Zitto afichua siri yake na Kikwete...

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
zitto_jk.jpg

Rais Kikwete na Zitto Kabwe

Na Mwandishi Wetu | Mwananchi | Novemba24 2012

MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe amefichua siri ya uhusiano wake na Rais Jakaya Kikwete kuwa, unatokana na kuheshimu mchango wake anaoutoa kwa taifa.

Kutokana heshima hiyo, Zitto anasema ndiyo maana Rais Kikwete hakufika jimboni kwake katika uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005 na mwaka 2010 kumnadi mgombe wa CCM.

Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema alisema hayo katika mahojiano maalum na Mtandao wa Jamii Forum juzi.

Mbunge huyo ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa Upinzani Bungeni, jana alilithibitishia gazeti hili kwamba alihojiwa na mtandao huo kwa saa nane.

"Kweli ni mahojiano baina yangu na Jamii Forum. Kwa Kfupi ni kwamba, yalikuwa mahojiano ya saa nane, kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa kumi jioni na walionihoji kwa njia ya mtandao walikuwa wakituma maswali na mimi nawajibu," alisema Zitto.

Alisema yeye na Rais Kikwete wana uhusiano nje ya siasa na hata siku moja hawajadili mambo ya vyama vyao wanapokutana na kwamba, Rais anaamini katika uzalendo wake.

Zitto alisema kutokana Rais Kikwete kuthamini mchango wake, ndiyo maana hajawahi kwenda kwenye jimbo lake kumfanyia kampeni mgombea wa chama chake cha CCM katika chaguzi za mwaka 2005 na 2010.

"Hatuna makubaliano yeyote, bali anaheshimu mchango wangu kwenye nchi yangu. Mwaka 2005 hakuja Kigoma Kaskazini na 2010 pia hakuja Kigoma Kaskazini," alisema.

Alisema kama ilivyo kwa wengine wenye uamuzi ya kuthamini kazi za wagombea wa vyama vingine, Rais Kikwete naye anayo haki ya kuheshimu na kuthamini kazi zake.

Aithdha, Zitto alisema anamheshimu Rais Kikwete kama mzee wake na kwamba, kuwaita kuwa wao ni marafiki ni kukosea.

"Kuita sisi ni marafiki ‘is understatement', yeye ni mzee wangu. Tunaheshimiana, lakini ninaiheshimu zaidi Tanzania na ninaipenda zaidi Tanzania," Zitto alisema.

Alichokifanya Rais Kikwete kutokuja katika jumbo langu si jambo geni, kwani hata vyama vingine vimewahi kuvifanya.

Alitoa mfano wa aliyekuwa mgombea wa urais kupitia Chadema katika uchaguzi mkuu mwaka 2005, Freeman Mbowe alipofika katika Jimbo la Musoma Mjini, alimpigia kampeni mgombea wa CUF.

Zitto alikumbusha kuwa na katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, aliyekuwa mgombea wa urais wa chama chake, Dk Willibrod Slaa alipofika jimbo la Kyela alimnadi mgombea wa CCM, Dk Harrison Mwakyembe kutokana na kutambua na kuheshimu mchango wake kwa taifa.

Uhusiano wa CCM

Kuhusu watu wanaomhusisha na CCM, mwanasiasa huyo alisema kuna kikundi kidogo cha watu wenye malengo mabaya dhidi yake ndio wanaoeneza uvumi huo.

"Wajue tu kwamba, hawawezi kuwadanganya Watanzania ambao wanafanya uamuzi wao si kutokana na propaganda, ila kutokana na matendo ya kila mmoja," alisema. 

Aliwaonya watu hao kuwa, hawawezi kummaliza yeye kisiasa bila kuiathiri Chadema kwani taswira yake imefungana na chama hicho.

