Mjadala: Je, ni siku zipi ambazo mwanamke huweza kupata ujauzito katika mzunguko wake wa kila mwezi?

Habari wakuu,

Turejee kichwa cha habari,

Wakuu naombeni msaada wenu,

Nahitaji kufahamishwa Tarehe za hatari kushika mimba. Nimeuliza hivi coz ya kitu kimoja baada ya kujifungua my first born miaka miwili ya kumwachisha kunyonya nikaweka kijiti mkononi cha miaka 3, baada ya mda huo nikaongeza tena miaka 3 so ikawa jumla 6yrs. Hapo mtoto akawa kashafikisha miaka 8. But kipindi chote wakati nikitumia hii kitu nimepata mateso makubwa coz mzunguko wangu wa period ukavurugika kuumwa sana kiuno ikawa kila mwezi naingia Tarehe mpya.

Lengo la Uzi huu ni hili naomba nielekezwe namna ya kutumia kalenda unasomaje kwenye mzunguko kujua hizi ni siku hatari za kushika mimba na hizi ni safe days coz bae wangu hapendi condom na mimi sitaki tena kuendelea kutumia hizo njia zingine panapo majaaliwa naitaji mtoto wa pili but kwa kipindi ninachosubiri nataka niupumzishe mwili.

Madoctor na wanawake wenzangu nisaidieni PSE ili na mimi nianze kuyafurahia maisha.

hahahaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
 
Ni hivi... Chukua mzunguko wako toa 14 then znazo baki toa 4,hapo hutakiwi kushiriki tendo.

Then chukua zilizobaki baada ya kutoa 14 jumlisha 3 hapo unaruhusiwa kufanya mapenzi

Mfano

Mwenye siku 28 fanya hivi...

28-14=14
Hiyo ndo cku ya ovulation kwake,

So
14-4=10
Tarh hiyo hatakiwi kufanya mapenzi bila kinga kwani atapata ujauzito

Then,

14+3=17
kuanzia tarehe 18 ndo anaweza fanya mapenzi bila kupata ujauzito mpaka tena mwez unaofuatia.

Na mwenye tareh 30 pia vile vile...

NB.

Tarehe huwa zinaongezeka kila mwezi Yaan.
Kama ulianza na 28 ,

Mwezi unaofuata waweza kuwa na 30

Na

Mwez mwingne 35

Na hii hutofautiana kutoka mwanamke mmoja na mwingne.

Chunguza tarhe zako kwa makini, kisha tumia hiyo formula hapo juu itakusaidia.

Nawasilisha.
Katwishen kazuri asee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heshima Mbele..

NITAKUWA NA ENDELEZA UZI HUU KILA BAADA YA SIKU 2. KIPANDE KINGINE KITAKUJA JUMANNE JIONI


Kwa siku kama 15-21 nitakuwa natoa mfululizo wa masomo ya mzunguko wa hedhi, na namna ya kutumia mzunguko wa hedhi kwa ajili ya kukokotoa siku salama siku za uzazi, siku ya kupata mimba na siku za hatari. Nitafafanua pia namna gani unaweza kubashiria kupata mtoto wa jinsia unayoitaka na namna unavyoweza kutumia mzunguko wako (njia ya asili) kupanga uzazi.

Sasa wengine wataanza kujiuliza huyu ni nani? Mimi sio daktari wala nesi, mimi ni mwalimu. Kumbuka kama bado hujaelewa vizuri usije tumia njii hizi kwa ajili ya kuzuia kupata mimba. Ufafanuzi wa mada hii umeegemea zaidi kwa wale wanaopenda na kuhangaika na kupata mimba, au kwa kuwa mzunguko wao wa hedhi hauko sawa au kwa sababu wanaishi mbali na wenzi wao.

Nimekuwa naulizwa maswali mengi sana katika simu kwa whatsapp au message za kawaida na wakati mwingine kwenye magroup pia za whatdapp na messenger - lakini kutokana na muda kuwa mdogo inakuwa ngumu sana kuwajibu watu wote kwa muda mwafaka na kwa ufanisi mkubwa. Hivyo nimeona nikiweka somo zima hapa JF inakuwa rahis mtu kusearch hata kwa google na kujifunza haraka - kwa kawaida mada za JF zinaonekana haraka kwenye google search kuliko blog na facebook.

ILI UELEWE VIZURI MADA HII MPAKA MWISHO - BASI HUNA BUDI KUJIFUNZA MAMBO KADHAA MUHUMI.

Kama wewe ni mara yako yakwanza kabisa kujifunza mzunguko wa hedhi basi itakufaa kuwa na KALENDA yako ya ukutani na PENI nyekundu na nyeusi kama utaweza.

1- Siku ya kwanza umepata bleed (wengi husema nimeingia siku zangu) ndio siku ya kwanza ya mzunguko wako wa hedhi katika mwezi husika.
2- Siku ya mwisho ya mzunguko wako wa hedhi ni siku moja kabla hujapata hedhi ya mwezi mwingine.
3- Mzunguko wa hedhi sio lazima kila mwezi uje siku ile ile na tarehe ile ile
4- Mzunguko wa hedhi sio lazima kila mwezi uwe na urefi/ukubwa ule ule.

5- Mzunguko wa hedhi ni nini?
Ni idadi ya siku unazochukua kuanzia siku ya kwanza umepata hedhi/bleed mpaka siku moja kabla ya kupata hedhi ingine ya mwezi mwingine.
6- Siku za Hedhi ni nini?
Siku za Hedhi ni siku kuanzia siku ya kwanza umepata bleed mpaka siku ya mwisho umemaliza ku-bleed
7- Siku za Hatari ni nini?
Siku za Hatari ni siku zote ambazo unaweza kufanya tendo la ndoa na kupata mimba
8- Siku za Uzazi ni zipi?
Siku za uzazi ni zile siku ambazo kwa mtu anayetaka kupata mimba ndio siku zenye uwezekano mkubwa wa kupa mimba, ni siku ambazo dalili zote za yai kutokea au kutoka zinaonekana (kawaida ni siku 3-4)
9- Siku ya Yai Kupevuka au siku ya Mimba
au kutoka katika nyumba yake (ovaries)
Hii ni siku ambayo yai hutoka/hutolewa katika nyumba yake (nyumba ya mayai au ovaries) na kuelekea kwenye mirija ya uzazi ili kushika mimba kwa kiingereza inaitwa ovulation day.
10- KATIKA MAISHA YA KAWAIDA – mwanamke akisema nimeingia kwenye siku zangu basi anamaanisha ameanza bleed. Kama atasema leo niko mwezini siku ya pili basi anamaanisha ako katika siku ya pili ya hedhi na siku ya pili ya mzunguko wa hedhi.

Kwa hiyo kama mwezi huu wa kumu ulianza kupata hedhi siku yeyote ile basi siku iyo ya kwanza ulipopata hedhi kwa mwezi huu wa kumi ndio siku yako ya kwanza ya mzunguko wa hedhi kwa mwezi huu wa kumi. Mfano kama NOLA aliingia siku zake tarehe 05/10/2017 basi leo tarehe 14/10 ni siku yake ya 10 ya mzunguko wako wa hedhi. Haijalishi kama alimaliza hedhi yake tarehe0810 au kabla ya hapo. Kwa hiyo kitu muhimu hapa ni kuwa siku za mzunguko wa hedhi na siku za hedhi ni ni vitu viwili tofauti sana. Katika mfano huu hapa ni kuwa Nola leo ni siku yake ya 10 ya mzunguko wa hedhi lakini alimaliza bleed tarehe 08/10 kwa hiyo siku zake za hedhi au siku zake za bleed zilikuwa 4 tu yaani tarehe 05/10, 06/10, 07/10 na tarehe 08/10.

Somo litaendelea JUMANNE - jinsi ya kuhesabu, kukotoa na kuweka alama kalenda yako ya uzazi.

