Zitambue tofauti za tiba za asili/mitishamba na tiba za kichawi/kishirikina

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,531
1479577437487.jpg
kuna ujinga tumejazwa kwamba tiba sahihi na zinazokubalika hata mbele za Mungu (kwa wale waamini na waaminio)ni tiba za hospitali ya mzungu almaarufu kama tiba za kisasa
Tiba za kisasa ni kinyume cha tiba za asili tiba za mitishamba...wenzetu kama wachina na hata wahindi walikataa huu upuuzi wakaboresha tiba zao za asili na zikawa kilimbilio la wengi huku waafrika tukizidharau za kwetu....yote hii ni kwasababu ya kutawaliwa na kuchukuliwa utumwa
Kuna siri kubwa yenye nguvu kubwa kwenye mimea na tiba za maradhi ya binadamu, tiba za mitishamba zisizo na ushirikina ndani yake ni tiba namba moja duniani zinazoheshimika mno, ukiifahamu mitishamba vizuri na matumizi yake unaweza kuwa guru kwenye tiba mbadala tiba zisizo na kemikali tiba zisizo na side effects
1479578069674.jpg
nachelea kusema mababu na mabibi zetu aidha kwa kutofahamu au pengine kwa uchoyo walishindwa kurithisha utaalam wa mitishamba kwa kizazi kipya matokeo yake wakaondoka na ujuzi wao
Mahitaji ya tiba mbadala kipato na changamoto za kimaisha vikaibua kundi jipya linalotumia mitishamba na ushirikina kutibu na kurekebisha mambo yaliyoenda mrama..! Mkanganyiko wa imani na elimu ya kisasa ikaleta tafsiri ya kuona kuwa tiba ya mitishamba na ushirikina ni dugu moja
Ukweli ni kwamba kuna nguvu ya ajabu ya asili katika mimea hivyo watu wenye ufahamu kwenye hili hufanya kolabo/cocktail na mambo ya kishirikina na kichawi kuongeza nguvu
1479578534964.jpg
lakini Ukweli ni huu hapa tiba yoyote ya mizizi na mitishamba bila kuhusisha maagano haina shida kabisa wala madhara LAKINI tiba yoyote ya mitishamba yenye kuhusisha tunguli mavumba makoa tunguli hirizi na damu, hiyo ni tiba ya kishirikina na kichawi yenye madhara ya baadae
Unapohitaji tiba mbadala kuwa makini na kile uambiwacho na upewacho ili usije kuingia kwenye maagano mabaya
Nb: Tiba ya kitunguu saumu ndimu na mafuta ya mzeituni havina uhusiano wowote na mambo ya kishirikina! Vitumie bila shaka
1479578958186.jpg
 
dawa za wazungu labda nilikunywa sijapata akili,lakini toka nimepata ufahamu dawa zangu kubwa ni,black seed(habat soda)mlonge,aloe vera na mwa40 niliotoka kujifukiza juzi na kunywa glasi kadhaa!nilikuwa nahis siko poa kabisa maumivu ya mwili sipati usingizi na vijipu uchungu kama vi4 nimepigwa mwa40 vimepotea na homa zimeisha na usingizi hata saa hivi naandika hapa huku nasinzia
 
Tiba asilia ni nzuri ila tatizo linakuja kweny vipimo.

Kuna jirani yangu hapa amefariki kwa kunywa mualovera.

Walikunywa wawili mmoja akaponea chupuchupu baada ya kufikishwa hospital.
 
Sasa rafiki yangu mshana, nikija kwako nataka dawa uliyotoka nayo congo juzikati ulipopotea kitambo, utanipa hiyo bila kuchanganya na ushirikina ili upate pesa nyingi?



$$
 
Kwaiyo ikituwe salama tufanyejee maaana kumjua huyu nimshirikina au anatumia ushirikina ni ngumu
Miongoni mwa viashiria vya tiba za kishirikina ni mganga kuhitaji ndege/mnyama yeyote mf. kuku, njiwa, mbuzi, kondoo n.k. ktk tiba hiyo. Hata kama atajifanya mtu wa dini vipi huyo ni mshirikina.
 
Walio wengi waganga wa tiba za asili wanachanganya na ushirikina. Utalishwa maji machungu mpaka sura inabadiliko kupona uponi siku zinaenda. Mashana Jr karibu ukumbin
 
Miongoni mwa viashiria vya tiba za kishirikina ni mganga kuhitaji ndege/mnyama yeyote mf. kuku, njiwa, mbuzi, kondoo n.k. ktk tiba hiyo. Hata kama atajifanya mtu wa dini vipi huyo ni mshirikina.
Lakini kuna wengine wanahitaji ndege au mnyama kwa kisingizio cha tiba kumbe kitoweo tu!, haijalishi wanatibu kishirikina, au ki sunna, ama ni matapeli tu.
 
Mshara jr naomba nisaidie tatizo la viganja vya miguu kuwaka moto mpaka unakosa usingizi kwa nyakati za usiku
 
Mshara jr naomba nisaidie tatizo la viganja vya miguu kuwaka moto mpaka unakosa usingizi kwa nyakati za usiku
Kuna ile tiba ya kuweka ndimu na kitunguu saumu kwenye beseni la maji ya vuguvugu na kuloweka miguu kwa nususaa ulishawahi kujaribu? Ni zoezi la siku saba tiba ya kitunguu saumu
 
Back
Top Bottom