Alisema: "Wanaoeneza sumu hiyo hawana nia njema na Chadema. Hawaelewi siasa. Maadui wanawachochea kwa kuwapa habari za uwongo na wao wanadhani watammaliza Zitto. Huwezi kummaliza Zitto bila kuiathiri Chadema. Hawatafanikiwa,"

Kuhusu kuwapo kwa utitiri wa vyama vya siasa nchini, Zitto alisema watu waachiwe kuanzisha vyama waanvyotaka, lakini baadaye vitajichuja na kubaki vyama viwili vyenye nguvu; Chadema na CCM.

Alisema vyama vitakavyobaki ni vile ambavyo vitakidhi matakwa ya wananchi na kwamba, hakuna haja ya kuweka sheria ya kuvifuta vyama vingine.

Zitto aliitabiria mabaya chama cha NCCR Mageuzi, akisema haoni kama kitaweza kitaendelea kuwapo.

Aliongeza kuwa, UDP hakiwezi kuwapo bila ya Mwenyekiti wake, John Cheyo na TLP hakiwezi kuwapo bila ya Mwenyekiti wake, Augustine Mrema.

"Sioni NCCR ikidumu. Sioni future (tumaini) ya UDP bila Cheyo na TLP bila Mrema," alisema.

Hata hivyo, alisema kuna uwezekano CCM kumeguka na kundi kubwa litakalotokana na tukio hilo likaunda chama kingine cha siasa ambacho kinaweza kuwa na nguvu zaidi hata ya Chadema.

Alisema baada ya uchaguzi wa 2015 tutaona mambo haya. "Tuache watu wawe huru kuunda vyama na vyenye nguvu vitabakia,"

Kuhusu tetesi kuwa amenzisha chama na Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, Zitto alisema hajawahi na wala hafikirii kuanzisha chama cha siasa.

Alisema chake chake ni Chadema na hataondoka kwenda chama kingine cha siasa na kushangaa kuona baadhi ya viongozi wa Chadema wanaamini uongo huo.

"Kinachonisikitisha ni kwamba, kuna viongozi wa Chadema wamekula sumu hii na bila woga wanaisema kana kwamba ni kweli," alisema

Ubunge wake
Zitto alirejea kauli yake aliyowahi kuitoa kwamba hatagombea ubunge katika jimbo la Kigoma Kaskazini na badala yake anataka kugombea urais kupitia cha hicho mwaka 2015.

Alisema ametangaza kutogombea ubunge, na anakiomba ridhaa ya chama chake kuwa mgombea urais na kuwa, hilo lisipowezekana atakuwa mpiga debe wa mgombea Urais.

Alisema hataki itokee yaliyotokea mwaka 2010 ambapo mgombea Urais alibaki mpweke kwani kila mtu alikwenda kugombea Ubunge.

Zitto alifafanua kwamba, Chadema kina viongozi wengi wanaoweza kupewa uongozi wa nchi na aliwataja baadhi yao kuwa ni Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, Katibu Mkuu Dk Slaa na mmoja wa makada wa Chadema, Dk Kitila Mkumbo.

"Wapo wengi sana ndani ya CHADEMA wenye sifa za kuwa Marais. Sina mashaka kabisa hilo," alisisitiza.

Aliongeza kuwa, ili Tanzania iwe salama ni lazima CCM ishindwe uchaguzi mkuu ujao.

Alibashiri kuwa, kama CCM kitashinda tena mwaka 2015, watu wengi hasa wanamageuzi watavunjika moyo na wengine wanaweza kabisa kukata tama.

"Njia pekee ya kuisadia CCM ili iweze kujipanga upya ni chenyewe kondoka madarakani. Chadema tuna nafasi kubwa ya kushinda na kuongoza dola. Muhimu chama kijipange na kuonekana kama chama kilicho tayari kushika dola. Tuyatende tunayoyasema na tujiimarishe zaidi," alisema Zitto.

Kuhusu demokrasia ndani ya Chadema, Zitto alisema chama hicho kina demokrasia ya aina yake na wanachama wanaridhika nayo.

