Zitto adaiwa kuhongwa kuitetea CHC -Tanzania Daima

MJIMPYA

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
506
271
WAZIRI kivuli wa Wizara ya Fedha, Zitto Kabwe na wajumbe wa Kamati ya Mashirika ya Umma wamedaiwa kuhongwa sh milioni 60 ili walitetee shirika hodhi la mali za umma (CHC).

Tuhuma hizo zilitolewa jana na mbunge wa viti Maalum, Anastazia Wambura, ambaye alisema kuna baadhi ya wabunge ambao wanaitetea CHC ili lipewe muda zaidi.

Wambura alitaka serikali itoe kauli juu ya jambo hilo kwani linadhalilisha Bunge na serikali.

Katika majibu yake Mkulo alikiri kupokea tuhuma hizo na wamewaomba Mdhibiti na Makaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG azifanyie kazi.

"Nimesikia rushwa waliyopewa ni sh milioni 60, hili la rushwa lilitajwa hapa bungeni, tumemuomba CAG achunguze madai kuwa kuna rushwa ilitembea kushawishi CHC lipewe muda wa kudumu badala ya muda uliopendekezwa na serikali.

Awali Zitto, alisema yuko tayari kujiuzulu uenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu ya Mashirika ya Umma (POAC) na ubunge iwapo itathibitika kuwa yeye au mjumbe wa kamati yake amehongwa.

"Naomba uchunguzi wa tuhuma hizo ufanywe kwa uwazi na endapo zitathibitika kuwa na ukweli mimi niko tayari kujiuzulu ubunge na uenyekiti wa kamati," alisema.

Zitto alisema anazo hadidu za rejea kutoka bodi ya CHC kwenda kwa CHC na amemuomba Mkulo na Waziri wa Utawala Bora aiagize Takukuru ifanye uchunguzi.

"Uchunguzi huu utangazwe na uwekwe wazi, Waziri Mkulo aahidi kuwa ikigundulika amesema uzushi na uongo mara moja ajiuzulu," alisema Zitto.

Zitto pia alimtaka Mkulo kuhakikisha kuwa hadidu za rejea zinazopelekwa kwa CAG zinafanyiwa marekebisho ili aweze kuzichunguza na kuweka wazi matokeo ya uchunguzi huo.

"Namuomba Waziri Mkulo aweke ahadi mbele ya Bunge kuwa atajiuzulu kama nitakavyofanya mimi endapo matokeo ya uchunguzi huo yatagusa pande zetu kulingana na tuhuma zilivyotolewa," alisema.

Waziri wa Fedha Mustafa Mkulo, alikana kuziona hadidu za rejea zilizoandikwa na bodi ya CHC kwenda kwa CAG.

"Mheshimiwa Zitto tuhuma hizi ni nzito ndiyo maana nikasema zitafanyiwa kazi kwani serikalini tuna utaratibu wa kuviagiza vyombo vya serikali kufanyia kazi mambo mazito," alisema.

"Utaratibu wa kujiuzulu unatokea kwa namna mbili kwanza tungesubiri uchunguzi ufanyike, taarifa ipatikane halafu lije suala la mtu kujiuzulu ama kutojiuzulu," alisema.

Mkulo alisema baada ya uchunguzi huo wa CAG taarifa itapelekwa bungeni mara moja.

Juni 23 wakati Bunge lilipokuwa likijadili Muswada wa Mabadiliko ya Sheria ya mwaka 2011, Zitto alipinga kauli ya serikali iliyowasilishwa na Mkulo na kudai Baraza la Mawaziri limerubuniwa ili kuliua CHC.

Katika maelezo yake, Zitto alisema kipengele cha kuhamisha kazi za CHC kilikataliwa na Kamati ya Fedha na Uchumi kwa kuwa kuhamishia kazi za CHC katika Ofisi ya Msajili wa Hazina kulilenga kuyaua mashirika ya umma nchini.

Najiuliza ni kwa nini TZ Daima wameamua kutumia title nzito kama hii "Zitto adaiwa kuhongwa kuitetea CHC" au ndo mwendelezo wa malalamiko ya Zitto juu ya gazeti la m/kiti wake?

Tusubiri uchunguzi tuone.
 
Najiuliza ni kwa nini TZ Daima wameamua kutumia title nzito kama hii "Zitto adaiwa kuhongwa kuitetea CHC" au ndo mwendelezo wa malalamiko ya Zitto juu ya gazeti la m/kiti wake?

Kwa sababu Tanzania Daima ni gazeti la Mbowe
 
Kwa sababu Tanzania Daima ni gazeti la Mbowe

hii sio issue ya gazeti ni issue hiko wazi hata zitto anaijua na umeona kaongelea kujiudhuru kama kweli hii kitu ni ya ukweli,
in fact hii habari haina madhara yoyote kwa zitto ila ni kinga maana watanzania tunajulishwa kinachoendela hivyo kuondoa nafasi za mchezo mchafu

aliye kwenye kona mbaya hapo ni mkullo na ndio maana hataki kusema hatajiudhuru kama itagundulika vinginevyo
sakata la ZITTO NA MKULLO kwenye hii issue ya CHC hiko wazi ni kwamba zitto kamkalia vibaya mkullo hasa baada ya mkullo kumfukuza kazi kihuni mkurugenzi wa CHC kwa kisingizio kwamba anatoa siri za serikali
 
hii sio issue ya gazeti ni issue hiko wazi

Tatizo lilikuwa ni chaguo la kichwa cha habari, kulikuwa na uwezekano wa kuandika tofauti na hivyo lakini historia ya gazeti hili na Zitto ipo wazi kabisa.
 
Hivi majukumu ya CAG ni yapi? kazi ya kuchunguza rushwa nilijua ni ya TAKUKURU, lakini siku hizi inafanywa na CAG, au ndio tuseme imani kwa TAKUKURU imetoweka? Anaefahamu anifahamishe.
 
Kuna bifu la wazi sana kati ya Zitto Kabwe na Tanzania Daima, je hili bifu la kuchafuliana majina liko kwa ajili ya manufaa ya nani? Mmiliki gazeti, mhariri, msomaji, Chadema au CCM?
 
Tz daima wame ripoti habari bila kupunguza wala kuongeza chumvi, mnakumbuka lile sakata la Mbowe na Nssf Tz daima walivyo ripoti bila kumpendelea mh mbowe hadi kujizolea sifa kibao? Kwanini others iwe nongwa?
 
Awali Zitto, alisema yuko tayari kujiuzulu uenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu ya Mashirika ya Umma (POAC) na ubunge iwapo itathibitika kuwa yeye au mjumbe wa kamati yake amehongwa.

Zitto Kabwe kama ni mkweli angelijitoa uenyekiti wa kamati tajwa ili kupisha uchunguzi na afahamu ya kuwa mwana wa kaisari hatuhumiwi,...........
 
tuachane na kuleta malumbano ya makusudi kuhusu Mbowe na Zitto,hayatusaidii,kama kuna aliyekwenda kinyume na sera za chama sawa lakini si haya na tena hilo tz daima si gazeti la chama,lina mlengo wake tu.
 
Kuna bifu la wazi sana kati ya Zitto Kabwe na Tanzania Daima, je hili bifu la kuchafuliana majina liko kwa ajili ya manufaa ya nani? Mmiliki gazeti, mhariri, msomaji, Chadema au CCM?

Hivi ulitarajia Tanzania Daima wafumbie macho yatokanayo na vikao vya Bunge? Mbona hutuelezi hilo bifu ni lipi......Zitto Kabwe amekuwa akitetea ufisadi sana tusisahau Richmond/Dowans alishinikiza walipwe kabla hata ya Mahakama Kuu kutoa maelekezo stahiki...
 
Tatizo lilikuwa ni chaguo la kichwa cha habari, kulikuwa na uwezekano wa kuandika tofauti na hivyo lakini historia ya gazeti hili na Zitto ipo wazi kabisa.

sio kwamba nyinyi ndio mnaitengeneza iwe hivi, mimi sijaona tatizo kwenye kichwa cha habari, hao ni wafanyabiashara content ndio kitu cha msingi , hacheni kuingilia biashara za watu kwa sababu tu mmiliki wake mna mjua

kanunni za biashara ziko wazi kabisa, hata kama zitto ndiye angekuwa mmiliki wa gazeti ili kuna siku habari ingeonekana kumkwaza mtu, biashara ya media ni ngumu wakuu sio tunapiga kelele tu.

cha msingi tuwe tunasoma habari yote
 
Mkulo anafanyia kazi majungu hata ivo yule mama inaonekana alipandikizwa Mkulo anahasira na Zitto si alimwambia serikali imefulia.
 
Kama Mkulo anahakika siangekubaliana na ZITTO kuwa kama si kweli akubali kujiudhuru lakini Makinda alimkinga nayeye akachoropoka kwani anajua analofanya sio kweli.
 
Kichwa cha habari ni kuhamasisha hadhira ili iweze kununua gazeti na kupata habari na kujuzwa!! Hakuna shida hapo!!
 
Mimi ninachofahamu kwa wakati huu ccm hali yao ni mbaya hiwatajitahidi kufanya lolote ili wajinusuru
 
Kuna bifu la wazi sana kati ya Zitto Kabwe na Tanzania Daima, je hili bifu la kuchafuliana majina liko kwa ajili ya manufaa ya nani? Mmiliki gazeti, mhariri, msomaji, Chadema au CCM?

wachagulie kichwa cha habari, siyo kulaumu tu, ungepropose vipi kiandikwe. Gazeti linahitaji kuuza ndugu au hata hilo hujui?
 
Zitto Kabwe kama ni mkweli angelijitoa uenyekiti wa kamati tajwa ili kupisha uchunguzi na afahamu ya kuwa mwana wa kaisari hatuhumiwi,...........

Kwa hiyo mkullo naye ajitoe kwenye nafasi ya uwaziri wa fedha ili kupisha uchunguzi??? masaburi bana hadi mtu unashindwa kushangaa
 
Watanzania bado sana! We ni mtu wa aina gani unaye-judge kichwa cha habari, sasa ingekuwa mtu unasoma kichwa cha habari halafu unatoa maamuzi kungekuwa na haja gani ya waandishi kutoa maelezo kuhusu kichwa cha habari, vilevile mkumbuke kuwa media ni biashara kama biashara nyingine hivyo unahitaji kumvutia mteja, we unafikiri watawavutiaje wateja wao, na ndio maana wewe ulikimbilia kusoma kinachotokana na hicho kichwa cha habari,
 
Hivi majukumu ya CAG ni yapi? kazi ya kuchunguza rushwa nilijua ni ya TAKUKURU, lakini siku hizi inafanywa na CAG, au ndio tuseme imani kwa TAKUKURU imetoweka? Anaefahamu anifahamishe.
<br />
<br />
distribution of power.
 
Back
Top Bottom