Zito laibuka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zito laibuka

Discussion in 'Matangazo madogo' started by MziziMkavu, Mar 19, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Na Mwandishi Wetu
  Wakati jamii ya muziki wa Kizazi Kipya na mashabiki wao wakiwa bado katika maombolezo ya msiba wa Julieth D. Mrina ‘Pendo’ (24), kubwa zito limeibuka kuhusu anayetajwa kuwa ni mchumba wake, Hamad Ally ‘Madee’, Amani limekusanya vielelezo...

  [​IMG] [​IMG]
  Baadhi ya waombolezaji kwenye msiba huo uliokuwa umepigwa kambi Kimara, jijini Dar ni wanamuziki wa Kizazi Kipya, akiwemo Joseph Haule ‘Profeja J’, ‘Tundaman’, Khadija Shaban ‘Keisha’, Kasim Maganga ‘Kasim’ na ma-andagraundi wengine kibao.

  Ulipofika muda wa kusomwa kwa wasifu wa marehemu Pendo, kwamba ni nani, alizaliwa wapi, mwaka gani na amefanya nini hadi kifo kinamkuta ndipo lilipoibuka jambo zito ambalo liliwaacha midomo wazi baadhi ya ‘kampani’ ya Madee.

  Wasifu huo ulimalizika bila kutajwa kuwa, marehemu alikuwa amechumbiwa na Hamad Ally ‘Madee’ jambo ambalo lilizua maswali lakini hakukuwa na mwenye jibu.

  Amani liliongea na baadhi ya wasanii waliohoji kulikoni kwenye vyombo vya habari kuandikwa wawili hao ni wachumba lakini asitajwe kwenye wasifu wa marehemu?

  “Mimi nilijua nakuja kwenye msiba wa mchumba wa Madee, sasa mbona kwenye wasifu hawajasema kama marehemu mpaka kifo chake alikuwa ameshachumbiwa?” Alihoji msanii mmoja wa Bongo Fleva, jina tunalo.

  [​IMG]
  Mwingine alisema kuwa, anavyojua yeye, wasifu wa marehemu unaacha kumtaja mtu kama alikuwa mpenzi tu, “lakini kuanzia mchumba mpaka mume au mke hutajwa,” alisema.

  Aidha, habari nyingine zinadai kuwa, licha ya Madee kutotajwa kwenye msiba huo kama mchumba wa marehemu, mama yake mzazi ‘mama Hamadi’ naye alikuwepo msibani hapo kama binadamu kwa sababu shughuli ya msiba ni ya kibinadamu zaidi na haihitaji mwaliko kama ilivyo kwenye sherehe za ndoa ‘harusi’.

  Habari zaidi chini ya zulia zinadai kuwa, baadhi ya ndugu wa marehemu wanamtambua Madee kama mchumba mtarajiwa, lakini hakuwahi kujitambulisha rasmi kwa barua na posa katika familia hiyo ndiyo maana hakupata ‘festiprioriti’ katika wasifu wa marehemu.

  Hata hivyo, bado ‘tano’ inatolewa kwa msanii huyo kutoka ‘skwadi’ ya TiP Top Connection, Manzese jijini Dar ikisemekana kuwa, ndiye aliyefanikisha kuusafirisha mwili wa marehemu Pendo kutoka Hospitali ya Mkoa wa Pwani, Tumbi, Kibaha kwenda Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Jijini Dar es Salaam.

  Marehemu Pendo alifariki dunia Machi, 13, 2010 katika ajali iliyoshirikisha basi la Shabiby na lori iliyotokea Kibaha, mkoani Pwani. Katika ajali hiyo, ni Pendo tu aliyepoteza maisha.

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  PENDO AACHA VILIO NA MAJONZI!


  [​IMG]
  Binti Juliet Mrina 'Pendo', ambae alikuwa girlfriend wa mwanamuziki wa bongo flava Madee, aliyeaga dunia wiki ilkiyopita katika ajali ya basi la Shabiby akielekea Dodoma, leo ameagwa katika Hospitali ya Muhimbili kabla ya maziko yatayoyafanyika nyumbani kwao Rombo, Moshi kesho. Eneo la kanisa la Muhimbili lilijawa na majonzi wakati wasanii mbalimbali, ndugu na marafiki wa Madee na Pendo walipojitokeza kuuaga mwili wake. Ilikuwa inatia simanzi kwa sababu ajali imekaztiza ndoto nyingi alizokuwa nazo Pendo ambaye alikuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John kilichopo Dododma na alikuwa katika mwaka wake wa mwisho uliotarajiwa kufikia tamata mwezi Juni mwaka huu!! Kamera yetu ilikuwepo mchana huu na kunasa taswira za majonzi na huzuni zifuatazo:

  [​IMG]
  ..Pendo akiwa ametulia tuli kwenye nyumba yake ya milele!

  [​IMG]
  ..Mama mzazi wa Pendo, Grace Zacharia, akilia kwa uchungu wakati wa kumuaga mwanae

  [​IMG]
  ..watu walishindwa kujizui kulia kwa uchungu!

  [​IMG]
  ...Mh. Mramba naye alikuwa miongoni mwa waombolezaji na mmoja wa wana familia ya kina Pendo

  [​IMG]
  Madee akimuangalia kwa jicho la mwisho mwandani wake

  [​IMG]
  Profesa Jay alikuwa miongoni mwa wasanii waliofika kumpa tafu mwenzao

  [​IMG]
  ..masikini Madee!

  [​IMG]
  ...majonzi ya mama mzazi wa Madee, Bi. Anzela Magenge

  [​IMG]
  ..swahiba mkubwa wa Madee, Tundaman (kulia) alishindwa kujizuia kulia

  [​IMG]
  Profesa Jay akimpa mkono wa pole Madee

  [​IMG]
  ...Madee na baadhi ya wenzake waliohudhuria

  [​IMG]
  ...Madee na Pendo enzi za penzi lao motomoto
  PICHA: Richard Bukos/GPL​
   
 3. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #3
  Mar 19, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,369
  Likes Received: 3,687
  Trophy Points: 280
  Hivi kati ya Madee na Allen Mtetemela (Yule lecturer wa pale chuoni) nani alikuwa wake halisi.....??? Inaonekana huyo Allen naye alikuwa anafanya mambo Pendo akiwa Dodoma
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Mar 19, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Kamanda inakuhusu nini?
   
 5. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #5
  Mar 19, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,167
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Kwa mtazamo wangu hakuna zito hapa.
  Sasa hata vijana wadogo wengine wakifa ma-girl/boy friends zao watangazwe!

  Nonsense!

  Mtazamo tu.
   
 6. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #6
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  How inappropriate!!

  Let the girl rest in peace.
   
Loading...