MASOMO YANAENDELEA SEHEMU YA PILI

>>>> NAMNA YA KUKOKOTOA MZUNGUKO WAKO WA HEDHI

Mfano leo umepata bleed tarehe 12/10/2017
Basi tarehe 12/10/2017 inakuwa siku yako ya kwanza ya mzunguko wa hedhi,
Na tarehe 13/10/2017 inakuwa siku yako ya pili ya mzunguko wa hedhi
Na teherhe 14/10/2017 inakuwa siku ya tatu kadhalika
tarehe 15/10//2017 ni siku ya 4
tarehe 16/10/2017 ni siku ya 5
.
.
Nakuendelea, utakoma kuhesabu mzunguko wako wa hedhi mara tu unapopata hedhi ingine.

Ikiwa Utapata bleed ingine tarehe 10/11/2017. Basi siku ya mwisho ya mzunguko wako wa hedhi kwa mwezi wa kumi inakuwa tarehe 09/11/2017. Na tarehe 10/11/2017 inakuwa ni siku yako ya kwanza ya mzunguko wa mwezi wa 11

ZINGATIA mwezi unaweza kuwa na siku 31,28,29 au 30 - kwa hiyo kama hujui ukubwa mbalimbali wa miezi lazima utumie kalenda yako vizuri.

Mfano wa Asha wa Makoroboi - Mwanza
Amepata bleed yake tarehe 02/10 ikaisha 05/10/17


KWANZA SIKU ZAKE ZA HEDHI kwa mwezi wa 10 au siku za kuwa mwezini ni 4 yaani
tarehe 02/10
tarehe 03/10
tarehe 04/10
tarehe 05/10


Mwezi huohuo wa kumi akipata bleed tena siku ya tarehe 28/10/017 na ikaisha tarehe 02/11.
2- Siku za hedhi kwa mwezi wa 11 ni 6 yaani kuanzia tarehe
tarehe 28/10
tarehe 29/10
tarehe 30/10
tarehe 31/10
na taerehe 01/11
na tarehe 12/12


JE ANAMZUNGUKO WA HEDHI WA SIKU NGAPI KWA MWEZI WA 10?

HAKIKISHA UMEWEKA ALAMA kwenye kalenda tarehe zako za kuanza kwa bleed

Namna ya kufanya
1- aliingia mwezini kwanza tarehe 02/10
2 - akaimgia tena mwezi huo huo tarehe 28/10

A. Siku ya kwanza ya ku bleed ni tarehe 02/10 - hii ndio siku ya kwanza ya kuanza kuhesabu siku za mzunguko wako wa hedhi.
2. Siku ya mwisho ya mzunguko wa hedhi ni tarehe 27/10 na sio 28/10
Utahesabu mzunguko wako wa hedhi kwa mwezi wa kumi kuanzia siku ya tarehe 02/10 hadi tarehe 27/10.

KITU CHA KUFANYA - kila unapoanza kubleed unaweka alama nyekundu mfano tarehe 02/10 pia weka alama ya X kwenye tarehe 28/10

kisha hesabu siku zote zilizopo kati ya terehe 02/10 na tarehe 27/10. UKISHESABU SIKU HIZO UNAPATA SIKU 26.
Kwa hiyo Asha wa Makoroboi Mwanza anamzunguko wa siku 26.


BAADA YA KUJUA NAMNA YA KUKOKOTOA MZUNGUKO WAKO WA HEDHI
- sasa inafaa ujue namna ya kukokotoa siku zako za salama
- ujue kukokotoa siku za uzazi
- ujue kukokotoa siku ya kupata mimba
- ujue kukotoa siku za hatari


Ili ufanikiwe kabisa katika zoezi hili basi huna budi kujua mizunguko yako ya hedhi ya zaidi ya miezi mitatu, na katika kuijua mizunguko hiyo pia inafaa utambue ya kwamba kunayo mizunguko ya hedhi ya aina mbalimbali na yote inaweza kufaa au kutokufaa ilimradi ipo kati ya siku 20 na 35. Nje na hapo mzunguko wako unakuwa siyo mzuri.

Labda utajiuliza kwa nini mzunguko wa siku chini ya 20 ni mbaya na mzunguko wa siku zaidi ya 35 ni mbaya?
- ni kwa sababu ili matukio muhimu ya uzazi yapate kufanyika kwa ufasaha ndani ya mwili wako basi angalau kwa wastani huchukua siku 28, au siku za chini kabisa ni siku 20 na angalua siku za juu kabisa ni 35. lasivyo kuna baadhi ya vitu vitakuwa havikamiliki au vinachukua muda mrefu isivyokawaida.


AINA YA MIZUNGUKO YA HEDHI.

(1) KUNA MZUNGUKO WA HEDHI USIOBADILIKA usiobadilika - yaani kila mwezi unaingia tarehe ile ile au karibia siku zilezile.
Mfano wa mzunguko wa hedhi uliokamili ni kama hivi.
-july mzunguko wa siku 26
- june mzunguko wa siku 26
- may mzunguko wa siku 26

(2) KUNA MZUNGUKO UNAOYUMBA KIDOGO LAKINI SIO ZADI YA SIKU 5
Mfano wa mzunguko unaoyumba kidogo
- july siku 26
- june siku 28
- may siku 30
Ukiangali hapa tofauti ya mzunguko mmoja na mwingine ni siku 2 na 4.

(3) KUNA MZUNGUKO UNAOYUMBA SANA - yaani kila mwezi unaingia siku tofauti ama mbele au nyuma kwa siku zadi ya 5
mfano wa mzunguko unaoyumba sana ni kama ifuatayo
- july ana mzunguko wa siku 26
- june anamzunguko wa siku 20
- maya ana mzunguko wa siku 35

(4) Kuna pia wenye mzunguko mfupi lakini au ni mzunguko kamili, unaoyumba kidogo au unayumba sana
(5) kuna wenye mzunguko mrefu lakini au ni kamili au mzunguko unaoyumba.

Sasa ukisha ujua mzunguko wako wa hedhi ni wa siku ngapi na ni wa aina gani basi inakuwa rahisi sasa kutumia siku hizo kwa ajili ya kubashiri mzunguko wa mwezi unaofuata, na kujua ni siku gani itakuwa hatari, salama, ya mimba na ya mtoto wa jinsia gani

Mfano mzunguko mrefu ni wa kuanzia siku 30 kwenda juu hadi 35. Mzunguko wa zaidi ya siku 35 haupo na haufai
Mzunguko mfupi ni kati ya siku 21 hadi 24, mzunguko wa siku chini ya 20 haupo na kama upo sio mzuri kwa kuwa yale matukio muhimu kwa ajili ya uumbaji wa mayi ya mwanamke hayatatimia

SOMO LITAKALO FUATA NI
- JINSI GANI UTATUMIA MZUNGUKO WAKO WA HEDHI ANA AINA YA MZUNGUKO ULIONAO KWA AJILI YA
- Kubashiri mzunguko unaofuta
- kujua siku salama
- kujua siku ya kupata mimba
- kujua siku za hatari
- kujua siku uzazi.

SEHEMU YA TATU
UKOKOTAOJI WA SIKU ZA MIMBA, SIKU ZA HATARI NA SIKU SALAMA KWA KUTUMIA MZUNGUKO WA HEDHI WA MWANAMKE.

Katika somo lilopita tulijifunza aina ya mizunguko ya hedhi na tukajua ya kwamba wanawake wanaweza kuwa na mizunguko ya aina mbalimbali, katika Maisha yao. Na mizunguko yenyewe ni kama
- mzunguko mrefu
- mzunguko mfupi
- mzunguko wa kawaida

Pia kuna mizunguko mingine inayotokana na namna unavyoingia kwenye siku zako za hedhi, na mfano ni kama ifuatavyo
- mzunguko kamili, kila mwezi unaingia bleed tarehe ileile
- mzunguko unaoyumba, kila mwezi unaingia bleed tarehe tofauti au zinarudi nyuma au kwenda mbele
- mzunguko unaoyumba sana, yani tofauti ya urefu wa mzunguko mmoja na mwingine inakuwa zaidi ya siku 4
Kwa hiyo leo tunaangalia namna ya kutumia mizunguko hiyo kwa ajili ya kukotoa siku zako za hedhi na siku salama na za mimba. Kumbuka ya kwamba kutokana na utofauti wa mizunguko ya hedhi basi kunakuwa na mbinu mbalimbali za kukokotoa siku salama na siku za hatari na za mimba. Kwa hiyo tutaanza na mzunguko usioyumba au mzunguko uliokamilika.