"Tuna utaratibu mzuri sana wa kujieleza na kutetea hoja zetu ndani ya chama na baada ya watu wote kukubaliana tunahakikisha tunasimama wote kwa kauli moja sehemu zote tunapokiwakilisha chama. Sio katika kupanga safu za uongozi tu, bali katika maeneo yote,"alisema.

Nimependa jinsi JF ilivyokuwa recognized na vyombo vya habari karibu vyote after interview na AshaDii, big up sana kwa AshaDii na uongozi wa JF.

Pia natambua mchango wa Zitto katika kujibu kero na maswali ya watu mashabiki, waso mashabiki na wale wenye open mind.
 
Last edited by a moderator:
Ndio maana huwa sipotezi muda wangu kununuwa magazeti ya Tanzania, JF inanitosha sana kuwa informed.
 
  • Thanks
Reactions: kui
sikushangai mh ZITTO ,hiyo ndiyo falsafa yako. Tanzania kwanza big up nakuamini saaana, nakufatilia saaana , jamii inaanza kukuelewa, wewe si mtu wa propaganda. baada ya mahojiano hayo wale waliokuwa wanakutakia mabaya kisiasa sasa wamekuelewa labda wakaze shingo zao ila nawaonya zitavunjika.
 
Dogo yupo makini naamini anajiandaa na uraisi 2020 anajua, akiambatana na mgombea uraisi huo ndio utakuwa wakati wa yeye kujiuza upya kwa ajili ya 2020, na pia ili aweze kutembea na kujiuza nchi nzima basi hana budi kuacha ubunge na afanye kazi ya chama kuanzia 2o15 hadi 2020 atakapo gombea.

Kila la heri Zitto.
 
Aliwaonya watu hao kuwa, hawawezi kummaliza yeye kisiasa bila kuiathiri Chadema kwani taswira yake imefungana na chama hicho.

Alisema: "Wanaoeneza sumu hiyo hawana nia njema na Chadema. Hawaelewi siasa. Maadui wanawachochea kwa kuwapa habari za uwongo na wao wanadhani watammaliza Zitto. Huwezi kummaliza Zitto bila kuiathiri Chadema. Hawatafanikiwa,"
Kweli ZZK ameongea mantiki! lakini hapo penye nyekundu sikubaliani. CDM au chama chochote chenye nguvu hakitakiwi kiwe na "indispensables".

Vile vile hayo ya kusema ni uzalendo wake ni propaganda za kitoto. Tunataka mfano ni wapi TZ toka vyama vya upinzani vianze CCM imewahi kusifu "uzalendo" wa wapinzani. Ni uwongo mchana kweupe leta mwingine! Dr Slaa nguvu nyingi zinatumika pamoja na TISS kumwondoa! Ni nani mzalendo kati ya Tundu Lissu na ZZK!?

JK aliwaomba wakazi wa singida wamnyime TL uwakilishi kwa gharama yoyote!! Come again ZZK come again son and tell us what is between and Magamba.
 
Hongera sana Zitto kwa maelezo mujarabu.

Nimependa ulivyofunguka na kutanabaisha uelewa wako wa siasa za ndani na nje ya chadema, binafsi sioni tatizo ukigombea uraisi 2015 maana ni haki yako kikatiba, lakini nimefurahi kuona kuwa unatambua uwepo wa viongozi wengine ndani ya chadema ambao pia wanao uzalendo unaotosha kuwa raisi wa Tanzania. Huu ni ukomavu mkubwa kisiasa.

Maelezo yako Zitto ni changamoto kwa vijana wanaopenda kuingia kwenye siasa, kimsingi unawashawishi vijana waingie kwenye siasa za HOJA zenye uzalendo na nchi yetu, majibu uliyotoa hanaya chembe ya vijembe bali reflection za maana zenye lengo la kukosoa ili kujenga.

Wakuu wa JF kama mnaweza, endeleeni kufanya interviews kama hizi kwa viongozi (hasa vijana) wa vyama vingine ikiwamo CCM, UDP,CUF nk, hii itasaidia sana kuakisi fikra za viongozi tulionao, pengine majibu yao yatatoa mwanga wa "kwa nini Tanzania ni masikini pamoja na raslimali ya asili iliyopo"
 
ole wa siasa batili zimnyonyazo mwananchi!bwana ameapa kuiadhibu nchi kwa hasira ya upanga wake!tubuni asema bwana!
 
Attachments

  • worlds-collision_2.pdf
    1 MB · Views: 64
  • 66001001-66001020.mp3
    761.5 KB · Views: 43
watanzania tunataka mapinduzi ya kweli siyo ya kinafiki..hicho unachofanya zito ni unafiki wa hali ya juu na usifikiri viongozi, wapenzi na wakereketwa wa chadema hatufahamu hivyo...zito inakuwaje uwasiliane na zoka mkurugenzi msaidizi usalama wa taifa kitego cha siasa kipidi cha uchaguzi.,na kwann jk asimnadi mgombea kwenye jimbo lako,..unakumbuka zito jinssi ulivyokuwa ukimnadi mgombea chanel 10 dr bilali kuwa anafaa kuwa makamu wa raisi.
Sisi wanatanzania mtuonee huruma jinsi tunavyoteseka na hiyo ccm na kwahiyo tunaihitaji mapinduzi ya ukweli.

Zito tunafahamu jinsi unavyohonga waandishi ili uendelee kupata hiyo cheap popularity lakini kumbuka bro zito ni maarufu kwakuwa upo chadema na hata kama ukiondoka tunayo watu wengi kibao..na kumbuka umaarufu wako utaisha gafla ukiondoka chadema, zito hukubaliki kama unavyodaganywa na wapambe wako . Na usijidanganye kwamba kufa kwako kisiasa ni kuua chadema kama mawazo hayo futa...zito hujawahi kuwa juu ya chadema na siyo muhimu kama unavyodhani.

Yaani kweli watanzania siye vichwa vyetu maji..,INAKUWAJE MWENYEKITI WA CCM AWE RAFIKI YAKO.,km kikwete anapenda uzarendo wako kwanini asikuombe uingie chama chake, mbona lema aliombwa na huyo na friend wako wa ikulu na alikataa..ETI ATUONGELEI SIASA...ivi ni kweli viongozi wa SIMBA na YANGA wakikutana hawaongelei mpira? tunajua unataka unataka uwe kama wassira ili uhame chadema uende ccm ukapewe uwaziri.

kikwete ni mnafiki km hufahamu muulize lowasa atakuambia, marafiki wawili EL na JK ambao waliingia ccm mwako 1975 wakati mama yako akiwa na mimba yako.lakini leo nafikiri umejua kilichompata lowasa. Kwani lowasa alichoiba kikwete hakuhusika,zito achakuwafake watanzania.unapenda.badala kipindi hichi wewe ungekuwa ndio mstari wa mbele kuwasaidia mwenyekiti na katibu kupanga mikakati ya m4c..kujiunga na chama tokea chuoni siyo ndo mwenye chama.

kama unamalengo ya kuharibu chadema ni bora ufe kimwili..

be blessed poor zito zuberi kabwe
 
Ndio maana huwa sipotezi muda wangu kununuwa magazeti ya Tanzania, JF inanitosha sana kuwa informed.
hakika mkuu,hata mimi huwa sipotezi hela yangu kununua magazeti ambayo waandishi wake wanasubiri kutafuniwa habari na JF.VIVA JF
 
Kweli ZZK ameongea mantiki! lakini hapo penye nyekundu sikubaliani. CDM au chama chochote chenye nguvu hakitakiwi kiwe na "indispensables".

Vile vile hayo ya kusema ni uzalendo wake ni propaganda za kitoto. Tunataka mfano ni wapi TZ toka vyama vya upinzani vianze CCM imewahi kusifu "uzalendo" wa wapinzani. Ni uwongo mchana kweupe leta mwingine! Dr Slaa nguvu nyingi zinatumika pamoja na TISS kumwondoa! Ni nani mzalendo kati ya Tundu Lissu na ZZK!?

