Zitto adai ripoti ya TISS yaonyesha Rais Magufuli hawezi kushinda 2020

Kumbe hizi figisu zilizoanza sasa hivi uchaguzi serikali za mitaa ni kwa kujihami baada ya ripoti ya TISS?
Lakini kulazimisha kura sio dawa Bali yeye sasa awaulize watumishi, wakulima, wafugaji, wanafunzi nk wanataka nini hasa? Aone kama watamuambia wanataka ndege basi anunue sana au kama hawataki wanataka vingine basi ndio afanye.
Aache kuwa MtuPori asiyesikia lolote la kuambiwa
Huyu mtu hapendwi hata kwao .
 
Ofcourse TISS kabla ya uchaguzi huwa wanafanya utafiti wao kujua nani anakubalika mbele ya wananchi.

Kabla ya uchaguzi wa mwaka 2015, ilikuwa around 2013/2014 na kabla ya Lowasa kuhamia Chadema Ripoti ya "KITENGO" ilionyesha kuwa miongoni mwa possible candidates nchini, Magufuli anakubalika sana kwa wananchi

Sasa sishangai tena ripoti kama hiyo ya TISS kuonyesha kuwa hakubaliki, Huwa wanafanya utafiti kujua hali ya kinchi inakwendaje.

Kinachomkwamisha JPM ni Uchumi uchumi uchumi uchumi uchumi na Demokrasia na haki za binadamu
Maisha ya watu yako duni, biashara zinakufa, Kilimo ambacho kinagusa watu wengi hajakipa kipaumbele, Hali ya usalama wa raia (mambo ya utekaji) ni ya mashaka, uonevu kwa wapinzani, wananchi hawapendi mambo ya maguvumaguvu kwenye siasa, ajira kwa vijana ni ngumu, Maslahi ya wafanyakazi yamesahauliwa, Stahiki za wastaafu zinapigwa danadana etc

Amebaki kuonyesha SGR, Stieglers, Flyover, Uwanja wa Ndege Chato, Daraja la baharini la Salender etc

URAIS NI ZAIDI YA UJENZI
SGR ni mradi mmojawapo wa miradi ya East African Community ikiwa ni sehemu ya ile ya Mombasa-Nairobi-Kampala-Kigali-Bhjumbura-Juba. Miradi mingine ni pamoja na barabara za Arusha By-pass, Arusha - Voi, Kenya (jiwe la msingi limekwisha wekwa), barabara toka mpakani Tanga hadi Bagamoyo itaunganisha Dar na Mombasa iko kwenye ujenzi. Flyover na Salender Bridge ni miradi ya Kikwete ikiendelea kutekelezwa wakati wa Awamu ya Tano, vivyo hivyo miradi ya Magufuli isipokamilika wakati wa Awamu ya Tano itakamilishwa na Awamu ya Sita au Saba.
 
Kuna jamaa alishawai kuniambia kuhusu utimamu wa Zito Sasa nimeanza kukubali mida mingine Ram yake huwa inafuta baadhi ya Mafaili
 
kuna dada mzungu aliniambia kulalamika ni sehemu ya mchango wa kuendeleza kinacholalamikiwa!! yaani kusema sema tu kuwa tuna tume feki ya uchaguzi tangu 1992 hadi leo bila kuweka mikakati na timu ya kupambana kuitoa ni ujuha!!

wapinzani kamwe hawatatoboa nchini sisiem itashinda kwa millenium!! mimi ni kijani ninaependa siasa za haki na ushindani nawashauri wapinzani wasimamie kudai tume huru kwa vitendo waunde task force Mwenyekiti Nyalandu nilimsikia kwenye kipindi cha television akijipambanua zaidi kwa mada hiyo na watafute ufadhili ndani na nje ya nchi na waweke time frame!!namimi niwe mshauri wao kupitia JF inbox!
 
SGR ni mradi mmojawapo wa miradi ya East African Community ikiwa ni sehemu ya ile ya Mombasa-Nairobi-Kampala-Kigali-Bhjumbura-Juba. Miradi mingine ni pamoja na barabara za Arusha By-pass, Arusha - Voi, Kenya (jiwe la msingi limekwisha wekwa), barabara toka mpakani Tanga hadi Bagamoyo itaunganisha Dar na Mombasa iko kwenye ujenzi. Flyover na Salender Bridge ni miradi ya Kikwete ikiendelea kutekelezwa wakati wa Awamu ya Tano, vivyo hivyo miradi ya Magufuli isipokamilika wakati wa Awamu ya Tano itakamilishwa na Awamu ya Sita au Saba.
HUJAMSIKIA AKIDAI HANA HAKIKA KAMA ATAKAYEKUJA ATAENDELEZA ANAYOFANYA? Mfano nani mwenye akili zake aendeleze ujenzi wa uwanja wa ndege chato na hifadhi ya mafisi burigi?
 
Kabisa yaani na dhana ya kulalamika ikikukaa kichwani ni Ulemavu... Maana hata sehemu ya kufanikiwa wewe ni kulalamika tu Kwa Lugha nyingine ni kudeka bila sababu kikubwa Pambana hata Shule sisi ambao tumesomea za kibabe mwanafunzi mbabe akikupiga siku ya kwanza ukaenda kumshitaki Kwa mwalimu alafu haadhibiwi vya kutosha na akarudia tena kukupiga inabida Sasa wewe ufanye mazoezi ya kuwa strong kupambana nae... Imeisha hiyo
 
Uchaguzi gani ulishashindwa au kushinda kabla ya kura kupigwa. Zitto una matatizo siyo bure. Nilikuwaga nakuona wa maana enzi zile tunawaona kwenye ITV mligomaga ili muongezewe bumu some one Mkili akakamatwa. Nakumbuka niliona kwenye TV na Omary na mkaka mmoja mweusi anavaa miwani mnasema Mkili must be free na kweli alitoka celo. Sasa naona umegauka na kuwa vuvuzela tu.

Huu uhuni wako ulioandika hapa, rejea kilichotokea uchaguzi wa SM.
 
Back
Top Bottom