Zito kutoka Chadema ni lazima

Status
Not open for further replies.

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
Mkuu ZZK
nikiwa kama mwanachama wa chadema naomba nikupe ukweli nini kitafata muda si mrefu:
bila kujali utafukuzwa au hufukuzwi chadema,napenda kukuhakikishia ni lazima kwa vyovyote vile uondoke chadema
Zito usifikirie kubaki chadema kwa sababu sisi wanachama ambao tumebeba chama hatuna imani na wewe tena kwa vyovyote vile
tunasubiri siku zako 14 ziishe uondoke,na kama uongozi utakuachia wewe kubaki chadema basi chadema itakuwa kwenye wakati mgumu zaidi kwani sisi wanachama hatutaki ubakie chadema,
kama kweli wewe ni mwana demokrasia naomba kwa moyo wote ondoka ili tuweze kushikamana na kuendeleza mapambano yaliyokwisha anza ya mabadiliko


 
Mi nadhani tunahitaji watu, hatufurahii mtu yeyote kufukuzwa ndani ya chama awe mkubwa ama mdogo, lengo kuu ni mtu kubadilika na kubaki ndani ya chama, hilo ndo lengo kuu
 
Akili za kuambiwa chsnganya na za kwako naona propaganda za mbowe na wrnzake zimewapata kwel kwel kiac hamuon Mazur ya beans zitto
 
Kama kweli chadema kinataka kisimame ni lazima kimuondoe kwenye chama,hakuna jinsi kwa sasa iwe alionewa au nikweli hizo tuhuma sababu kubwa ni kwamba tayari mpasuko umetokea kwenye chama, wapo wanaomuunga mkono Zitto na wapo wanaounga mkono uongozi uliopo madarakani hivyo haitatokea wakaiva chungu kimoja,kwani kunawanachama ambao wamepoteza uaminifu na Zitto hivyo hata akibaki wataendelea kumuona msaliti hawatamkubali na wapo wanaoona uongozi uliopo ni wa ukanda,ukabila na ukandamizaji na nia ni mwenyekiti anataka aeendelee kutawala hivyo nao hawatakubalina uongozi huo uendelee. hivyo njia pekee ni kumtoa Zitto na wafuasi wake watamfuata kuondoa mpasuko nimesema Zitto sababu sio rahisi kuuondoa uongozi kwa kipindi hiki na ukisema usubiri uchaguzi ndio chama kitaendelea kusambaratika. Busara pekee inayoweza tumika ni Zitto kujishusha kunusuru chama vinginevyo ajitoe au asubiri wamuondoe.
 
Kama chadema watamfukuza zitto ni km Barcelona wamuuze messi kwenda madrid
 
Aondoke,aanzishe chama chake au ajiunge na NCCR ,CCM au CUF au kile chama cha akina 6,wanaodhani kaonewa watamfuata huko atakapoenda,ni bora CHADEMA itikisike kuliko kuwa na watu mbayuwayu/chamelleon.History is full of example ya watu kama Zito ambao mwisho wa siku wanabaki kwenye politica Archive.
 
Hakuna ulazima wa kuondoka.. Abaki tu ndani ya chama.. Na yule mwenye kadi ya magamba vp na yeye aondoke au ndo kusema mkubwa akijamba amepumua ila mtoto ndo hujamba
 
Chadema ipo moyoni mwake hata ikitokea atanyang'anywa uanachama wake hatojiunga na chama chochote.... atarudi chuo kikuu akawafundishe vijana.
 
mkuu zzk
nikiwa kama mwanachama wa chadema naomba nikupe ukweli nini kitafata muda si mrefu:
Bila kujali utafukuzwa au hufukuzwi chadema,napenda kukuhakikishia ni lazima kwa vyovyote vile uondoke chadema
zito usifikirie kubaki chadema kwa sababu sisi wanachama ambao tumebeba chama hatuna imani na wewe tena kwa vyovyote vile
tunasubiri siku zako 14 ziishe uondoke,na kama uongozi utakuachia wewe kubaki chadema basi chadema itakuwa kwenye wakati mgumu zaidi kwani sisi wanachama hatutaki ubakie chadema,
kama kweli wewe ni mwana demokrasia naomba kwa moyo wote ondoka ili tuweze kushikamana na kuendeleza mapambano yaliyokwisha anza ya mabadiliko



inawezekana wewe ni gamba
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom