Mjadala: Je, ni siku zipi ambazo mwanamke huweza kupata ujauzito katika mzunguko wake wa kila mwezi?

princess ariana, Kama umebleed tarehe 21 mwezi wa pili na uka bleed tena tarehe 23 mwezi wa tatu,ina maana mzunguko wako ni wa siku 30 [siku saba za mwezi wa pili zilizosalia kukamilisha siku 28 za mwezi wa pili jumlisha siku 23 za mwezi wa tatu)

Hivyo basi siku ya ovulation hapo inauwekano mkubwa wa kuwa siku ya 16 [yaani 30 -14]. Sasa kama ovulation ni siku ya 16,siku za hatari hapo ni kuhesabu siku nne kabla ya 16 hadi siku tatu baada ya 16 [Yaani siku ya 12 hadi 19 hizo ni hatari].
 
Kama umebleed tarehe 21 mwezi wa pili na uka bleed tena tarehe 23 mwezi wa tatu,ina maana mzunguko wako ni wa siku 30 [siku saba za mwezi wa pili zilizosalia kukamilisha siku 28 za mwezi wa pili jumlisha siku 23 za mwezi wa tatu)

Hivyo basi siku ya ovulation hapo inauwekano mkubwa wa kuwa siku ya 16 [yaani 30 -14]. Sasa kama ovulation ni siku ya 16,siku za hatari hapo ni kuhesabu siku nne kabla ya 16 hadi siku tatu baada ya 16 [Yaani siku ya 12 hadi 19 hizo ni hatari].

Hapa nimeelewa
 
Mkuu nina swali kuhusu concept ya double ovulation is that true? Je unakwepaje mimba katika concept ya double ovulation?
Kwenye utungaji wa mimba kuna ishu ni exceptional na hatuwezi kuzikwepa,kumbuka hata hiyo calenda method bado ina shindwa mara nyingi tu,kuna concept kama zifuatazo kwa mfano.

Superfecundation:ambapo mayai zaidi ya moja yanarutubishwa kwenye kizazi katika vipindi tofauti lakini ndani ya siku za mzunguko huo.

Kwa mfano kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28,ovulation ya kwanza inatokea siku ya 14 na fertilization kufanyika,ovulation inatokea tena siku tuseme ya 24 na fertilization kufanyika,matukio yote yametokeaa ndani ya mzunguko uleule [kabla ya 28 days].

Superfetation:hapa fertilization pia inatokea mara mbili,ya kwanza ndani ya siku za mzunguko na yapili nje ya siku za mzunguko.

Kwa mfano mwanamke anamzunguko wa siku 28,fertilization ya kwanza inatokea siku ya 14,halafu fertilization nyingine inatokea baada ya siku ya 28.

Hizo ni condition ni nadra sana,almost hazipo lakini in theory zinaweza tokea. Kwahiyo nikujibu tu kwa ufupi,kuna condition nyingine hatuwezi kufanya chochote
 
Hebu na mie nipe darasa kidogo ili nijue mzunguo wangu ni wa siku ngapi
Mwez wa kwanza nimeingia tarehe 19 - 22
Mwez wa pili tarehe 22 - 26
Mwez wa tatu 20 - 24 mwezi huu wa nne nimeanza leo tarehe 21 naenda siku nne mpaka siku tano.

Msaada please wa kujua mzunguko ni wa siku ngaIpi
 
Kwa nini unazipa sifa ya uhatari? Kwa wanaotafuta mtoto hizo ndio siku muafaka
 
Asante sana, je inakuwa ni tatizo gani linamfanya mwanamke kutokuona siku zake kwa miezi hata miwili halafu mwezi unaofuatia anaanza kuona tena? Hapo unakuta hajabadili hali ya hewa
 
Kwa watu wa Physics hii theory tungemalizia kwa kusema "Other factors remain constant" hizo factor ni kama vile kutokuwepo mabadiliko ya hedhi. Kwenye suala la hedhi za akina dada kuna changamoto nyingi sana ukirely kwenye nadharia hii. Kwa sababu huwa kuna siku kupungua, kuongezeka hata kupitisha miezi hata miwili mitatu, anarudia tena kawaida yake. Mimi nadhani wanasayansi tuje na kipimo kinachoweza kupima ni siku zipi yai limeshuka. Watu wa Biochemistry inawahusu hii.
 
Yaa ni kweli kabisa,bado kuna kazi kubwa sana inabidi ifanyike kuhusu menstrual cycle
 
Asante sana, je inakuwa ni tatizo gani linamfanya mwanamke kutokuona siku zake kwa miezi hata miwili halafu mwezi unaofuatia anaanza kuona tena? Hapo unakuta hajabadili hali ya hewa
Mzunguko wa hedhi una changamoto nyingi,maelezo yaliyo tolewa hapo ni kuhusu mzunguko wa hedhi wa kawaida usio na tatizo lolote[normal menstrual cycle]

Kuna mizunguko isiyo ya kawaida[abnormal menstrual cycle ambayo ina visababishi vingi na vingine sababu zake hazijulikani.

Miongoni mwa mambo yanayoweza sababisha mwanamke kutoona siku zake kwa miezi kadhaa ni pamoja na kutokuwa na uwiano mzuri wa homoni za kike [hormonal imbalance,kufanya mazoezi sana,kuwa na stress, utumiaji wa vidonge vya uzazi wa mpango, kupungua sana uzito, kuumwa sana, baadhi ya magonjwa ya kurithi [kwa mfano Kallman Syndrome, Tuner Syndrome], kutoa mimba kwa kukwangua mfuko wa uzazi (asherman syndrome)
 
Niambieni basi
Mwezi wa kwanza kwenda wa pili siku 33,mwezi wa pili kwenda wa tatu siku 26,mwezi wa tatu kwenda wa nne siku 32,hizo ndo siku za mizunguko yako.

Sijajua miezi iliyopita ulikuwa una bleed kila baada ya siku ngapi.

Bado mzunguko sio mbaya sana,hiyo ishirini na sita ndo imetufautiana na hizo nyingine,lakini inaonesha mzunguko wako ni wa kila baada ya siku thelathini na kitu hapo [tazama hizo 32 na 33 zilivoelekeana].
 
Back
Top Bottom