Zitto Afichua Siri Nzito

MamaParoko

JF-Expert Member
Jan 14, 2008
463
60
na Kulwa Karedia na Salehe Mohamed

NCHI wahisani zimetishia kutochangia bajeti ya nchi ya mwaka 2008/2009 kama serikali haitachukua hatua kali dhidi ya mafisadi waliochota mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na mkataba wa kinyonyaji wa kufua umeme wa dharura kati ya serikali na Kampuni ya kitapeli ya Richmond.

Hayo yalibainishwa jana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) wakati akichangia katika kikao cha mwongozo wa kutayarisha mipango na bajeti ya serikali kwa kipindi cha mwaka 2008/2009 kwenye Ukumbi wa DICC, Dar es Salaam, kauli ambayo ilimlazimisha Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo kukiri.

Zitto, mwanasiasa aliyeibua hoja kuhusu utata uliozunguka kusainiwa kwa mkataba wa mgodi wa madini wa Buzwagi katikati ya mwaka jana na kusababisha mtafaruku mkubwa nchini, alisema wahisani wameonyesha nia hiyo ya kutochangia kiasi cha fedha kama serikali haitachukua hatua kali dhidi ya mafisadi.

"Mheshimiwa mwenyekiti, ningependa kupata maelezo kwa kuwa, kuna habari kwamba mwaka huu wahisani wameonyesha nia ya kutochangia kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya bajeti yetu, je tatizo nini?" alihoji Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema.

Alisema serikali iliomba kiasi cha sh bilioni 970 kwa ajili ya kuchangia bajeti ijayo, lakini wamegoma baada ya kutoa masharti kwa serikali, na kwamba yasipotekelezwa kuna uwezekano mdogo wa kuchangiwa.

Mbunge huyo alisema, moja ya sharti lililotolewa ni kwamba, serikali inatakiwa kuhakikisha inawakamata wahusika walioiba fedha kwenye Akaunti ya EPA na kuwataja majina, kisha kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Alisema sharti la pili lililotolewa na wahisani hao ni kwamba, wameitaka serikali kuhakikisha inamaliza suala la mpasuko wa kisiasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).

"Wahisani wameonekana kutaka suala la mazungumzo kati ya CCM na CUF limalizike haraka, kwa vile limeonekana kuwa tatizo kwa muda sasa," alisema Zitto.

Akijibu hoja hizo za Zitto, Waziri Mkulo, alisema ni kweli wahisani walishtushwa na hali ya mambo ilivyokuwa nchini, na kuonyesha nia ya kutochangia bajeti kutokana na ufisadi katika EPA na Richmond.

Alisema si wahisani peke yake walioshtushwa na hali hiyo, bali hata serikali nayo ilipata mshtuko huo, lakini ilijipanga vilivyo na kuwawajibisha watendaji wote waliohusika na kashfa hizo ambazo zimelitia taifa aibu na kukwamisha maendeleo.

Mkulo alisema, wahisani walitaka kuona hatua zitakazochukuliwa na serikali dhidi ya watu waliohusika na ufisadi huo ili waendelee kutoa misaada ya maendeleo nchini pamoja na kuchangia bajeti ya taifa ambayo asilimia 40 inategemea fedha kutoka kwao.

"Kwa kusema kweli wahisani walisita kutoa misaada yao au kuahidi watatuchangia nini katika bajeti yetu, lakini mambo hivi sasa yanakwenda vizuri," alisema Mkulo.

Alisema uwazi wa serikali katika kuwashughulikia watu waliohusika na kashfa za Richmond na EPA ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kwa kiasi kikubwa umechangia kurudisha imani kwa wafadhili hao.

Alisema mazungumzo kati ya serikali na wahisani hivi sasa ni mazuri na mwezi ujao wanatarajia kutangaza ahadi za wahisani ambao wanatarajia kuchangia bajeti ya Tanzania inayotegemewa kuwasilishwa bungeni mwezi Juni.
"Ili kuuthibitishia umma juu ya uhusiano mzuri unaoendelea baina yetu, mwezi ujao nitatangaza ahadi za nchi 16 ambazo ni wahisani wetu wanaotusaidia katika bajeti yetu," alisema Mkulo.

Alisema baadhi ya wahisani wana uhusiano wa karibu na wapinzani ambao huwapa taarifa za hali ya mambo hapa nchini na kuwaambia wasitoe fedha mpaka serikali itekeleze baadhi ya mambo ambayo wakati mwingine huanzishwa na wapinzani.

