johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,914
- 141,863
Nimemsikiliza kwa makini mbunge wa Kigoma mjini wakati akichangia hotuba ya Ofisi ya Rais Utawala bora.
Ameongea mambo matatu mosi habari ya Vodacom na DPP ile iliyomvutia Dr Albert Msando.
Pili akaongelea taarifa " alizonazo" juu ya mahesabu ya Takukuru kutokaguliwa na mkaguzi yoyote kwa takribani miaka nane sasa.
Na tatu akazungumzia Wakala wa ndege za serikali kuhamishiwa Ofisi ya Rais kutoka Wizara ya ujenzi.
Zitto anasema si sahihi wakala huyo kuhamishiwa OR na hapo ndipo ninapopingana naye. Kwa uwekezaji mkubwa na wa kihistoria uliofanywa kwa wakala huo ni sawa kabisa uhamisho uliofanyika.
Pale Ikulu kuna usalama wa uhakika wa rasilimali zetu na ni vema kabisa taasisi ya Rais ikawa inapata taarifa za moja kwa moja kuhusu uwekezaji wa nchi kwenye ATCL.
Niendelee kuwatakia kwaresma yenye baraka
Maendeleo hayana vyama!