1- MZUNGUKO WA HEDHI USIYOYUMBA

Ikiwa mzunguko wako wa mwezi wa 7, 8 na 9 umekuwa wa siku 26 (angalia juu namna ya kuhesabu mzunguko wako wa hedhi). Basi ni rahisi kusema mzunguko wako wa hedhi kwa kawaida ni siku 26. Na hapa utatumia ile njia ya kawaida ya kuhesabu siku zako ukianzia na siku ya kwanza umepata bleed.

Mfano
- Mwezi wa 7 Nuranonga alikuwa na mzunguko wa hedhi wa siku 26.
- Mwezi wa 8 Nuranonga alikuwa na mzunguko wa hedhi wa siku 26.
- Mwezi wa 9 Nuranonga alikuwa na mzunguko wa hedhi wa siku 26.

Kwa hiyo ni rahisi sana kusema mzunguko wa Nuranonga kwa mwezi wa 10 utakuwa wa siku 26, kwa sababu historia ya Nura inaomnyesha ya kwamba huwa anachukua siku 26 kupata hedhi ingine tangia awe amepata hedhi iliyopita.

Kwa hiyo tutatumia historia ya mzunguko wa Nuranonga uliokuwa kamili kuweza kubashiri
- siku za hedhi za Nuranonga za mwezi wa 10
- siku za hatari za Nuranonga za mwezi wa 10
- siku za mimba za Nuranonga za mwezi wa 10


KWANZA rudi kwenye kalenda yako kujua ni lini ulipata hedhi kwa mwezi wa 9. Utakuta kwa mfano ulipata hedhi tarehe 30/09/2017. Kwa hiyo tarehe 30-09-2017 ilikuwa siku ya kwanza ya mzunguko wa hedhi wa Nura na tarehe 01-10-2017 ilikuwa siku ya pili. Na leo kwa mfano tareh 22-10-2017 ni siku ya 24. Kwa hiyo siku ya hedhi ya Nura inakaribia sana, infact inafaa leo hii Nura aanze kuona dalili za kupata bleed. Siku ya 26 itakuwa tarehe 24-10-2017.

ILI KUJUA SIKU YA MIMBA YA NURANONGA

- toa siku 14 kutoka siku 26 za mzunguko wa hedhi wa Nura yaani 26-14 = 12. Utakuja kujua baadae kwa nini tunatoa na 14.
- kwa hiyo siku ya kupata mimba ya Nuranonga ni siku ya 12 ambayo ilikuwa ni tarehe 11-10-2017 siku ya Jumatano. Hiyo ndio siku ya yai kuungana na mbegu za kiume kama Nura atafanya tendo la ndoa siku hiyo na kukutana na mbegu za kiume zenye afya bora. Hapa pia inafaa ujue ya kwamba – siku ya kupata mimba ni tofauti na siku za uzazi – siku ya kupata mimba ni moja tu kwa kuwa yai huishi masaa24 tu baada ya kutoka katika mfuko wake wa mayai (ovulation) kwa hiyo kama utafanya tendo la ndoa siku 4 kabla ya siku ya 12 au siku 4 kabla ya tarehe 11 bado kuna uwezekano wa kupata mimba, kwa kuwa mbegu za kiume huweza ishi ndani ya uke kwa muda wa masaa zaidi ya 72 yaani siku 3+.
Kwa hiyo siku za uzazi ni siku yenyewe ya kupata mimba yaani siku ya 12, na siku nne kabla, yaani 12-4 = 8. Siku zote kuanzia siku ya 8,9,10,11,12 ni ziku za mimba, lakini mimba itatungwa siku ya 12. Yaani tarehe 11, kwa hiyo kuanzia tarehe 7 au siku ya 8 hadi tarehe 11 au siku ya 12 kwa Nura zilikuwa siku za mimba.