Waziri huyo alisema taarifa wanazozipata wahisani hao kutoka kwa jamaa zao huzichukulia ndiyo ukweli wa mambo na hivyo kutotoa misaada mpaka masharti hayo yatekelezwe.

"Wahisani wana uhusiano na vyama vya upinzani na huwa wanatusaidia kwa kuwasikiliza wapinzani, hivyo wanapopewa hoja na upinzani hutaka zifanyiwe kazi na serikali ili watoe fedha zao kinyume na hapo mambo huwa magumu," alisema Mkulo.

Aidha, alisema bajeti ya mwaka huu inaweza kuwa nzuri zaidi baada ya wahisani wengi kuonyesha nia ya kuchangia, hivyo mipango mingi ya maendeleo inaweza kufanyika na hivyo kupunguza umasikini unaozidi kushamiri siku hadi siku.

Wakichangia katika kikao hicho, wabunge waliishambulia serikali kwa kile walichosema kuwa imekuwa na urasimu mkubwa katika suala zima la mikataba.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Fedha, Dk. Abdallah Kigoda alisema anasikitishwa na hatua ya serikali kuvunja Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji na kuiunganisha na Wizara ya Fedha hatua ambayo alisema itasababisha upangaji wa mipango kuwa mgumu.

"Mwenyekiti wizara hii ndiyo ilikuwa nguzo yetu ya kupanga mipango, sasa imeunganishwa, nina wasiwasi kwamba suala zima la mipango halionekani katika mwelekeo huu wa bajeti, kwani limeguswa kidogo sana," alisema Kigoda.

Alitaka wataalamu kutoka serikalini kufanya tathimini ya kupungua kwa wawekezaji wa kigeni, kwani hali hiyo imesababisha serikali kukosa mapato.

Mbunge wa Mchinga, Mudhihir Mudhihir (CCM), alilia na serikali kwa kitendo cha kuzalisha gesi ya Songo Songo katika mikoa ya kusini kisha kuhamishia Dar es Salaam.

"Gesi inazalishwa katika mikoa yetu ya kusini, lakini wananchi wameendelea kubaki kwenye giza na tunaona mambo yote yanafanyika Dar es Salaam," alisema Mudhihir.

Alisema kama Bunge halitachukua hatua zinazostahili, kuna kila sababu kikao kijacho wabunge wote wanaotoka mikoa ya Mtwara na Lindi watafute mbeleko ya kuwabeba kutokana na kuhojiwa kila wakati na wananchi.

Mbunge wa Kwela, Chrisant Mzindakaya (CCM) alisema ni aibu na fedheha kubwa kwa mawaziri kupokea chakula cha msaada kutoka nje wakati nchi ina uwezo wa kujitegemea.

"Nashangazwa na hatua ya waziri kupokea chakula bandarini pale, hii ni aibu, serikali yetu inapaswa kufanya biashara kwani duniani serikali zote zinafanya biashara, lakini Tanzania kazi yake ni kuchimba mashimo… jamani nani katuroga?"alisema Mzindakaya na kuhoji.

Aliwataka mawaziri kujiangalia upya katika utendaji kazi wao, na wasibweteke kupeperusha bendera kwenye magari ya kifahari.

Mbunge wa Muleba Kusini, Willson Masilingi (CCM) alilishauri Bunge kufuta ushuru wa magari na pikipiki kwani umekuwa kero kubwa kwa Watanzania licha ya vyombo hivyo kuwa mkombozi wa watu wa chini. Aidha, alisema ni vema serikali ikaboresha mishahara ya wafanyakazi ambao wamekuwa wakilipwa fedha kidogo ambazo haziwawezeshi kumudu gharama za maisha ambazo hupanda kila kukicha. Aliitaka serikali kuanzisha benki ya wakulima ambayo itakuwa ikiwasaidia wakulima katika shughuli zao na hatimaye kunyanyua kilimo ambacho ndiyo uti wa mgongo wa Tanzania.
 
Nadhani pressure toka nje ndo itawatia adabu hawa watu otherwise tunavyolalamika kila siku wao wanaona sisi wehu.
As result mtu kaiba bado mnaleta usanii mara oooh,mara eeeeeeeeeeeh.
Mbaya zaidi mhalifu anatandikiwa Red Carpet,ni dharau kubwa sana hii.

External Pressure keep it up as it is worthless kuwachangia watu ambao wanafuja pesa za umma
 
mnataka tanzania ipi? tanzania inayohukumu wake kwa utashi na hisia au sheria?

tusiwe wafata hewa
 
Zitto afichua siri

na Kulwa Karedia na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

NCHI wahisani zimetishia kutochangia bajeti ya nchi ya mwaka 2008/2009 kama serikali haitachukua hatua kali dhidi ya mafisadi waliochota mabilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) na mkataba wa kinyonyaji wa kufua umeme wa dharura kati ya serikali na Kampuni ya kitapeli ya Richmond.

Hayo yalibainishwa jana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema) wakati akichangia katika kikao cha mwongozo wa kutayarisha mipango na bajeti ya serikali kwa kipindi cha mwaka 2008/2009 kwenye Ukumbi wa DICC, Dar es Salaam, kauli ambayo ilimlazimisha Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo kukiri.

Zitto, mwanasiasa aliyeibua hoja kuhusu utata uliozunguka kusainiwa kwa mkataba wa mgodi wa madini wa Buzwagi katikati ya mwaka jana na kusababisha mtafaruku mkubwa nchini, alisema wahisani wameonyesha nia hiyo ya kutochangia kiasi cha fedha kama serikali haitachukua hatua kali dhidi ya mafisadi.

"Mheshimiwa mwenyekiti, ningependa kupata maelezo kwa kuwa, kuna habari kwamba mwaka huu wahisani wameonyesha nia ya kutochangia kiasi chochote cha fedha kwa ajili ya bajeti yetu, je tatizo nini?" alihoji Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema.

Alisema serikali iliomba kiasi cha sh bilioni 970 kwa ajili ya kuchangia bajeti ijayo, lakini wamegoma baada ya kutoa masharti kwa serikali, na kwamba yasipotekelezwa kuna uwezekano mdogo wa kuchangiwa.

Mbunge huyo alisema, moja ya sharti lililotolewa ni kwamba, serikali inatakiwa kuhakikisha inawakamata wahusika walioiba fedha kwenye Akaunti ya EPA na kuwataja majina, kisha kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria.

Alisema sharti la pili lililotolewa na wahisani hao ni kwamba, wameitaka serikali kuhakikisha inamaliza suala la mpasuko wa kisiasa kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF).

"Wahisani wameonekana kutaka suala la mazungumzo kati ya CCM na CUF limalizike haraka, kwa vile limeonekana kuwa tatizo kwa muda sasa," alisema Zitto.

Akijibu hoja hizo za Zitto, Waziri Mkulo, alisema ni kweli wahisani walishtushwa na hali ya mambo ilivyokuwa nchini, na kuonyesha nia ya kutochangia bajeti kutokana na ufisadi katika EPA na Richmond.

Alisema si wahisani peke yake walioshtushwa na hali hiyo, bali hata serikali nayo ilipata mshtuko huo, lakini ilijipanga vilivyo na kuwawajibisha watendaji wote waliohusika na kashfa hizo ambazo zimelitia taifa aibu na kukwamisha maendeleo.

Mkulo alisema, wahisani walitaka kuona hatua zitakazochukuliwa na serikali dhidi ya watu waliohusika na ufisadi huo ili waendelee kutoa misaada ya maendeleo nchini pamoja na kuchangia bajeti ya taifa ambayo asilimia 40 inategemea fedha kutoka kwao.

"Kwa kusema kweli wahisani walisita kutoa misaada yao au kuahidi watatuchangia nini katika bajeti yetu, lakini mambo hivi sasa yanakwenda vizuri," alisema Mkulo.

Alisema uwazi wa serikali katika kuwashughulikia watu waliohusika na kashfa za Richmond na EPA ikiwa ni pamoja na uamuzi wa kujiuzulu kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kwa kiasi kikubwa umechangia kurudisha imani kwa wafadhili hao.

Alisema mazungumzo kati ya serikali na wahisani hivi sasa ni mazuri na mwezi ujao wanatarajia kutangaza ahadi za wahisani ambao wanatarajia kuchangia bajeti ya Tanzania inayotegemewa kuwasilishwa bungeni mwezi Juni.

"Ili kuuthibitishia umma juu ya uhusiano mzuri unaoendelea baina yetu, mwezi ujao nitatangaza ahadi za nchi 16 ambazo ni wahisani wetu wanaotusaidia katika bajeti yetu," alisema Mkulo.

Alisema baadhi ya wahisani wana uhusiano wa karibu na wapinzani ambao huwapa taarifa za hali ya mambo hapa nchini na kuwaambia wasitoe fedha mpaka serikali itekeleze baadhi ya mambo ambayo wakati mwingine huanzishwa na wapinzani.

Waziri huyo alisema taarifa wanazozipata wahisani hao kutoka kwa jamaa zao huzichukulia ndiyo ukweli wa mambo na hivyo kutotoa misaada mpaka masharti hayo yatekelezwe.

"Wahisani wana uhusiano na vyama vya upinzani na huwa wanatusaidia kwa kuwasikiliza wapinzani, hivyo wanapopewa hoja na upinzani hutaka zifanyiwe kazi na serikali ili watoe fedha zao kinyume na hapo mambo huwa magumu," alisema Mkulo.

Aidha, alisema bajeti ya mwaka huu inaweza kuwa nzuri zaidi baada ya wahisani wengi kuonyesha nia ya kuchangia, hivyo mipango mingi ya maendeleo inaweza kufanyika na hivyo kupunguza umasikini unaozidi kushamiri siku hadi siku.

Wakichangia katika kikao hicho, wabunge waliishambulia serikali kwa kile walichosema kuwa imekuwa na urasimu mkubwa katika suala zima la mikataba.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi na Fedha, Dk. Abdallah Kigoda alisema anasikitishwa na hatua ya serikali kuvunja Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji na kuiunganisha na Wizara ya Fedha hatua ambayo alisema itasababisha upangaji wa mipango kuwa mgumu.

"Mwenyekiti wizara hii ndiyo ilikuwa nguzo yetu ya kupanga mipango, sasa imeunganishwa, nina wasiwasi kwamba suala zima la mipango halionekani katika mwelekeo huu wa bajeti, kwani limeguswa kidogo sana," alisema Kigoda.

Alitaka wataalamu kutoka serikalini kufanya tathimini ya kupungua kwa wawekezaji wa kigeni, kwani hali hiyo imesababisha serikali kukosa mapato.

Mbunge wa Mchinga, Mudhihir Mudhihir (CCM), alilia na serikali kwa kitendo cha kuzalisha gesi ya Songo Songo katika mikoa ya kusini kisha kuhamishia Dar es Salaam.

"Gesi inazalishwa katika mikoa yetu ya kusini, lakini wananchi wameendelea kubaki kwenye giza na tunaona mambo yote yanafanyika Dar es Salaam," alisema Mudhihir.

Alisema kama Bunge halitachukua hatua zinazostahili, kuna kila sababu kikao kijacho wabunge wote wanaotoka mikoa ya Mtwara na Lindi watafute mbeleko ya kuwabeba kutokana na kuhojiwa kila wakati na wananchi.

Mbunge wa Kwela, Chrisant Mzindakaya (CCM) alisema ni aibu na fedheha kubwa kwa mawaziri kupokea chakula cha msaada kutoka nje wakati nchi ina uwezo wa kujitegemea.

"Nashangazwa na hatua ya waziri kupokea chakula bandarini pale, hii ni aibu, serikali yetu inapaswa kufanya biashara kwani duniani serikali zote zinafanya biashara, lakini Tanzania kazi yake ni kuchimba mashimo… jamani nani katuroga?"alisema Mzindakaya na kuhoji.

Aliwataka mawaziri kujiangalia upya katika utendaji kazi wao, na wasibweteke kupeperusha bendera kwenye magari ya kifahari.

Mbunge wa Muleba Kusini, Willson Masilingi (CCM) alilishauri Bunge kufuta ushuru wa magari na pikipiki kwani umekuwa kero kubwa kwa Watanzania licha ya vyombo hivyo kuwa mkombozi wa watu wa chini.

Aidha, alisema ni vema serikali ikaboresha mishahara ya wafanyakazi ambao wamekuwa wakilipwa fedha kidogo ambazo haziwawezeshi kumudu gharama za maisha ambazo hupanda kila kukicha.

Aliitaka serikali kuanzisha benki ya wakulima ambayo itakuwa ikiwasaidia wakulima katika shughuli zao na hatimaye kunyanyua kilimo ambacho ndiyo uti wa mgongo wa Tanzania.Maoni ya Wasomaji
Maoni yanayotolewa na wasomaji wa safu hii ni ya kwao na sio maoni ya kampuni ya Freemedia Ltd. Aidha sio maoni ya mtunzi au mwandishi wa habari au makala husika hapo juu. Maoni haya hayajahakikiwa wala kuafikiwa na kampuni ya Freemedia Ltd.
Maoni 13 yameshatolewa. (Nawe toa maoni yako!)
Asante kwa taarifa, labda wasipotoa hela watanzania wataamini kila siku tunavyopiga kelele magazetini kuwa serikali hii haifai, imetuletea umaskini lakini bado watatnzania wengi hawajaliona hili labda wa mijini.shida ikija watu wataamka

WAFADHILI MSIMAMO UWE HUO HUO.

Zito umekuwa mpole sana vipi kamati ya madini imekumeza??na imani - 27.03.08 @ 02:36 | #3695

huyu waziri wa fedha kama si kuchekesha basi hajui analolisema inashangaza kuwaambia wabunge kuwa wapinzani ndiyo wanaosasabisha nchi isipewe misaada. serikali ya c.c.m ndiyo inayosababisha nchi isipewe misaada kwa kushindwa kudhibiti na kutumia vizuri misaada inayopewa kwahiyo hakuna haja ya kutafuta n\mchawi wakati ni wewe mwenyewe. inashangaza pia anavyodai kuwa serikali imeshtushwa na mambo yaliyotokea hii inachekesha kwa sababu ni sawa ni mtu kushangaa kivuli chake wakati yeye mwenyewe ndiyo amekisababisha kivuli ni ajabu na kweli. Tanzania ikikosa misaada wakulaumiwa ni serikali ya c.c.m kwa kuwasaliti watanzania walio wengi na kuwakumbatia wezi wachache kwa kushindwa kuwachukulia hatua za kisheria. mtu kujiuzuru aitoshi kwani mtu huyu amecommit criminal offense ni lazima achukuliwe hatua kama wengineo tena huyu ilibidi achukuliwe hatua kali kwa kuusaliti umma tofauti na kibaka anayemwibia mtu mmoja.Tanzania aiwezi kusonga mbele kama ili eneo la kuoneana aibu alitafanyiwa kazi na wale wote wanaoturudisha nyuma kuchukuliwa hatua kali ili kuwa mfano kwa wengineo. hivi unatoa mfano gani kwa jamii kwa kuwalinda wezi kwa kukataa kuwaanika hadharani badala yake unawaandalia utaratibu maalum kwa kuwawezesha kurudisha pesa bila kuwa exposed. hii ni aibu kubwa.

na nick, Tanzania, - 27.03.08 @ 05:17 | #3700

MIMI NASEMA SIKU ZOTE NI AIBU KUSHURUTISHWA NA JIRANI KUSAFISHA NYUMBA YAKO AMBAYO INANUKA KILA SIKU NI AIBU KUBWA, SIELEWI KWA NINI VIONGOZI WETU HAWALIONI HILO. MTU MUUNGWANA UNATAKIWA KUFANYA MAAMUZI YA KIUNGWANA MAPEMA HASA YALE YANAYOLLETA MASLAHI KWA TAIFA NA WANANCHI. KUSUBIRI MPAKA TUTUKANWE NA KUCHEKWA NA KUSHURUTISHWA NA WAGENI VITU AMBAVYO NI OBVIOUS NI AIBU.

na Jicky MM, UK, - 27.03.08 @ 05:17 | #3701

Hii nchi ina nini jamani? Mbona viini macho viekuwa vingi? eti pesa zinaendelea kurudishwa BOT? na nani? tunataka mtuambie fulani karudisha kiasi kadhaa na amechukuliwa hatua kadhaa? Mini naamini kuwa hakuna kinachorudishwa kwani tuna ushahidi gani kuwa kuna pesa zinarudishwa? Suluhisho ni kuchapana bakora kama kenya labda wananchi tutaheshimika kidogo

na Mafuru George, Tanzania, - 27.03.08 @ 05:31 | #3703

tunashukuru kwa kujua ukweli kuhusu hili swala,ila waziri anasema serikali ilipata mshtuko baada ya mambo haya kutokea,sasa ina mana serikali ililala wkt haya mambo yanatokea au ilikua haijui kinachotokea,yani pesa wachukue ccm kwa kazi wanazojua wao halafu waziri unasema serikali ilistuka waache usanii,na km mkuu hapo juu alivyosema hizi pesa yasemekana zinarudishwa,kuna ushahidi gani km kweli zinarudishwa na km kweli,na nani tunaomba ukweli utawale kwenye hili swala,haya jana makamba kasema gavana atakua huko butiama kwenye kikao cha ccm au ndio kwenda kumziba mdomo

na mstari wa mbele, calif/usa, - 27.03.08 @ 05:57 | #3707

Mimi Ni Mtanzania Mzalendo, Ombi langu Kubwa ni kwa hao wafadhili, naomba wakazie msimamo huo huo. Hakuna kutoa msaada kwa mafisadi hawa! ni aibu nchi inakuwa ombaomba wa bilioni 970 wakati tumefisadi bilioni (CHECK OUT EPA BILIONI 133 + MEREMETA BILIONI 155 MINARA YA BABELI(TWIN) BILIONI 600) JUMLA BILION 888, Hivi hao wahisani hawana uchungu na Kodi za raia wao hadi kuziweka rehani kwenye midomo ya MAMBA?
lABDA WAFKIRIE UTARATIBU MWINGINE

na Sabasi, Tz, - 27.03.08 @ 07:45 | #3713

Wahisani wamekuwa wakitoa misaada mingi kwa Tanzania kwa lengo la kuikwamua kutoka kwenye umaskini. Pamoja na nia nzuri inayoambatana na utoaji wa misaada hiyo, matokeo yamekuwa ni tofauti kwani badala ya kujikwamua Tanzania imezidi kuzama kwenye dimbwi la umaskini sababu kubwa ikiwa ni misaada hiyo kuishia kwenye mifuko ya mafisadi wachache wanaoneemeka kutokana na fedha hizo. Kwa sasa ni vyema Wahisani hao wakasitisha kabisa kutoa misaada hiyo kwani haina faida yoyote kwa Watanzania wa kawaida walio wengi. Kama mateso yatokanayo na umaskini yamekuwepo kwa miaka mingi hivyo hatuoni faida ama umuhimu wa kuendelea kupatiwa misaada ambayo haina faida kwa Wananchi, WAACHE KABISA WASISAIDIE TENA KWANI INANUFAISHA MAFISADI WACHACHE.

na Msaiki, Dodoma/Tz, - 27.03.08 @ 09:11 | #3714

Wabunge wa CCM mnashangaza,hayo mnayolalamikia mnamlalamikia nani wakati serikali ni ya chama chenu? je,si ni nyie hao hao mlikuwa mnawabeza wapinzani wakati wakiikosoa serikali yenu?je walikuwa wanadai mashangingi au walikuwa wanapinga matumizi mabaya ya fedha za serikali yenu kwa kununulia hayo mashangingi ambayo ninyi wenyewe sasa mnayakebehi[Mh.Mzindakaya umesemaje kuhusu mawazizri kubweteka na mashangingi?Pengine mnaanza kujua kuwa wakati umefika tujenge nchi si kushabikia chama.Nci hii haina mipango mizuri ya kutumia rasilimali zetu,kwa nini tuombe misaada wakati madini tunayo?hao wafadhili kwa nini wasitusaidie kujua namna ya kuvua samaki badala ya kutuonyesha namna ya kula samaki?watuwezeshe tuwe na migodi yetu wenyewe,na tuweze kuuza vitu vinavyotokana na madini na si vnginevyo.huenda wanatusaidia kwa mkono huu ,wanarudishia mkono mwngine maradufu. Tzs 970bilioni ni wakia za dhahabu laki nane hivi,kuna mgodi unaomilkiwa na wageni unazalisha wakia 1.15milioni kwa mwaka hapa ncini,haijulikani wachimaji wadogo
wadogo wanazalisha kiasi gani?nani anafuatilia au anayejali?Tubabilike sasa.tunaweza bila wahisani wasanii.

na ANDREW GADI MRINJI, GEITA/TANZANIA, - 27.03.08 @ 09:38 | #3718

nashukuru Ndg Mashiringi kwamba pamoja na wewe kuwa na shangingi la serikali unakumbuka wavuja jasho.
Ukweli ni kuwa gari kama piuckups au gari zingine ndogo zisizo za kifahari sio anasa bali husaidia kutenda kazi na hivyo kuleta maendeleo ya nchi.Hizi kodi zilizowekwa kwenye magari za kila mwaka badala ya kusaidia zinashusha maendeleo.Mwenye gari aendapo shambani kwenye mafuta amelipia kodi unamjaza kodi nyingine 150,000tshs ati kwa gari cc1500 na kuendelea au 300,000tshs mkulima uchwara peasant atapata wapi?
Leo mnafanya nchi iwe ombaomba wa chakula kwani hao mapeasants mnawakatisha tamaa ya kuwa na kilimo endelevu.Magari kama pick ups sio anasa bali ni kikapu cha shamba na baiskeli ya kisasa ya shamba,ondoa kodi hata ushuru wa kuingiza magari kama hayo ikiwezekana ufutwe!Kumbuka baba wa taifa nmyakati zake aliona hayo hivi vichwa vyenu haviwasaidii?Uchumi wa nchi utakuaje bila kufikiria maendeleo ya wakulima safari zao shambani,kubeba mbolea, majani ya mifugo,nk.
Mfalme wa Nchi Ndg Rais Kikwete Tupunguzie mzigo angalau tukikopa hizo pick-ups zitusaidie sisi wa shamba na kuwalisha ninyi wea mjini chakula.Kwa kubeba kwenye baiskeli isiyo na kodi HAMTASHIBA.
Kisujwa

na Kisujwa, TZ, - 27.03.08 @ 10:13 | #3722

Mimi nashangaa sana kwa jinsi mambo yanakwenda katika nchi yetu. Hivi tumefika mahala ambapo hata kuwachukulia hatua za kisheria mafisadi mpaka tushinikizwe na wafadhili?. Mbona akina Mahalu kesi iko mahakamani?. Haya mambo ya EPA kwa nini kuna usiri mpaka sasa wakati makampuni yalihusika yanajulikana? Kutekeleza muafaka wa ccm na cuf napo mpaka wafadhili washinikize?. kwa nini tunalindana kiasi hicho?. Zi wapi sera nzuri za ccm?.

na Mwangodo G.J.M, Iringa, - 27.03.08 @ 09:21 | #3734

....aibu aibu aibu ...halafu ndo mnasema tujitegemee na tuwe huru???!
wenyewe tumeshindwa kufanya maamuzi mpaka waume zetu toka ulaya na marekani waanze kutusukuma kwa "mti" ndo tuwataje mafisadi? huu ni wendawazimu maana wendawazimu ni kwamba mtu kufanya vitendo vile vile siku zote akitarajia kupiga hatua tofauti tokana na vitendo vya kikithiri kwa uovu.

Aidha mimi sitegemei kuwa viongozi wetu watajifunza uadilifu na uaminifu toka katika nafasi walizopo ikiwa hawakufundishwa uadilifu katika familia na dini(imani) zao, wao kuwa na elimu ya vyuo vikuu mpaka shahada za kupika viungo haitasaidia kujenga uadilifu.

Pole Tanzania,pole mtanzania.Mtanzania wanaokuongoza ndio wanaokujengea maisha hafifu, mtanzania shikamana tokana na shida yako pinga uovu na kuwa tayari kupigania mema mtoto wa matonya aende shule na pia apate huduma bora za afya na ale chakula meza moja na raisi wake.

Haya Tanzania na mtanzania uliyejaa vidonda na mjerha ya kila aina tutafika au majereha na vidonda vitakupumzisha mapema.!

Mimi nasubiri kuona kama upasuaji huu wa EPA kama maisha ya mama yatokolewa au mtoto au wote watapoteza maisha.Lakini madakitari wanasema pressure na sukari vyote juu.Mimi sijui lakini mtanzania utajua huko uliko.

Pole Tanzania,pole mtanzania,pole mvuja jasho!
Lugalo

na lugalolugalo, England, - 27.03.08 @ 09:31 | #3737

Alaa kumbe Kikwete alihaidi maisha bora kwa kutegemea fedha za wafadhili? Hivi aliongea nao kwanza au aliropoka tu? Nitafurahi sana kama wafadhili watagoma kuipa serikali misaada maana ni misaada hii ndiyo inaifanya serikali ya CCM kuwa ya kifisadi na isiyotaka kujitegemea, miaka zaidi ya 40 bado omba omba, aibu kwa CCM Aibu kwa kikwete

na mapepe, China, - 27.03.08 @ 09:33 | #3739

Safari hii kidogo wanameremeta hebu angalia......
Mbunge wa Muleba Kusini, Willson Masilingi (CCM) alilishauri Bunge kufuta ushuru wa magari na pikipiki kwani umekuwa kero kubwa kwa Watanzania licha ya vyombo hivyo kuwa mkombozi wa watu wa chini.

Aidha, alisema ni vema serikali ikaboresha mishahara ya wafanyakazi ambao wamekuwa wakilipwa fedha kidogo ambazo haziwawezeshi kumudu gharama za maisha ambazo hupanda kila kukicha.

na annonymous - 27.03.08 @ 11:01 |
 
..hivi,kuna ulazima wa kupata hiyo misaada ya fedha za bajeti?

..kwanini tusile pale kamba iliyotufunga inapofika?

..yangu macho,hii bajeti ina kila dalili za kudoda.
 
..hivi,kuna ulazima wa kupata hiyo misaada ya fedha za bajeti?

..kwanini tusile pale kamba iliyotufunga inapofika?

..yangu macho,hii bajeti ina kila dalili za kudoda.

Mie nashangaa na kujiuliza .Je ni kweli JK alijiandaa kuwa Rais kwa maendeleomya Watanzania ama alitaka ndoto yake itimie kama amekuwa Rais yeye na washkaji zake ?Usiri ni mkubw akila mahali na majibu si ya uwazi kabisa .Kulikuwa na haja ya Mkullo kulia na wapinzani ? Kwani hii Nchi si yetu sote ?
 
..uliwahi kuona lini mtanzania mwenye nafasi ya kuleta mabadiliko aki-act?

..ni nadra sana!

..nishaanza kumkumbuka JKN! ngoja waende butiama!
 
lakini cha ajabu na mambo yote haya ukifika uchaguzi wanashinda,sasa sijui tatizo ni nani?
 
lakini cha ajabu na mambo yote haya ukifika uchaguzi wanashinda,sasa sijui tatizo ni nani?
Tatizo Wapinzania wetu huwa wanashindwa kujipanga na sera makini ,huwa wanakimbilia mapungufu ya CCM katika Kampeni zao badala ya kuja na sera mpya,Kushinda uchaguzi ni mpigango iliyo dhabiti n siyo mipango ya kama kufungua ukumbi wadisco
 
Haya mambo ya donors kushtuka niliyasema a few days ago hapa hapa JF, nikasema tuangalie budget yetu ya financial year inayokuja tuone tofauti.
 
lakini cha ajabu na mambo yote haya ukifika uchaguzi wanashinda,sasa sijui tatizo ni nani?

wanaoshinda huwa wanajua kuwa hawakupaswa kushinda baadhi ya mbinu zinojulikana na wao pia wanajua kuwa tunajua kuwa hawashindi hila wanatumia njia za kimafia mafia. Sasa nafikiri yote yanatokea tunaona na tunakubali. Inabidi hata wakiiba wafanye kazi, kazi hawafanyi ni utapeli tu.

Inatakiwa mapambano ya kifikra yawabadilishe, isipokuwa hivyo kuwe na time frame, strategy zibadilike.
 
mi naona hao donors watie biti wasitoe chochote tuone itakuwaje, labda tutatia akili ku mkichwa.
 
Hivi huu UMATONYA wa kuombaomba pesa kwa wafadhili utaisha lini?? Wafadhili kuleni bati hivyo hivyo. Halafu tuone kama wananchi wa CHATO biharamulo wataathirika na uamuzi wenu.
 
wanaosshinda huwa wanajua kuwa hawakupaswa kushinda bahadhi ya mbinu zinojulikana na wao pia wanajua kuwa tunajua kuwa hawashindi hila wanatumia njia za kimafia mafia. Sasa nafikiri yona yanatokea na tunakubali. Inabidi hata wakiiba wafanye kazi, kazi hawafanyi ni utapeli tu.

Inatakiwa mapambano ya kifikra yawabadilishe isipokuwa hivyo kuwe na time frame.

Tunategemea hawa viongozi wetu watawajibika kwa nani??? who voted them in??? wananchi au pesa za watu??

Kama ni wananchi, bila shaka wangewapigania wananchi...ila kama ni hela, mfanye mtakalo, lazima wawapiganie na kuwalinda waliotoa hela zao....

Unategemea kiongozi aogope eti he/she failed to perform?? anaripoti kwa nani?? mwananchi au mtoa hela??? the ongoing scenarios (EPA, Richmond) tell the truth, hata wananchi walalamikeje the issue itazimwa kisanii, na hawa mafisadi wataendelea kudunda tu mitaani. Kwani wahisani hawaoni usanii unaofanywa EPA na Richmond? Je wanasiasa wetu hawaogopi au hawajui kwamba wahisani wanaona kinachoendelea?? Wanasiasa wetu they dont care....kwamba wananchi wataumia, si tatizo lao kabisa. Hawajawahi kuwajali wananchi hata siku moja.

Ngoja tukae mkao wa kusubiria hiyo mwezi ujao, tuone wahisani watakaotangazwa..
 
Kuna wakati nakaa nafikiri "Hivi Mkuu wa kaya na suti yake kali ikiwa na tai kweli hafikii mahali akajisikia vibaya na aibu kuwa mwombelezaji, huku kiasi kile kile cha pesa unachoomba na kupewa ndo unachowaachia WAHINDI na baadhi ya Watanzania kuiba?" Baba yeyote wa nyumba ambaye anatanguliza uombelezaji kabla ya kuhahakikisha kuwa ame-exhaust njia zote ili kujitegemea, anamatatizo ya akili. Kibaya zaidi pale anakuja na kujigamba kuwa yeye ni kiombelezaji mzuri na anakubalika na Wafadhili"
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom