Zitakuja nyakati tutatamani Magufuli arudi hata siku moja madarakani

Ulichonena kitatokea tu ..subiri muda ..huyu Rais ndio Taifa lilimuhitaji ,ila wapiga dili ,wanaharakati uchwara ndio hawamatak..wapiga kura wanamuhitaji sana
 
Sekta binafsi ndio injini ya uchumi, serikali haiwezi simamia kila kitu. Waafrica hatuna utamaduni na nidhamu ya usimamizi wa mambo.Ni kuzijengea uwezo serikali ibaki kukufanya kodi,Tozo,nk.No ameajiri watu wengi wa moja Kwa moja na wasio wa moja Kwa moja zaidi ya laki Mbili kuanzia viwanda ni,mashambani nk.Kusaidia watu sio kuwapa pesa ya kula mia tano miatano mbele ya macamera.Kuwekeza kwenye nchi moja ni hatari hasa siasa za kiafrica hazitabiliki,chukulia awamu hii ya matajiri kutakiwa washushwe chini waishi kama mashetani, vipi kama umewekeza bongo pekee hali ingekuwa vipi?.Iddi amini na Nyerere Kwa sera zao za kuwashugulikia matajiri Uganda kufukuzwa wahindi,Tz utaifishaji wakati wa Sera za ujamaa lengo likiwa ni kuwafanya watu wawe masikini ili iwe rahisi kuwatala, hapa wafanyabiashara wengi ndipo wakaja na idea ya kuwekeza nchi mbali mbali ili kulinda mitaji yao pale Sera za nchi zinapobadilika.
Nikuambie kitu kwa kifupi tu, wajerumani siku za nyuma wakati wa utawala wa Chancelor Gerhard Schroeder walijaribu kubinafsisha miradi mingi sana ambayo ilikuwa inasimamiwa na serikali yao.

Baada ya mda sio mrefu miradi mingi ilirudi tena mikononi mwa serikali. Unajua kwa nini? Kwasababu sekta binafsi ilitaka kuendesha hiyo miradi kwa mtindo wa " profit maximization" kitu ambacho hakikuwa rahisi kwa wawekezaji.

Ili kufanya hivyo walilazimika kuchukua baadhi ya hatua kama ku-reduce idadi ya wafanyakazi na kupunguza efficience au ufanisi wa Services ili ku-garantii ubora wa services. Matokeo yake serikali ilipata mzigo mkubwa wa kuwahudumia watu wake katika mahitaji muhimu kama energy, maji na huduma nyingine za kimaisha ikiwemo chakula na makazi.

Deutsche Bahn kwa mfano ni kampuni ambayo inatoa huduma za transport ya abria na mzigo kwa njia ya reli. Hili shirika liko to 100% chini ya serikali yao.

Hili sjirika sio tu linatoa service bali linajihusha na mambo mengi ya kiteknolojia. Majaribio mengi yanfanyika chini ya Deutsche Bahn iwe kwa faida au bila faida. Sasa niambie sekta gani binafsi iko tayari kufanya majaribio ya teknologia bila faida Tanzania?

Usi dream ndugu yangu. Ukiona vya elea ujue vimeumbwa.

Naomba mwuulize Mohamed Dewj kama yuko tayari kuwekeza kwa hao vijana walio tengeneza gari kwa kutumia baterii, usikie atakuambia nini.

Mnajua nyie wengi wenu mna maisha ya kasuku. Mkisikia jambo mtu amelitoa basi mna dakia bila kujiuliza ni kweli au sio? Inawezekana au haiwezekani?

Sekta bina is always destructive katika maisha ya community. Sitapenda kutoa maelezo mengi ukashindwa kusoma. Maana maelezo yangu nafikiri yanawachosha.

Naomba fanya uchunguzi wa kina wewe mwenyewe, ukiwa uko tayari na kama una maswali unaweza ukaniuliza tena.

Ulimwengu unahitaji sekta binafsi katika mfumo wa "Worker Cooperative" na sio capitalism kama hivi sasa. Sisi binadam tuna ung'ang'ania huo mfumo kwa sababu ya mazara, lakini ukweli wa mambo unatakiwa kubadilishwa haraka sana. Huko tunako kwenda utabadilishwa tu tutake tusitake.

Hizo mia tano tano za Magufuli zisikupe shida. Hata uwanaja wa ndege wa Chato usikubabaishe. Chato haishi Magufuli chato wako wa Tanzania. Ni vizuri wakiwa na kwanza wa ndege kwani hata wewe ilitaka unaweza kwenda uchi huko hakuna atakaye kufukuzwa.

Mmmmh! Wafanya biashara hawako Tanzania na Uganda tuna pia biashara haija anza na sisi. Hiyo ya ID Amini Dada kuwafukuza wahindi zilikuwa sababu zake binafsi. Nyerere haja fanya hivyo.

Naomba kama una nafasi basi wasikilize hawa waamerika wawili utajifunza mengi kuhusu sekta binafsi!

Nashukuru na wewe umegundua kuwa unatuchosha na utopia zako. Uchumi wa umma umefeli na uliondoka baada ya communist block kuanguka mwaka 1989 enzi za Gorbachev kwa falsafa ya Perestroika na Glasnost.

Hata kwenye syllabus vijana hawasomi tena Marxist-Leninist theories kama mfumo wa uchumi siasa, bali wanataja kidogo kama historia.

Wakeup bro Maneno Meier diaspora inakuharibu
 
Ukipita mitandaoni utaona baadhi ya vijana wanavyolalamika bila Sababu

Wanamlaumu Rais magufuli kwamba maisha magumu
Ati zile maisha magumu zimeripotiwa na Rais wetu mpendwa

Tuliobahatika kuishi awamu zote tano Tunajua Mambo yalivyo na yalivyokuwa

Sisi wengine tumejifunza somo la uvumilivu tulivumilia hali ngumu kipindi cha Nyerere kutokana na Nchi yetu chini ya Nyerere kuwapinga mabeberu kwa vitendo

Mabeberu walifanya kila hila kimkwamisha Nyerere ila Kwasababu tulijua Nyerere anachopigania tulimvumilia hatukutaka tuwe wasaliti Ndani ya nchi yetu na Alifanya kazi kubwa

Baada ya hapo walipita ma Rais watatu kabla ya magufuli na walifanya kadri ya wawezavyo kuijenga Tanzania ila alipokuja magufuli tulipiga magoti kumshukuru Mungu tulijua magufuli ni nani na anataka nini
Nilikuwapo pale uhuru wakati magufuli akiapishwa sio siri nilitokwa na machozi nilimwona pia kadinali pengo akiifuta mawani yake bila shaka alitokwa na machozi

Siku ile mvua ilinyesha sana sikumbuki maneno mengi ya magufuli ila nakumbuka mstari mmoja tu alisema NiTAANZA KAZI LEO LEO Hii sentensi iliniamsha Ari ya uzalendo ule niliouamini kutoka kwa Baba wa Taifa mwl.Nyerere

Moja ya ziara za kwanza kabisa ya magufuli ilikuwa ni pale BOT baada ya ziara alisema banki kuu ni kama haina fedha maana yake zilitembea na wahuni kutokana na upole wa kikwete

Tuliomwamini magufuli tuliendelea kumwombea tulijua nguvu ya mafisadi katika Nchi Hizi maskini ni kubwa sana tulijua mafisadi watutumia kila mbinu kumkwamisha ni kweli wengine walihamisha pesa zao wengine walifunga biashara wengine walifanya kila aina ya ufedhuli kuhakikisha magufuli anakwama

Lakini miaka minne baadae Mzee yupo imara zaidi maadui zake wapo hoi wengine waliamua kuonyesha hasira zao hadharani kwa kumhujumu