Siku za hatari kwa Nura Hapa pia kuna jambo unatakiwa ujifunze, siku za hatari ni kwa yule asiyetaka kupata mimba, kama wewe unatafuta mimba huwezi kuita siku za hatari au danger days, kwa kuwa wewe huna hatari yeyote ya kutaka mimba. Maneni haya hutumika na wale tu wasiotaka kupata mimba, kwa hiyo wanakwepa kabisa wasipate mimba. Hivyo huziita siku za danger au za hatari.

Ili ukwepe kabisa kabisa usipate mimba basi chukua mzunguko wako tafuta siku ya kupata mimba then ongeza siku 4 mbele na siku 4 nyuma ya mzunguko. Yaani kama una mzunguko wa siku 26 unafanya hivi 26-14 = unapata 12 then unatoa na 4 unapata 8 alafu 14 unaongeza na 4 unapata 16.

Kwa hiyo siku ya kwanza ya hatari kwako ni siku ya 8 ya mzunguko wako wa hedhi na siku a ya mwisho ya hatari yako ya kupata mimba ni siku ya 16. Unaweza jiuliza kwa nini uwe na wasiwasi na siku 4 baada ya yai kutoka? Kumbuka hizi ni hesabu tu, kiukweli mwili wako unaweza badilika saa yeyote na wiki yeyote nan kujikuta siku zako za uzazi zinabadilia, na kama ulikuwa hutaki kupata mimba ukajishtukia unapata. Kawaida sababu za kawaida zinaweza yumbisha mzunguko wako kwa siku 4 tu zaidi ya hapo kunakuwa na tatizo kubwa.

Kwa hiyo kwa mzunguko wa siku 26, uliokamilika.
1- siku ya kutungwa mimba ni siku ya 12
2- siku za uzazi ni siku ya 8,9,10,11 na 12
3- siku za hatari ni kuanzia siku ya 8 hadi ya 16.
4- Siku zote zilizobakia ni siku salama yaani siku ya 1 hadi ya 7, siku ya 17 hadi ya 26

Siku hizi inafaa uwe umeziandika na kuziwekea alama kwenye kalenda yako ya ukutani au notebook.

Kwa sasa tuangalia mwanamke mwingine SNURATA mwenye mzunguko wa siku 28 na mzunguko wake ni kamili. Snurata amenitumia taarifa leo ya kwamba mzunguko wake ni wa siku 28 tangu May 2017.
Yeye huishi mbali na mmewake, bwana yuko Mbeya yeye yuko Njombe.
Na huwa wanaonana kila mwezi mara moja, lakini amekuwa akihangaika kupata mimba, amepima hospitalini wote wameambiwa wako vizuri sana, wako na kilo sawa kabisa, wanaurefu mzuri pia na ni vijana wa miaka chini ya 30.
Kwa hiyo Snurata anaomba ushauri afanyaje ili kupata mimba haraka?

USHAURI WANGU KWA SNURATA
- cha kwanza ni kujua siku ya kutungwa mimba ambayo itakuwa siku ya 14 (28 toa 14) na siku hiyo ya 14 itakuwa siku ya tarehe 04-11-2017 siku ya Jumapili. Bahati iliyoje imeangukia siku ambayo siyo ya kazi. Kwa hiyo siku 4 za uzazi ni kuanzia siku yenyewe ya mimba tarehe 04(Jumapili), tarehe 03(Jumamosi), tarehe 02(Ijumaa), tarehe 01(Alhamisi)

- cha pili mme wa Snurata itafaa ndiye asafiri toka Mbeya kuja Njombe kwa kuwa ikiwa kama unahangaika sana kupata mimba, ni bora bwana ndiye asafiri kutokana na mbadiliko ya haraka ya hali ya hewa ya Njombe na Mbeya. Pengine aombe ruksa kazini ijumaa kabisa.

