MamaParoko
JF-Expert Member
- Jan 14, 2008
- 463
- 60
na Kulwa Karedia na Salehe Mohamed
NCHI wahisani zimetishia kutochangia bajeti ya nchi ya mwaka 2008/2009 kama serikali haitachukua hatua kali dhidi ya mafisadi waliochota mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na mkataba wa kinyonyaji wa kufua umeme wa dharura kati ya serikali na Kampuni ya kitapeli ya Richmond.
Hayo yalibainishwa jana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) wakati akichangia katika kikao cha mwongozo wa kutayarisha mipango na bajeti ya serikali kwa kipindi cha mwaka 2008/2009 kwenye Ukumbi wa DICC, Dar es Salaam, kauli ambayo ilimlazimisha Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo kukiri.
Zitto, mwanasiasa aliyeibua hoja kuhusu utata uliozunguka kusainiwa kwa mkataba wa mgodi wa madini wa Buzwagi katikati ya mwaka jana na kusababisha mtafaruku mkubwa nchini, alisema wahisani wameonyesha nia hiyo ya kutochangia kiasi cha fedha kama serikali haitachukua hatua kali dhidi ya mafisadi.
"Mheshimiwa mwenyekiti, ningependa kupata maelezo kwa kuwa, kuna habari kwamba mwaka huu wahisani wameonyesha nia ya kutochangia kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya bajeti yetu, je tatizo nini?" alihoji Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema.
Alisema serikali iliomba kiasi cha sh bilioni 970 kwa ajili ya kuchangia bajeti ijayo, lakini wamegoma baada ya kutoa masharti kwa serikali, na kwamba yasipotekelezwa kuna uwezekano mdogo wa kuchangiwa.
Mbunge huyo alisema, moja ya sharti lililotolewa ni kwamba, serikali inatakiwa kuhakikisha inawakamata wahusika walioiba fedha kwenye Akaunti ya EPA na kuwataja majina, kisha kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.
Alisema sharti la pili lililotolewa na wahisani hao ni kwamba, wameitaka serikali kuhakikisha inamaliza suala la mpasuko wa kisiasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).
"Wahisani wameonekana kutaka suala la mazungumzo kati ya CCM na CUF limalizike haraka, kwa vile limeonekana kuwa tatizo kwa muda sasa," alisema Zitto.
Akijibu hoja hizo za Zitto, Waziri Mkulo, alisema ni kweli wahisani walishtushwa na hali ya mambo ilivyokuwa nchini, na kuonyesha nia ya kutochangia bajeti kutokana na ufisadi katika EPA na Richmond.
Alisema si wahisani peke yake walioshtushwa na hali hiyo, bali hata serikali nayo ilipata mshtuko huo, lakini ilijipanga vilivyo na kuwawajibisha watendaji wote waliohusika na kashfa hizo ambazo zimelitia taifa aibu na kukwamisha maendeleo.
Mkulo alisema, wahisani walitaka kuona hatua zitakazochukuliwa na serikali dhidi ya watu waliohusika na ufisadi huo ili waendelee kutoa misaada ya maendeleo nchini pamoja na kuchangia bajeti ya taifa ambayo asilimia 40 inategemea fedha kutoka kwao.
"Kwa kusema kweli wahisani walisita kutoa misaada yao au kuahidi watatuchangia nini katika bajeti yetu, lakini mambo hivi sasa yanakwenda vizuri," alisema Mkulo.
Alisema uwazi wa serikali katika kuwashughulikia watu waliohusika na kashfa za Richmond na EPA ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kwa kiasi kikubwa umechangia kurudisha imani kwa wafadhili hao.
Alisema mazungumzo kati ya serikali na wahisani hivi sasa ni mazuri na mwezi ujao wanatarajia kutangaza ahadi za wahisani ambao wanatarajia kuchangia bajeti ya Tanzania inayotegemewa kuwasilishwa bungeni mwezi Juni.
"Ili kuuthibitishia umma juu ya uhusiano mzuri unaoendelea baina yetu, mwezi ujao nitatangaza ahadi za nchi 16 ambazo ni wahisani wetu wanaotusaidia katika bajeti yetu," alisema Mkulo.
Alisema baadhi ya wahisani wana uhusiano wa karibu na wapinzani ambao huwapa taarifa za hali ya mambo hapa nchini na kuwaambia wasitoe fedha mpaka serikali itekeleze baadhi ya mambo ambayo wakati mwingine huanzishwa na wapinzani.
Waziri huyo alisema taarifa wanazozipata wahisani hao kutoka kwa jamaa zao huzichukulia ndiyo ukweli wa mambo na hivyo kutotoa misaada mpaka masharti hayo yatekelezwe.
"Wahisani wana uhusiano na vyama vya upinzani na huwa wanatusaidia kwa kuwasikiliza wapinzani, hivyo wanapopewa hoja na upinzani hutaka zifanyiwe kazi na serikali ili watoe fedha zao kinyume na hapo mambo huwa magumu," alisema Mkulo.
Aidha, alisema bajeti ya mwaka huu inaweza kuwa nzuri zaidi baada ya wahisani wengi kuonyesha nia ya kuchangia, hivyo mipango mingi ya maendeleo inaweza kufanyika na hivyo kupunguza umasikini unaozidi kushamiri siku hadi siku.
Wakichangia katika kikao hicho, wabunge waliishambulia serikali kwa kile walichosema kuwa imekuwa na urasimu mkubwa katika suala zima la mikataba.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Fedha, Dk. Abdallah Kigoda alisema anasikitishwa na hatua ya serikali kuvunja Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji na kuiunganisha na Wizara ya Fedha hatua ambayo alisema itasababisha upangaji wa mipango kuwa mgumu.
"Mwenyekiti wizara hii ndiyo ilikuwa nguzo yetu ya kupanga mipango, sasa imeunganishwa, nina wasiwasi kwamba suala zima la mipango halionekani katika mwelekeo huu wa bajeti, kwani limeguswa kidogo sana," alisema Kigoda.
Alitaka wataalamu kutoka serikalini kufanya tathimini ya kupungua kwa wawekezaji wa kigeni, kwani hali hiyo imesababisha serikali kukosa mapato.
Mbunge wa Mchinga, Mudhihir Mudhihir (CCM), alilia na serikali kwa kitendo cha kuzalisha gesi ya Songo Songo katika mikoa ya kusini kisha kuhamishia Dar es Salaam.
"Gesi inazalishwa katika mikoa yetu ya kusini, lakini wananchi wameendelea kubaki kwenye giza na tunaona mambo yote yanafanyika Dar es Salaam," alisema Mudhihir.
Alisema kama Bunge halitachukua hatua zinazostahili, kuna kila sababu kikao kijacho wabunge wote wanaotoka mikoa ya Mtwara na Lindi watafute mbeleko ya kuwabeba kutokana na kuhojiwa kila wakati na wananchi.
Mbunge wa Kwela, Chrisant Mzindakaya (CCM) alisema ni aibu na fedheha kubwa kwa mawaziri kupokea chakula cha msaada kutoka nje wakati nchi ina uwezo wa kujitegemea.
"Nashangazwa na hatua ya waziri kupokea chakula bandarini pale, hii ni aibu, serikali yetu inapaswa kufanya biashara kwani duniani serikali zote zinafanya biashara, lakini Tanzania kazi yake ni kuchimba mashimo… jamani nani katuroga?"alisema Mzindakaya na kuhoji.
Aliwataka mawaziri kujiangalia upya katika utendaji kazi wao, na wasibweteke kupeperusha bendera kwenye magari ya kifahari.
Mbunge wa Muleba Kusini, Willson Masilingi (CCM) alilishauri Bunge kufuta ushuru wa magari na pikipiki kwani umekuwa kero kubwa kwa Watanzania licha ya vyombo hivyo kuwa mkombozi wa watu wa chini. Aidha, alisema ni vema serikali ikaboresha mishahara ya wafanyakazi ambao wamekuwa wakilipwa fedha kidogo ambazo haziwawezeshi kumudu gharama za maisha ambazo hupanda kila kukicha. Aliitaka serikali kuanzisha benki ya wakulima ambayo itakuwa ikiwasaidia wakulima katika shughuli zao na hatimaye kunyanyua kilimo ambacho ndiyo uti wa mgongo wa Tanzania.