Mimi binafsi nafurahi mwenyezi Mungu kunijalia uhai kushudia maajabu ya awamu ya tano awamu iliyojaa uzalendo,kupenda wananchi wake na kupigania maslahi ya Nchi
Ni bahati mbaya sana kuna baadhi ya wanasiasa na watu wasio wazalendo wanakubali kutumika na mabeberu ila hawatafanikiwa

Mimi nitawasilimua wajukuu wangu uzalendo wa Huyu msukuma toka kanda ya ziwa aliyeamua kuitengeneza ile Tanzania ya Nyerere aliyoitarajia

Ahsante magufuli ipo siku wanaokubeza watatamani urudi Ikulu hata saa moja tu urekebishe Mambo
Kwani ni ngumu kupata Rais mwaminifu na mchapa kazi kama wewe
Nakuelewa sana bro ni kweli hi nchi ilifika sehemu akawa anahitajika raisi km Magu watu walikuwa wanapiga tu kisa baba yangu raisi
Tuliobakia tukawa tunaonekana mafara sasa hivi tunaheshimiana
 
Na mimi sikatai kuwa kujenga uchumi sio swala la mwaka mmoja mkuu ila kulingana na hali ilivyo hivi sasa serikali hainabudi kumwaga pesa katika miradi mbali mbali mikubwa ili wananchi wapate ajira. Na kama unavyojua kuwa ajira ni kipato kwa mtu mmoja mmoja.

Sielewi kwa nini Rais Magufuli aweke reserve ya US Dollar bilioni sita ya nini? Hizo hela si angezitumia tu kwenye projects tofauti ambazo zitaisaidia nchi kupata maendeleo?

Wewe unajua kuwa Tanzania tuko nyuma sana kwenye mambo ya Telecomuniction technogy kama 5G na mambo ya satellite technology kwanini asitilie mkazo hizi technologies zikatusaidia baadae?

Asiwaze kuingiza faida tu bali pia ajifunze ku invest kwa faida ya baadae pia. Investment isiwe one sided kwenye majengo na madaraja mazuri na barabara tu isipokuwa pia kwenye technologies za baadae kwa vijana wetu. Haya ni mambo ambayo wanafunzi wetu wanatakiwa kujifunza vyuoni.

Ili vijana wetu wawe competitive baadae lazima wawe wamesindikwa imara kiteknolojia na sio tu kuimiza uchuuzi wa umachinga. Kwa hali hii hatuwezi jenga vijana ambao watajiamini baadae kamwe.

Serikali lazima iweke mikakati madhubuti ya maisha yetu na vijana wetu baadae.

Anacho kifanya mpaka sasa ni kitu vizuri sana ila kwa mtazamo wangu naona hiyo miradi yaliyo ianzisha bado haitoshi kuwawezesha watanzania wengi wakawa na ajira. Rais Magufuli anatakiwa aachie pesa kwenye miradi mingi na sio kukumbatia pesa.

Sioni sababu ya kukumbatia pesa wakati nchi bado tuna rasilimali kubwa. It doesn't make any sence!

Kama kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma, hilo kwa kiasi kikubwa amefanikiwa, lakini hai-justfy kuwa aendelee kubana matumizi yenye tija wakati wananchi wanaumia kwa kukosa pesa za kuendesha maisha yao. Ina msaidia nani?

To be honest, haya mambo ya kuwa-motivate wamachinga peke yake is a ridiculous thing. Wamachinga wana potential gani ya kusaidia kuinua uchumi wa hii nchi na kuleta maendeleo ya kweli?

Magufuli ni mwoga wa ku-deal na Diaspora. Hajui kuwa hawa watu baadhi yao wana exposure kubwa ya kusaidia nchi yetu kwenye maendeleo.

Nilimsikia siku akiisifu Morocco kuwa ina watalii wengi kwa mwaka kuliko sisi, kitu ambacho hajui ni kwamba wamoroko wana dual citzenship sisi hatuna. Waturuki wana dual cutzenship pia na ndiyo maana wame fanikiwa kupiga hatua katika technology kama hii ya SGR mpaka sasa.

Watu wanashida ya kipato. Amwage tu pesa kwenye miradi mingi itakuja kulipa baadae ninauhakika. Kulimbikiza pesa nyingi hajui marais watakao kuja baadae watakuwa na msimamo gani? Watazila pesa zote na wananchi hawata ambulia kitu. Je, atakuwa amekamilisha ndoto zake za kuwasaidia wanyonge?

Yeye na Rais Nyerere ni exceptionals wanatakiwa wawe saints, lakini hao wengine wote ni wabinafsi. Watazipiga hizo hela kwa manufaa yao. Hatujui lini tutapata marais kama hawa wawili tena.
mtu anaye tamani maraika afunge mitandao ndiye unayetaka awekeze kwenye technology ya 5G ! hiyo nisawa na kumwambia kibaka avae nguo nyeupe usiku akiwa anaingia kwenye nyumba za watu kuchomoa tv.
 
Nakuelewa sana bro ni kweli hi nchi ilifika sehemu akawa anahitajika raisi km Magu watu walikuwa wanapiga tu kisa baba yangu raisi
Tuliobakia tukawa tunaonekana mafara sasa hivi tunaheshimiana
Hata sasa hivi wewe bado fala kwa vile akina Bashite, Mnyeti na wasukuma wengine ndiyo zamu yao kupiga
 
Nashukuru na wewe umegundua kuwa unatuchosha na utopia zako. Uchumi wa umma umefeli na uliondoka baada ya communist block kuanguka mwaka 1989 enzi za Gorbachev kwa falsafa ya Perestroika na Glasnost.

Hata kwenye syllabus vijana hawasomi tena Marxist-Leninist theories kama mfumo wa uchumi siasa, bali wanataja kidogo kama historia.

Wakeup bro Maneno Meier diaspora inakuharibu
Naomba kuanzia leo katika maisha yako jaribu kutofautisha kati ya Marxism na Socialism au Communism. Vinginevyo utaumbuka vibaya sana.

Usijifanye umesoma kitabu cha Carl Marx "DAS KAPITAL" ukajikuta uko kwenye ideology ya Socialism ya warusi na wachina au Korea ya Kaskazini.

Nchi zote za kishosalist ikiwemo Tanzania zili missuse maandishi ya Carl Marx kwenye kitabu chake "DAS KAPITAL" kwa faida zao.

Carl Marx kwenye kitabu chake "DAS KAPITAL" (Samahani natumia neno la kijerumani kwa sababu nimesoma kwa kijerumani) haku dokeza chochote kuhusu u-communism au u-socialism kwa misingi ya Perestroika (Friedom of Press) na Glasnost (Transparency) ya Soviet Union.

Carl Marx alikuwa amejikita kwenye "Socialism at work place" wakati wa industrial Revolution in England na Amerika, akiwahamasisha wafanyakazi kudai haki zao za partcipation kweye profit na conditions nzuri za kazi.

Wewe utakuwa umesoma Carl Marx version ya warusi ambako umetwika madude mengine ambayo hayahusiani chochote na Carl Marx kwenye Capitalism England. Be careful utaumbuka?

Kwa taarifa yako kama hujui Amerika na Europe hivi sasa discussion kubwa sana inatokea kuhusu System ya capitalism.
Watu wengi wana hoji kama hiyo System iko up to date, maana takwimu zinaonyesha kupanda kwa uchumi, lakini maisha ya wafanya kazi yanazidi kuwa mabaya?

Ni mfumo gani huo wa uchumi ambao wafanyakazi wana henyeka, Amerika wengine wanafanya kazi mbili, lakini mshahara hautoshi ku-afford vitu vingi bila credit card?
 
mtu anaye tamani maraika afunge mitandao ndiye unayetaka awekeze kwenye technology ya 5G ! hiyo nisawa na kumwambia kibaka avae nguo nyeupe usiku akiwa anaingia kwenye nyumba za watu kuchomoa tv.
Mawazo yako ni ya kiwiziwizi! Acha ujinga wewe. Amka ujifunze maisha ya kisasa badalanya kusikiliza gumzo la kijiweni.
 
Kweli tunatofautiana maono, yaani na huyu Magufuri unamfananisha na Nyerere na kumuita saint?? Hata shetani ameshituka alipoona maandishi yako, anyway kumbe wewe ni diaspora
Asante mkuu umenifurahisha sana.

Any way turudi kwenye mada yetu. Ina maana kuwa Diaspora ni dhambi?

Hapana mimi hivi sasa niko hapa hapa kwetu Bongo ila nilikwenda ujerumani kusoma na nika bahatika kuishi huko mda mrefu sana nikifanya kazi. Kwa sababu nina familia yangu huko sometimes huwa naenda huko kutembelea watoto na wajukuu zangu.

Naweza sema ujerumani kwa mimi pia ni nyumbani kama hapa Bongo na hasa Berlin.
 
Sidhani kama kuna MTU anatamani IDD Amin arudi huko Uganda
Ukipita mitandaoni utaona baadhi ya vijana wanavyolalamika bila Sababu

Wanamlaumu Rais magufuli kwamba maisha magumu
Ati zile maisha magumu zimeripotiwa na Rais wetu mpendwa

Tuliobahatika kuishi awamu zote tano Tunajua Mambo yalivyo na yalivyokuwa

Sisi wengine tumejifunza somo la uvumilivu tulivumilia hali ngumu kipindi cha Nyerere kutokana na Nchi yetu chini ya Nyerere kuwapinga mabeberu kwa vitendo

Mabeberu walifanya kila hila kimkwamisha Nyerere ila Kwasababu tulijua Nyerere anachopigania tulimvumilia hatukutaka tuwe wasaliti Ndani ya nchi yetu na Alifanya kazi kubwa

Baada ya hapo walipita ma Rais watatu kabla ya magufuli na walifanya kadri ya wawezavyo kuijenga Tanzania ila alipokuja magufuli tulipiga magoti kumshukuru Mungu tulijua magufuli ni nani na anataka nini
Nilikuwapo pale uhuru wakati magufuli akiapishwa sio siri nilitokwa na machozi nilimwona pia kadinali pengo akiifuta mawani yake bila shaka alitokwa na machozi

Siku ile mvua ilinyesha sana sikumbuki maneno mengi ya magufuli ila nakumbuka mstari mmoja tu alisema NiTAANZA KAZI LEO LEO Hii sentensi iliniamsha Ari ya uzalendo ule niliouamini kutoka kwa Baba wa Taifa mwl.Nyerere

Moja ya ziara za kwanza kabisa ya magufuli ilikuwa ni pale BOT baada ya ziara alisema banki kuu ni kama haina fedha maana yake zilitembea na wahuni kutokana na upole wa kikwete

Tuliomwamini magufuli tuliendelea kumwombea tulijua nguvu ya mafisadi katika Nchi Hizi maskini ni kubwa sana tulijua mafisadi watutumia kila mbinu kumkwamisha ni kweli wengine walihamisha pesa zao wengine walifunga biashara wengine walifanya kila aina ya ufedhuli kuhakikisha magufuli anakwama

Lakini miaka minne baadae Mzee yupo imara zaidi maadui zake wapo hoi wengine waliamua kuonyesha hasira zao hadharani kwa kumhujumu

Mimi binafsi nafurahi mwenyezi Mungu kunijalia uhai kushudia maajabu ya awamu ya tano awamu iliyojaa uzalendo,kupenda wananchi wake na kupigania maslahi ya Nchi
Ni bahati mbaya sana kuna baadhi ya wanasiasa na watu wasio wazalendo wanakubali kutumika na mabeberu ila hawatafanikiwa

Mimi nitawasilimua wajukuu wangu uzalendo wa Huyu msukuma toka kanda ya ziwa aliyeamua kuitengeneza ile Tanzania ya Nyerere aliyoitarajia

Ahsante magufuli ipo siku wanaokubeza watatamani urudi Ikulu hata saa moja tu urekebishe Mambo
Kwani ni ngumu kupata Rais mwaminifu na mchapa kazi kama wewe
 
Asante mkuu umenifurahisha sana.

Any way turudi kwenye mada yetu. Ina maana kuwa Diaspora ni dhambi?

Hapana mimi hivi sasa niko hapa hapa kwetu Bongo ila nilikwenda ujerumani kusoma na nika bahatika kuishi huko mda mrefu sana nikifanya kazi. Kwa sababu nina familia yangu huko sometimes huwa naenda huko kutembelea watoto na wajukuu zangu.

Naweza sema ujerumani kwa mimi pia ni nyumbani kama hapa Bongo na hasa Berlin.
Mawazo yako na speed sana. Unafiikiria vitu vikubwa sana kutatua mambo mepesi. Sina nia ya kuku embarass lakini nataka niseme issues nyingi zinakosewa na viongozi wetu. Hebu fikiria ni kazi ngapi zimepotea kwa chuki binafsi ya Jiwe dhidi ya Yusuf Manji. Manji through makampuni yake alikuwa anaajiri watu kwa maelfu. Mtu mmoja mwenye madaraka ana kisasi naye amemvuruga na Manji kafunga viwanda na ahughuli zake yuko Canada. Wanao suffer ni Watanzania waliokuwa wanafanya kazi kwenye makampuni yake.
 
Uhuni wako wa mtaani usiuhsmishie hapa kama bangi zimekuchosha hamia kwenye ngada
Mjinga kabisa we
Ati yupo kutoa laana huyo mchumia tumbo

Apambane kuileta familia yake maisha bora
Usikae kufikiri kila mmoja anawaza mambo zako kichwani

Sisi ni wazalendo tupo imara kupigania wapotoshaji washindwe km wewe

Kazi ya magufuli inatambulika
Labda wapo radhia watoto wao wewe kuhudumiwa na magufuli wakiketi nyumbani bila kazi

Wajinga sana hawa

Nimekwoti baadhi ya majibu yako....

Unaonekana kupaniki sana mzee wangu uliyezishuhudia tawala za awamu zote tano Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli......

Nadhani hukutegemea andiko lako kutopata uungwaji mkono wa kiwango hiki kutoka kwa wajumbe wengi bila shaka......

Pole sana mzee wangu......

USHAURI:

Ukileta hoja, jaribu kufokasi kwenye lengo la hoja yako. Wanaojadili kistaraabu unawajibu kistaarabu....

Unaohisi wanakukejeli na wakitaka kukutoa kwenye mstari, usiwadharau bali wote hao onyesha appreciation kwa michango yao kwa ingalao ku - like comment zao.....

Si lazima uwajibu kama unadhani hakuna cha kujibu.....

Wewe waache hivyo hivyo, achana na tabia ya kurushiana vijembe na matusi eti tu kwa sbb mtu hajajibu upendavyo wewe....

Kinachonishangaza zaidi mimi, ni umri wako kuwa mkubwa kwani umejinasibu kuwa umeziona na kuziishi awamu zote za tawala za taifa hili kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli....

Kwa hiyo ni wazi umri wako umekwenda kidogo miaka pengine si chini ya 60.....

Kwa mukutadha huu, kama unaanzisha mjadala na kisha kuusimamia kwa kujibu hoja za wachangiaji kwa staili na kwa kutumia lugha hii, napata shaka na busara na hekima yako....!!

Kwa maoni yangu, ni makosa sana kuwaita watu wanaotofautiana na mtazamo wako juu ya uongozi wa Magufuli kama Rais kuwa ni wajinga na aina nyingine za matusi....

Kama huwezi kuwa mvumilivu na mwenye subira, nakushauri usiwe na account zozote ktk social media vinginevyo utam- block kila mtu.....

Bahati tu kuwa hapa JF huna uwezo huo.....

Unachoweza kukifanya kwa ushauri wangu na kama huna ngozi ngumu ya kuvumilia kukosolewa, usianzishe mada (mjadala) wowote humu, vinginevyo utamtukana kila mtu.....

Sasa hiyo ni mbaya sana maana utadhihirisha na kujifunua wazi kuwa wewe ni mtu wa namna gani.....

Mpaka hapa mimi nimeshakuelewa na kukufahamu tayari. Kuwa wewe ni Mzee mwenye shida kidogo upstairs na unahitaji kusaidiwa....!!

Mimi ni kijana mdogo tu. Nikiwa na akili za utu uzima nikisoma sekondari nimeanza kuuona utawala wa Mkapa na kidogo nikiwa mtoto utawala wa Mwinyi. Lakini naweza kukushauri na uahauri wangu ndiyo huu...uzingatie.....

Asante, nakutakia kila la kheri
 
Nimekwoti baadhi ya majibu yako....

Unaonekana kupaniki sana mkubwa...

Hukutegemea andiko lako kutoungwa mkono na wajumbe wengi bila shaka, au siyo bwana?

USHAURI:

Ukileta hoja, jaribu kufokasi kwenye lengo la hoja yako. Wanaojadili kistaraabu unawajibu kistaarabu....

Unaohisi wanakukejeli, una - like comment zao kisha unawaacha hivyo hivyo bila kuanza kurushiana vijembe na matusi....

Kinachonishangaza zaidi mimi, ni umri wako kuwa mkubwa kwani umejinasibu kuwa umeziona na kuziishi awamu zote za utawala kuanzia Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na sasa Magufuli....ni wazi una umri wa miaka pengine zaidi ya 60.....

Kwa mukutadha huu, kama unaanzisha mjadala na kisha kuusimamia kwa kujibu hoja za wachangiaji kwa staili na kwa kutumia lugha hii, napata shaka na busara na hekima yako....!!

Kwa maoni yangu, ni makosa sana kuwaita watu wanaotofautiana na mtazamo wako juu ya uongozi wa Magufuli kama Rais kuwa ni wajinga na aina nyingine za matusi....

Kama huwezi kuwa mvumilivu na mwenye subira, nakushauri usiwe na account zozote ktk social media vinginevyo utam- block kila mtu.....

Bahati tu kuwa hapa JF huna uwezo huo. Unachoweza kukifanya kwa unziahauri wangu kama huna ngozi ngumu ya kuvumilia kukosolewa, usianzishe mada (mjadala) wowote humu, vinginevyo utamtukana kila mtu.....

Sasa hiyo ni mbaya sana maana utadhihiriaha na kujifunua wazi kuwa wewe ni mtu wa namna gani.....

Mpaka hapa mimi nimeshakuelewa na kukufahamu tayari. Kuwa wewe ni Mzee mwenye shida kidogo up stairs na unajitaji kusaidiwa....!!

Asante, nakutakia kila la kheri
Naamini huyu Mikocheni Junction ni kati ya wale wanaoitwa Buku 7 wa Lumumba. Wapo tayari kubisha na kutetea hata vitu vya kijinga ambavyo Serikali inafanya. Wanadhalilisha elimu zao kama wamesoma na heahima zao kwenye jamii. Kama hajakuelewa kwenye hiyo ushauri uliompa basi amekwisha.
 
Back
Top Bottom