- cha tatu, itafaa sana Snurata ahakikishe bwanake anakuwa na nguvu za kutosha yaani anatoa mbegu nyingi na anarudia tendo la ndoa mara kwa mara akiweza basi hata 3x2. Jioni mara 3 na asubuhi mara tatu. Hii ni kutumia tu kanuni ya kawaida ya kwamba mbegu zikiwa nyingi basi ni rahis kujitokeza mbegu bora nyingi.

USHAURI KWA MUME WA SNURATA

Wakati akijiandaa kusafiri tarehe 30-10-2017 ili kuwahi siku za uzazi za Snurata kaunzia tarehe 01-11-2017 basi inafaa awe angalau anakula chakula bora, apunguze kunywa pombe na sigara, alale mapema, pia ajaribu kula vyakula vyenye kutia nguvu mwilini, kutia joto na vyakula vyenye kuongeza mawasiliana ya mwili na kuongeza uzalianaji wa mbegu za kiume.
Watajaribu hivyo miezi kadhaa, Mungu sio Athumani, alitoa agizo la kuzaa na kujaza dunia, lazima atasikia kilio chao.

Somo linalofuata tutaangalia namna ya ukokotoaji wa siku za hedhi kwa wanawake wenye mizunguko isiyokamili na wenye hedhi vurugu - USIKAE MBALI

NAMNA YA KUKOKOTAO SIKU ZA SALAMA, HATARI NA SIKU YA MIMBA KWA MTU MWENYE MZUNGUKO UNAOYUMBA KIDOGO

Kumbuka ya kwamba tulisema mizunguko ya hedhi huwa haifanani kwa kila mwanamke na kila mwezi. Hii ni kwa sababu mbalimbali ikiwemo umri na afya saa ingine hata wasiwasi tu. Kuna dada mmoja aliniambia alistuka sana kuona mme wake ana mchepuko, na baada ya hapo mzunguko wake wa hedhi ulivurugika kabisa.... ni kweli hii ni kwa sababu dada huyu alipata stress KUBWA SANA.

KWA HIYO KAMA UNA MZUNGUKO WAKO UNAOKUWA UNAYUMBAYUMBA KILA MWEZI
>>>> basi ni vizuri ukajifunza ukubwa wa myumbuko wako, kama mzunguko wako wa mwezi hadi mwezi hautofautiani kwa siku si zaidi ya tano basi unatumia njia ya wastani kutafuta mzunguko wako wa hedhi wa miezi mitatu, na hatimaye kupata siku za salama, hatari na za uzazi. NDIO NJIA TUTAKAYO IELEZEYA LEO

>>>> kama mzunguko wako wa hedhi unayumba sana, yaani zaidi ya siku 5 basi unatumia njia ya mzunguko mkubwa na mdogo ili kupata siku zako za salama, hatari na siku za uzazi. SOMO LITAFUATA SIKU INGINE

BIG NO - wengine huchukua mizunguko ya mwaka mzima na kutafuta wastani wake, hii inaweza isikupe uhalisia wa mwili wako, kwa kuwa miezi 12 iliyopita unaweza kuta ulikuwa na hali tofauti kabisa na sasa, kwa hiyo njia hii ya wastani inafaa kwa angalau miezi mitatu hadi minne.

MFANO WA EMILIANA.
Mwezi wa KUMI ana mzunguko wa hedhi wa siku 27
Mwezi wa TISA ana mzunguko wa hedhi wa siku 25
Mwezi wa NANE ana mzunguko wa hedhi wa siku 28
Mwezi wa SABA ana mzunguko wa hedhi wa siku 24

Ukiangalia hapo tofauti ya mzunguko mmoja na mwingine ni chini ya siku 5, mzunguko mkubwa ulikuwa mwezi wa 8 wa siku 28, na mzunguko mdogo ulikuwa wa siku 24, tofauti ya siku ni 4 tu. kwa hiyo ni rahisi sana kuchukua siku (27+25+28)/3

AMBAYO UTAPATA YA KWAMBA KWA WASTANI EMALIANA ANA MZUNGUKO WA SIKU 27, na huu ni mzunguko wa kawaida sio mrefu wala sio mfupi.

