gani anazofuata ZITTO ????
  Mbona hakuzifuata hizo Kanuni wakati waTanzania tunaburuzwa kwenye Giza !? Huna jipya rudi KIGOMA kapigwe chale za ulimi ili ujipange upya.
  Watu Kama Zitto ni saratani (Cancer) kwenye jamii na TAIFA.

  WATANZANIA tumuangalie kwa jicho la tatu huyu ZITTO na Wanasiasa wa aina yake.
   
 8. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Mfikishie ZZK ujumbe kwamba aachane na kuvimba kichwa na asaidiane na wenzake kujenga chama hadi katika maeneo ya vijijini, mwaka 2015 bado miaka 3 mbele. Akae chini aone kazi inayofanywa na Hechena Katibu wake, Mwikwabe, Lema na Milya, na Nanyaro wa Arusha. Siyo hao tu, pia hata umoja wa wakinamama CHADEMA-Morogoro kwa siku za hivi karibuni, na wengineo wengi. Hawa watu wamejitoa maisha yao kuhakikisha kwamba kwa rasilimali ndogo zilizopo CHADEMA wanafanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kwamba CHADEMA inafahamika mpaka vijijini. Huu siyo wakati muafaka kwake kukaa na kukinzana na wenzake ndani ya CHADEMA kwa maslahi binafsi badala ya kuunganisha nguvu na wenzake ili ukombozi ufikiwe. Kwani, kwa kazi kubwa inayofanywa na wana-CHADEMA kwasasa, ikifika mwaka 2015 na tukashindwa kuchukua nchi kwasababu tu ya tamaa au hulka hizi za kujiamini kupita kiasi badala ya kusaidiana na wenzako ili chama kisonge mbele, hili litakuwa ni pigo moja mbaya sana kwa mustakabali waukombozi wa nchi yetu.

  Pia ni bora mkampe ushauri mzuri Zitto, kwani mwelekeo wake siyo constructive in all ways.
   
 9. m

  manucho JF-Expert Member

  #9
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mawazo yako binafsi usifanye ni ya wote, 'Kakomaa kisiasa' hiyo ni wewe na akili yako kinachoangaliwa ni daily performance anatetea upumbavu wa kina mhando anapigwa chini hii ni CDM not CCM akitaka ahamie huko kwa magamba.

  Saa hizi mapema yote hii asubuhi hata hakujakucha vizuri yeye anakimbilia kupayuka Urais kama siyo PepO limetumwa nini hii ghasia, balaa.
  Makamanda wanapambana usiku na mchana piga uwa garagaza pori kwa pori kwa ajili ya kujenga chama yeye kakaa mjini eti URAIS. Hili ni balaa la kufukuzia baharini. Aliyeku2ma mwambie muanze Upya
   
 10. U

  Ubongo Silaha Senior Member

  #10
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 140
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Kwa mtazamo wangu haitoshi kwa Zitto kuziita tuhuma hizo uzushiZimesemewa Bungeni ambapo hapapaswi kutolewa kauli yoyote isiyo na ushahidiKwa sababu Zitto ameita ni uzushi na kwa sababu amedai anasimamia kanuni, aanze kwa kutumia kanuni za Bunge kudai mtoa tuhuma athibitishe au afute kauliKila mtu hukana tuhuma hata kama ni za kweliWatu walikana Richmond na Epa na BuzwagiNarudia haitoshi kwa Zitto kukana, aende mbele zaidi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. U

  Ubungo JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 1,239
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hizi ni double standards, bunge la April Chami aliwajibishwa kwa kushindwa kumsimamisha kazi Ekerege wa TBS kupisha uchunguzi, leo Mhandio wa TANESCO kasimamishwa kupisha uchunguzi baadhi ya wabunge hawataki, nadhani iko namna hapo.
   
 12. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #12
  Jul 27, 2012
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,176
  Trophy Points: 280
  Ukishasema sitatoa statement ushatoa statement, hawa watu vipi?
   
 13. B

  Bob G JF Bronze Member

  #13
  Jul 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Hasikii ZZK tumemshauri saana aache kutumika, awakemee hao ccm wanaompamba kwa uongo na kumvimbisha kichwa, afanye kazi asitafute sifa za kijinga, yeye ameacha ccm wamtumie na kufurahia kutumika, kumbuka ilivokuwa kwa Karamagi alimtetea na hata kumwandikia barua Rais kumlinda Karamagi, amekuja na Majenereta ya Downs anaishauri serikali inunue USed tena mitambo iliyoingia kifisadi, Wenzie wanapambana Arumeru yeye analopoka yake, haya Hili la Mhando yeye ZZK amejipeleka kimbelembele mpaka waungwana wakajiuliza kunani hapa huyu kijana!, Jamani huyu mtu amelikoroga mwenyewe hana budi kulinywa, Mi muda mwingine namwona kama mtoto mtukutu kama Balotel vile! akikua ataacha Jamani
   
 14. m

  manucho JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 3,410
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Yaani huyu this time hana lake, piga chini mazima
   
 15. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ushabiki wako tu huo hauna msingi wowote katika hili, hata bungeni wamenena.Sasa yeye si mjinga kukubali kama kala mlungula....... TUNA MUOMBA ATOE TAMKO NDO TUTAHAKIKI.AKI KAA KIMYA ANALAKE JAMBO
   
 16. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #16
  Jul 28, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,693
  Likes Received: 12,742
  Trophy Points: 280
  Zitto tunataka utoe tamko sio maandishi haya mepesi.
   
 17. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #17
  Jul 28, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  Mimi ni mwanachama wa cdm na pia ndani ya cdm zitto ni kati ya viongozi ninaemkubali, ila tatizo lake ni moja he is so ARROGANT kwa mafankio ya kisiasa aliyopata yaliyomfanya avimbe KICHWA na kuwa na dharau na kujiona mjuaji kama si bora kulko wenzake.
   
 18. A

  Africa_Spring JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2012
  Joined: Jun 16, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Bila shaka nice2 ndo zito mwenyewe amekuja humu jf kuji safisha.
   
 19. kisururu

  kisururu JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2012
  Joined: Jan 3, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ZZK kwakweli kama umepokea hongo ili umsafishe mtu hufai kabisa kua mwana mageuzi.kwa sasa hivi hatuwezi kukuhukumu ila tutakapojua ukweli unahusika nafikiri itakua muda muafaka wa kukutema kwenye hiki chama.
   
 20. M

  Mkirindi JF-Expert Member

  #20
  Jul 28, 2012
  Joined: Mar 2, 2011
  Messages: 3,335
  Likes Received: 950
  Trophy Points: 280
  Anaweza kusaidia Tan\zania na watanzania. he is a nationalistic and a clean one. "Dua za kuku hazimpati mwewe" Go Zitto Go
   
Loading...