Zipo Wapi Zile Taasisi za Kutetea Haki za Binadamu Tanzania? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zipo Wapi Zile Taasisi za Kutetea Haki za Binadamu Tanzania?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by anney, Sep 3, 2012.

 1. a

  anney Senior Member

  #1
  Sep 3, 2012
  Joined: Jul 9, 2010
  Messages: 156
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tanzania leo hii imerudi zile zama za kikoloni au zile na kumwogopa balozi wa nyumba kumi ambapo serikali inaweza kufanya chochote bila kuhojiwa na umma. Polisi anaweza kukupiga risasi bila kuhojiwa na mamlaka za utawala. Malalamiko ya umma yanaishia kwenye vyombo vya habari, mitaani na kwenye mifumo ya kijamii kama Facebook, JF nk. Watanzania leo tujifaraji ya kuwa demokrasia yetu inakua na kusonga mbele. hivi ni aina gani ya demkrasia inayakua huki ikienda kinyume na haki za binadamu. Mimi binafsi naona ukuaji huu wa demokrasia hauendani na ukuaji wa 'haki za binadamu'. Napenda kulitolia mifano ni jinsi gani leo hii binadamu anaonekana ni sawa na sismizi wanaokanyagwa na magari barabarani.
  1.Kila wakati tunasikia Polisi wameua majambazi watano, watatu, wawili nk. lakini hakuna uchunguzi unaofanywa kujua kweli waliouawa ni majambazi.
  2. Mauaji kwenye maeneo yenye migodi ya madini, hakuna uchunguzi unaofanywa kuangalia kwanini watu wameuawa au mtu ameuwa?
  3. Mauaji kwenye mikutano ya vyama vya upinzani. Hakuna tume huru iliyowahi kuundwa kufahamu ukweli.
  4. Sasa mauaji yamewafikia waandisha wa habari naamini hakuna hatua itakayochukuliwa kujua ukweli. Waandishe watu wataandika makala baada ya wiki mbili kimya wameshasahau.

  Sasa najiuliza zile presure groups mfano, Tamwa, tume haki za binabamu, University student organizations, Politcal parties, trade unions, UDASA, SUASA, Tanzania Law sociaety, NGO nk zinafanya nini kuwasaidia watanzania ambao haki zao zinakanyagwa kama sisimizi na kuawa kila siku? Kwa nini siku moja watanzania tusisema inatosha hatuendi kazini kwa siku mboli, twendeni barabarani mpaka haya mauaji haya yachunguzwe.
  Mimi Namsikitikia sana Rais kwa sababu yeye ameapa kulinda katiba, na katiba inalinda haki za watu wetu, lakini kwa nini hachunguzi haya mauaji na kupata ukweli?

  Tukiendela hivi bila kuchukua hatua yatatokea mauaji makubwa kiasi kwamba tutajilani kwa uhawani wetu huu wa vyombo vya dola.

  Napenda kuwapa taarifa CHADEMA KUWA HAYA MAUAJI KWENYE MIKUTANO YENU NI MBINU ILIYOPANGWA ILI CHADEMA IONEKANE CHAMA CHA VURUGU ILI MSIWEZE KUAMINIWA UKANDA WA PWANI, MOROGORO, IRINGA, DODOMA, SINGIDA NA TANGA. Mfumo dola umeshafanya utafiti ukaona kuwa mlifanikiwa lindi na mtwara, hivyo lazima wahakikishe kuwa haya maeneo mapya msifikie malengo. TUNAOMBA MTUMIE BUSARA KUPAMBANI NA CHIZI!
   
Loading...