Zitakuja nyakati tutatamani Magufuli arudi hata siku moja madarakani

Kawe Alumni

JF-Expert Member
Mar 20, 2019
8,685
11,988
Ukipita mitandaoni utaona baadhi ya vijana wanavyolalamika bila Sababu

Wanamlaumu Rais magufuli kwamba maisha magumu
Ati zile maisha magumu zimeripotiwa na Rais wetu mpendwa

Tuliobahatika kuishi awamu zote tano Tunajua Mambo yalivyo na yalivyokuwa

Sisi wengine tumejifunza somo la uvumilivu tulivumilia hali ngumu kipindi cha Nyerere kutokana na Nchi yetu chini ya Nyerere kuwapinga mabeberu kwa vitendo

Mabeberu walifanya kila hila kimkwamisha Nyerere ila Kwasababu tulijua Nyerere anachopigania tulimvumilia hatukutaka tuwe wasaliti Ndani ya nchi yetu na Alifanya kazi kubwa

Baada ya hapo walipita ma Rais watatu kabla ya magufuli na walifanya kadri ya wawezavyo kuijenga Tanzania ila alipokuja magufuli tulipiga magoti kumshukuru Mungu tulijua magufuli ni nani na anataka nini
Nilikuwapo pale uhuru wakati magufuli akiapishwa sio siri nilitokwa na machozi nilimwona pia kadinali pengo akiifuta mawani yake bila shaka alitokwa na machozi

Siku ile mvua ilinyesha sana sikumbuki maneno mengi ya magufuli ila nakumbuka mstari mmoja tu alisema NiTAANZA KAZI LEO LEO Hii sentensi iliniamsha Ari ya uzalendo ule niliouamini kutoka kwa Baba wa Taifa mwl.Nyerere

Moja ya ziara za kwanza kabisa ya magufuli ilikuwa ni pale BOT baada ya ziara alisema banki kuu ni kama haina fedha maana yake zilitembea na wahuni kutokana na upole wa kikwete

Tuliomwamini magufuli tuliendelea kumwombea tulijua nguvu ya mafisadi katika Nchi Hizi maskini ni kubwa sana tulijua mafisadi watutumia kila mbinu kumkwamisha ni kweli wengine walihamisha pesa zao wengine walifunga biashara wengine walifanya kila aina ya ufedhuli kuhakikisha magufuli anakwama

Lakini miaka minne baadae Mzee yupo imara zaidi maadui zake wapo hoi wengine waliamua kuonyesha hasira zao hadharani kwa kumhujumu

Mimi binafsi nafurahi mwenyezi Mungu kunijalia uhai kushudia maajabu ya awamu ya tano awamu iliyojaa uzalendo,kupenda wananchi wake na kupigania maslahi ya Nchi
Ni bahati mbaya sana kuna baadhi ya wanasiasa na watu wasio wazalendo wanakubali kutumika na mabeberu ila hawatafanikiwa

Mimi nitawasilimua wajukuu wangu uzalendo wa Huyu msukuma toka kanda ya ziwa aliyeamua kuitengeneza ile Tanzania ya Nyerere aliyoitarajia

Ahsante magufuli ipo siku wanaokubeza watatamani urudi Ikulu hata saa moja tu urekebishe Mambo
Kwani ni ngumu kupata Rais mwaminifu na mchapa kazi kama wewe
 
Kuna kundi jingine kubwa sasa hivi linazaa hovyo huko bila kuwa na malengo halafu mwisho wa siku nao wanaishia kumlaumu JPM..

Awamu hii hakuna cha dezo, bila kufanya kazi halali hakuna hela tena naomba aongezewe miaka 5 ikamilike 15 na imani tutapata kizazi cha wachapakazi, achana na hiki kilichokuwa kimezoea dezo muda wote katika awamu zilizopita..
 
Kuchapa kazi Hakuna asiyependa kama mazingira Mazuri yakiwekwa ili MTU aweze kufanya kazi.Kaa nafasi ya wasio na ajira mtaani baada ya Sera za Kusomesha watu no
 
Kuna kundi jingine kubwa sasa hivi linazaa hovyo huko bila kuwa na malengo halafu mwisho wa siku nao wanaishia kumlaumu JPM..

Awamu hii hakuna cha dezo, bila kufanya kazi halali hakuna hela tena naomba aongezewe miaka 5 ikamilike 15 na imani tutapata kizazi cha wachapakazi, achana na hiki kilichokuwa kimezoea dezo muda wote katika awamu zilizopita..
Kachukue buku 7 chumba no 7 kwa chakubanga
 
Ukipita mitandaoni utaona baadhi ya vijana wanavyolalamika bila Sababu

Wanamlaumu Rais magufuli kwamba maisha magumu
Ati zile maisha magumu zimeripotiwa na Rais wetu mpendwa

Tuliobahatika kuishi awamu zote tano Tunajua Mambo yalivyo na yalivyokuwa

Sisi wengine tumejifunza somo la uvumilivu tulivumilia hali ngumu kipindi cha Nyerere kutokana na Nchi yetu chini ya Nyerere kuwapinga mabeberu kwa vitendo

Mabeberu walifanya kila hila kimkwamisha Nyerere ila Kwasababu tulijua Nyerere anachopigania tulimvumilia hatukutaka tuwe wasaliti Ndani ya nchi yetu na Alifanya kazi kubwa

Baada ya hapo walipita ma Rais watatu kabla ya magufuli na walifanya kadri ya wawezavyo kuijenga Tanzania ila alipokuja magufuli tulipiga magoti kumshukuru Mungu tulijua magufuli ni nani na anataka nini
Nilikuwapo pale uhuru wakati magufuli akiapishwa sio siri nilitokwa na machozi nilimwona pia kadinali pengo akiifuta mawani yake bila shaka alitokwa na machozi

Siku ile mvua ilinyesha sana sikumbuki maneno mengi ya magufuli ila nakumbuka mstari mmoja tu alisema NiTAANZA KAZI LEO LEO Hii sentensi iliniamsha Ari ya uzalendo ule niliouamini kutoka kwa Baba wa Taifa mwl.Nyerere

Moja ya ziara za kwanza kabisa ya magufuli ilikuwa ni pale BOT baada ya ziara alisema banki kuu ni kama haina fedha maana yake zilitembea na wahuni kutokana na upole wa kikwete

Tuliomwamini magufuli tuliendelea kumwombea tulijua nguvu ya mafisadi katika Nchi Hizi maskini ni kubwa sana tulijua mafisadi watutumia kila mbinu kumkwamisha ni kweli wengine walihamisha pesa zao wengine walifunga biashara wengine walifanya kila aina ya ufedhuli kuhakikisha magufuli anakwama

Lakini miaka minne baadae Mzee yupo imara zaidi maadui zake wapo hoi wengine waliamua kuonyesha hasira zao hadharani kwa kumhujumu

Mimi binafsi nafurahi mwenyezi Mungu kunijalia uhai kushudia maajabu ya awamu ya tano awamu iliyojaa uzalendo,kupenda wananchi wake na kupigania maslahi ya Nchi
Ni bahati mbaya sana kuna baadhi ya wanasiasa na watu wasio wazalendo wanakubali kutumika na mabeberu ila hawatafanikiwa

Mimi nitawasilimua wajukuu wangu uzalendo wa Huyu msukuma toka kanda ya ziwa aliyeamua kuitengeneza ile Tanzania ya Nyerere aliyoitarajia

Ahsante magufuli ipo siku wanaokubeza watatamani urudi Ikulu hata saa moja tu urekebishe Mambo
Kwani ni ngumu kupata Rais mwaminifu na mchapa kazi kama wewe
Moja ya bandiko la hovyo kabisa kuwahi kukumbana nalo ndani ya JF tangu nizaliwe.

Hebu jipige pige kifuani huku kwa sauti ya chini kabisa ukijiita popoma!
 
Back
Top Bottom