JK aliwaomba wakazi wa singida wamnyime TL uwakilishi kwa gharama yoyote!! Come again ZZK come again son and tell us what is between and Magamba.

Tukikuondoa mkono hatujaathiri mwili wako?
 
Zitto unahitajika kuacha ubunge kweli ili waTZ wakupime uzalendo wako nje ya bunge kwa miaka5 kama anavyopimwa sasa Dr.SLAA. Hii itatoa fursa kwa umma kufanya maamuzi sahihi kama unafaa uwe rais 2025 au la.
 
watanzania tunataka mapinduzi ya kweli siyo ya kinafiki..hicho unachofanya zito ni unafiki wa hali ya juu na usifikiri viongozi, wapenzi na wakereketwa wa chadema hatufahamu hivyo...zito inakuwaje uwasiliane na zoka mkurugenzi msaidizi usalama wa taifa kitego cha siasa kipidi cha uchaguzi.,na kwann jk asimnadi mgombea kwenye jimbo lako,..unakumbuka zito jinssi ulivyokuwa ukimnadi mgombea chanel 10 dr bilali kuwa anafaa kuwa makamu wa raisi.
Sisi wanatanzania mtuonee huruma jinsi tunavyoteseka na hiyo ccm na kwahiyo tunaihitaji mapinduzi ya ukweli.

Zito tunafahamu jinsi unavyohonga waandishi ili uendelee kupata hiyo cheap popularity lakini kumbuka bro zito ni maarufu kwakuwa upo chadema na hata kama ukiondoka tunayo watu wengi kibao..na kumbuka umaarufu wako utaisha gafla ukiondoka chadema, zito hukubaliki kama unavyodaganywa na wapambe wako . Na usijidanganye kwamba kufa kwako kisiasa ni kuua chadema kama mawazo hayo futa...zito hujawahi kuwa juu ya chadema na siyo muhimu kama unavyodhani.

Yaani kweli watanzania siye vichwa vyetu maji..,INAKUWAJE MWENYEKITI WA CCM AWE RAFIKI YAKO.,km kikwete anapenda uzarendo wako kwanini asikuombe uingie chama chake, mbona lema aliombwa na huyo na friend wako wa ikulu na alikataa..ETI ATUONGELEI SIASA...ivi ni kweli viongozi wa SIMBA na YANGA wakikutana hawaongelei mpira? tunajua unataka unataka uwe kama wassira ili uhame chadema uende ccm ukapewe uwaziri.

kikwete ni mnafiki km hufahamu muulize lowasa atakuambia, marafiki wawili EL na JK ambao waliingia ccm mwako 1975 wakati mama yako akiwa na mimba yako.lakini leo nafikiri umejua kilichompata lowasa. Kwani lowasa alichoiba kikwete hakuhusika,zito achakuwafake watanzania.unapenda.badala kipindi hichi wewe ungekuwa ndio mstari wa mbele kuwasaidia mwenyekiti na katibu kupanga mikakati ya m4c..kujiunga na chama tokea chuoni siyo ndo mwenye chama.

kama unamalengo ya kuharibu chadema ni bora ufe kimwili..

be blessed poor zito zuberi kabwe
Mkuu haya ndiyo mawazo chambuzi! Siyo hao walioingia kwenye mkumbo wa kuhadaika na majibu ya Kiswahili mrefu mrefu!!
 
Ndio maana huwa sipotezi muda wangu kununuwa magazeti ya Tanzania, JF inanitosha sana kuwa informed.

Umenena mkuu, ila mwananchi lina siri nzito na Zitto!

Tuanchane na hilo!

Hongera jf,

Binafsi kutoka moyoni ZITTO ni mnafiki na muuongo mkubwa!

Amejaribu kutumia jf na kulaghai watu nashanga kweli watu wanaojiita GT wamelaghaika na wanamshangilia!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom