Zipo wapi helkopta za CCM na CUF Igunga?

TUMBIRI

JF-Expert Member
May 7, 2011
1,933
1,199
Wakati uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga unakaribia vyama vya CUF na CCM vilitutangazia kwamba vitatumia helkopta kwenye uchaguzi huo. Na hii ndiyo ingekuwa kwa mara ya kwanza kwa CUF kutumia helkopta katika chaguzi na mara ya pili kwa CCM kutumia katika chaguzi ndogo baada ya ule wa Tarime. Hadi leo ambapo tumebakiwa na takribani siku tano hakuna chama hata kimoja kati ya hivyo ambavyo vimeingiza helkopta jimboni humo.

Watu wenye akili timamu wanasema kwamba ni kwa sababu CDM bado hawajaanza kuitumia. Kwa hiyo somo tunalolipata hapa ni kwamba CDM ndicho chama kinachoongoza vyama vingine vifanye nini na nini visifanye.

Mtakumbuka wakati wa Uchaguzi mdogo Jimbo la Tarime, CDM ilipoongiza helkopta dakika za mwisho wa kampeni, CCM nao wakaingiza helkopta mbili zilizofadhiliwa na Rostam.
 
CUF wana jeuri wataitoa wapi? ikiwa bajeti yao ni mil 75, ndo maana waliingiza pikipiki.
 
CCM hawawezi kufanya hivyo kwasababu wanajali rasilimali za nchi
wanazingatia matumizi bora ya rasilimali za nchi..
CDM kwenye kampeni hizi wameishiwa... budget yao wameimalizia kwenye maandamano na posho za viongozi wa ngazi za juu
 
Hehe eheh ehehe ehee! hahaha ahahaha ahah!!!!!
 
Leo ndio vyama vya siasa vinaanza kampeni na Helkopta.
Vyama vitatu CUF, CDM, CCM, vyote vitatumia Helkopta
 
CCM hawawezi kufanya hivyo kwasababu wanajali rasilimali za nchi
wanazingatia matumizi bora ya rasilimali za nchi..
CDM kwenye kampeni hizi wameishiwa... budget yao wameimalizia kwenye maandamano na posho za viongozi wa ngazi za juu

Umesema ukweli tumeona jinsi CCM inavyojali rasilimali kwenye Umeme wa Richmond $ mil. 161 zilipotea na hakuna umeme uliozalishwa
na pia tuliona jinsi CCM inavyojali rasilimali za nchi pale waliponunua radar ya sterling pound mil.10 na badala yake wakalipa pound milion 28.

kwa kuonyesha kabisa kuwa wanazingatia matumizi ya rasilimali za nchi walinununua dawa za bilioni 5 na kuziacha kwenye bohari ya madawa hadi zina expire wakati wananchi wanakufa mahospitalini kwa ukosefu.

Nice Try rejao.
 
CCM hawawezi kufanya hivyo kwasababu wanajali rasilimali za nchi
wanazingatia matumizi bora ya rasilimali za nchi..
CDM kwenye kampeni hizi wameishiwa... budget yao wameimalizia kwenye maandamano na posho za viongozi wa ngazi za juu

contain malware signature
 
Wafanyabiashara safari hii wamegomea michango kudhamini siasa uchwara Igunga.
wewe unaonaje matukio wanayofanya CHADEMA, si watatungua hellkopta za wastaarabu? kama wamechoma nyumba, kumwagia watu tindikali, kununua kadi za wapiga kura na kuwazuia wanawake wasipige kura watashindwa kutungua helkopta? au ww ndo ulipangwa klwenye operation hiyo?
S-LAA, FREEMANSONY bwana noma.
 
CUF jumatano tarehe 28.09.2011. kuanzia saa 2.00 tazameni macho juu mtaiona ikielekea igunga.
 
CCM hawawezi kufanya hivyo kwasababu wanajali rasilimali za nchi
wanazingatia matumizi bora ya rasilimali za nchi..
CDM kwenye kampeni hizi wameishiwa... budget yao wameimalizia kwenye maandamano na posho za viongozi wa ngazi za juu

ccm ipi mkuu?
 
Back
Top Bottom