Kwa hiyo tutatumia mzunguko wa wastani wa Emelia wa siku 27 kwa ajili ya kujua je mwezi wa 11 Emelia atakuwa na siku zipi za hatari, salama na za uzazi?

Ili uweze kufaulu zoezi hili kama kawaida huwa nawambia watu uwe na kalenda, kuhesabu kwa kutumia kichwa ni nzuri pia lakini unaweza jichanganya kirahisi sana...

Ikiwa Emilia amepata hedhi yake mwezi huu wa kumi tarehe 26
1- Je siku yake ya kutungwa mimba (fertilisation) ni ipi?
2- Je siku zake za uzazi (fertile days) ni zipi?
3- Je siku zake za hatari (danger days) ni zipi)
4- Je siku zake salama (free) ni zipi

Kwa kutumia mzunguko wa siku 27 na kwa kufahamu ya kwamba baada ya yai kupevuka mwanamke yeyote huchukua siku 15 hadi kupata hedhi ingine
Na kwa kufahamu yakwamba, mbegu za mwanaume zinaweza ishi ndani ya uke kwa zaidi ya masaa72
Basi tunaweza pata siku za uzazi, hatari na salama za EMILIANA
1f447.png
1f447.png
1f447.png
1f447.png
1f447.png
1f447.png

>>>1- Siku ya kutunga mimba ni siku ya 13, ambayo itakuwa ni tarehe 7/11 siku ya jumanne mwezi wa kumi na moja, weka alama siku hii kwenye kalenda yako - NYOTA YA KIJANI...
>>>2- Kumbuka ya kwamba Emiliana hata akifanya tendo la ndoa tarehe 06/11 bado anaweza pata mimba, hata tarehe 05/11, hata tarehe 04/11, hata tarehe 03/11.... kwa kuwa mbegu za kiume zitaingia na kuendelea kuishi ndani ya uke wa Emiliana, siku ya 13 au tarehe 07/11 yai likitoka tu linakutana na mbegu za kiume... ofcourse kama mbegu za kiume zitakuwa na nguvu na ubora wa kuishi siku zote hizo...
>>>3 -
1f3c3_200d_2640.png
‍♀️
1f3c3_200d_2640.png
‍♀️
1f3c3_200d_2640.png
‍♀️ Ikiwa Emiliana hata taka kupata mimba, basi itafaa kabisa akwepe kufanya tendo la ndoa siku zote 4 kabla ya siku ya mimba (fertilisation) na siku 4 baada ya siku ya kupata mimba

yaani kuanzia siku ya 9 hadi siku ya 17, ambazo ni tarehe 03/11 hadi tarehe 11/11.

>>>4- SIKU SALAMA ni siku zote kuanzia siku ya kwanza amepata hedhi mpaka siku ya kwanza ya hatari na siku zote kuanzia siku ya mwisho ya hatari mpaka siku anapata hedhi ingine
Yaani siku ya 1- 8 na siku ya 18-26 au tarehe 26/10 hadi tarehe 02/11 na tarehe 12/11 hadi 19/11. Tarehe 20 anategemea kupata hedhi ingine

SOMO LINGINE LITAFUTA KWA WALE WENYE MIZUNGUKO INAYOYUMBA SANA.
mfano, mwezi wa kumi ana mzunguko wa siku 35
mwezi wa tisa alikuwa na mzunguko wa siku 29
na mwezi wa nane alikuwa na mzunguko wa siku 21

usikae mbali na JF
 
Mbegu za mwanaume zinauwezo wa kuishi hata siku 5 ukeni hivyo siku za hatari kwa mwanamke ni almost siku 6
 
Somo zuri lenye mifano inayoeleweka. Nina jambo moja hapa. Wengine husema kuwa hata baada ya ovulation day unaweza kuongeza siku mbili zaidi na kuna uwezekano wa kupata je hili ni sahihi au ni lazima iwe kabla na siku yenyewe ya ouvulation?
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom