Zitambue dalili za maradhi ya akili Kama 'Bipolar' na 'schizophrenia '

Andrew Mushi

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
630
696
Kama alivyoagiza Mh Rais tusijadili watu tujadili maendeleo, ktk utekelezaji wa azimio Na kauli ya Rais wetu Mpendwa, napenda nitimize ahadi hio,

Wananchi wengi ktk nchi yetu wanakosa ustadi wa kufahamu maradhi sugu yanayoathiri ndugu zetu tunaoishi nao na kudhani tabia zao ni kawaida tu, kumbe ni out of normal,

Maradhi yenye athari kubwa ya akili, Kama Bipolar na Schizophrenia yaani 1 kati ya 100 tunayo na recent study imeelezwa kwa tz athari yake kubwa mtu 1 kati ya 4, hapa nitajaribu kuelezea baadhi ya dalili ya kila gonjwa, ili tujiwezeshe kupata elimu yake na kuweza kuchukua first step ktk kusaidia waathirika, na tutegemee serikali imejipanga vipi kutokana na haya maradhi sugu ambayo ni janga kwa taifa.

Kwa kuanzia Bipolar dalili ni Kama ifuatavyo:-

Kufoka foka ovyo yaani kuwa na hasira za karibu

Kuwa na wasi wasi

Kutoambilika, kufanya maudhi ya makusudi kwa watu(irritable),

Kuwa na mood swings hususan wakati wa psychosis attack, yaani inaposhambulia

Kupata nguvu za ajabu hatimae kuongea kwa kutumia nguvu pasipo hitajika, vile vile kucheka cheka pasipo chekwa, yaani muathirika hasomeki na familia au jamii iliyomzunguka,

Kutomuangalia mtu USONI unapoongea naye

Kukosa usingizi, kukesha wakati wa kuzidiwa,

Muathirika anafanya maamuzi ya ajabu pasipo kujali athari ya matokeo ya maamuzi yake

Na kwa upande wa Schizophrenia dalili ni Kama ifuatavyo:-

- Kuwa na extreme reaction watu wakikukosoa

- Kuwa na chuki na watu bila ya sababu za msingi. Yaani kucheka au kulia bila mpango

- Kukosa kufurahi na watu

- Kulala sana

- Kutoa statements za ajabu ajabu yaani zisizoeleweka na kutosemeka hata na watu wako wa karibu kama familia

- Kutoa hotuba ambayo haiendani na maudhui au tafrija iliyokuwepo, yaani mara umeongea hili Mara lile, very disorganised and incoherent

Kuwa delusions au kuwaza mambo ya ajabu, na hii inawapata wagonjwa schizophrenia kwa asilimia 90%

Delusion kujihisi wewe ndio una akili sana kuliko wengine wote, unawaona ovyo.

Delusion kujihisi unaonewa, unahisi watu au kikundi cha watu wanataka kukudhuru.

Delusion hata sehemu ya ulinzi na usalama unahisi kama kuna madhara, kwa hio unahitajia excessive protection, yaani hata television unahisi kama adui kwako..

Kutoshirikiana na watu wengine ndani na nje ya nchi, yaani total social withdrawal

Je serikali ya Mh Rais inajipanga vipi kukabiliana a janga hili la taifa, ukizingatia kwa habari zilizokuwepo na takwimu zilizoripotiwa watu 1-4 wana matatizo ya akili,

Ewe Mungu wawafanyie wepesi waathirika na serikali yetu liwekee utatatibu na uzingatio wa kufahamu matatizo haya yanayogusa familia nyingi sana.

Tunaenda, tunarudi, tunaona lkn hii kitu hatuna elimu nayo, iwe ni chanzo cha discussion ktk serikali na private institution Kama hospitali nk. Usiwe mirembe na tuondokana na stigma attached to Mental issues.
 
Duh kuna mgonjwa namfaham ataanza kusema "mnazungumzia mapungufu yangu bila tiba mnanipangia hadi maradhi???"

Mkuu hajatajwa mtu, lakini kitu kimoja tunalipuuzia sana hili swala na hatuna wataalam wengi nchini,

Tatizo kubwa ya hii issue ni very expensive to treat, inahitajia multiple sessions kufanya assessment na treatments, na ndio maana nchi nyingi sana inakua subsidised na government, wakishirikiana na private entities, treatment for every patient is different.

Sio Kama Malaria na maradhi mengine yaani yana uhusiana mmoja
Kwa kila mgonjwa, na treatment yake all the same to each and everyone.

Muhimu kwa serikali kuhamasisha vyuo na college kutoa mafunzo ya psychiatry and counselling, kushirikiano na private sectors kwa kuwawezesha kufungua private clinics through targeted tax incentives nk.

Trust me, it is only going to get worse, na hapo hatujagusia anxiety Kama General Anxiety Disorder(GAD) associated with panic attack, depression na maradhi mengine yanayoathiri akili, ambapo GAD ni very common.
 
Hahahaha..!! Kuna ndugu yangu ana dalili zote hizo halafu ni kiongozi mkubwa
 
Kukosa kufurahi na watu
afu tz ni nchi ya 3 kutoka mwisho kati ya nchi 155 kwa watu wenye furaha kwa ranks za mwaka 2017 na kwa 2016 tulikua wa 149 kati ya nchi 157,
my take, nadhani wagonjwa watakua wengi kuliko tunavyo dhani, somebody should do something
kama hali itaendelea hv nxt year tutakua tunaongoza tokea chini
 
Nimekuelewa sana ndugu.....

Sasa tushauri, tuwatibuje hawa waja??? Maana wapo, kwa dalili hizo, tuna uhakika wapo aiseeee.....tena nimekumbuka, siku moja tuko mahala, mtu mmoja alikuwa akizungumzia mambo ya MWANGA.....ghafla akatokea mwingine, akaanza kuzungumzia MOSHI.....

Tueleze TATUZI aiseee, zisi izi vere siriasi!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom