Unataka mikopo na kodi zetu ziwe zinatumika kuongeza watu mishahara tu sio!!
Hizo Marco ni uwekezaji wa muda mrefu ambao Nchi yeyote inayotaka kupiga hatua kimaendeleo lazima iwekeze huko
Huwezi kupiga hatua kiviwanda wakati hauna umeme wa kutosha never
Huwezi kupiga hatua kama hauna reli ya kisasa angalau standard gauge
Tuwe wavumilivu mkuu matokeo yataonekana
Hakuna maendeleo yeyeto yanayowezapatikana Kwa Kusomesha watu no ( kuuwa secta binafsi).Huwa wanaanza na kuwainua watu kwanza Kwa kuwatengenezea mazingira ya wao kukua mfano kufuta au kupunguza kodi direct tax,kujenga mireji ya umwagiliaji kila sehemu, kujenga vyuo vya maendeleo, ujasiliamali ufundi chini ya veta kila kata na kuwakopesha watu elimu,kuwapa ruzuku za vifaa vya Kilimo na kufungua mipaka, kuruhusu hela kwenye mzunguko ili watu waweze kuuza na kununua. Hii uongeza idadi ya walipa kodi na kuchochea uzalishaji wakiongeza uzalishaji utapata kodi nyingi sana ukipata kodi za kutosha ndo unafanya macro economy project bila kuathiri watu wako.Ya macro economic ni kuhofia ya Ethiopia yasijitokeze pale miradi imekwisha na hainufaishi wote zaidi ya kufurahisha macho ya waliyoianzisha huku vijana wao wakifa kwenye malori ugenini.huku mapato yote utumika kulipia madeni ya mikopo nje,ambapo hadi wakimaliza kulipa mikopo miradi imeshachakaa inataka ukarabati.