Zipo taarifa za kutisha wilayani Lushoto za ukosefu wa amani, wizi na mauaji. Serikali mna taarifa?

Chemtrail

JF-Expert Member
Aug 15, 2016
827
442
Nimepokea kwa masikitiko kutoka kwa ndugu zangu walioko Wilayani Lushoto kwamba hali ya usalama Wilayani humo, hasa Lushoto ya Kaskazini ni tete sana. Wote tutakumbuka matukio ya Tanga kule Amboni na Magamba. Inaelekea huu ni muendelezo wa matukio yale.

Taarifa nilizonazo kutoka Lushoto ni kwamba yapo mauaji ya watu wapatao kumi na sita yaliyofanywa maeneo ya Shume kwenye kijiji cha Gologolo baada ya miili ya watu hao kukatwa viungo na hatimaye kutelekezwa. Zipo pia taarifa za isolated incidences za wauaji hao kukata viungo vya miili ya wananchi maeneo mbalimbali na hatimaye kuitelekeza miili hiyo msituni.

Watu hao wanaoaminika kuwa makao yao makuu yapo maeneo ya Kata ya Rangwi. Wilayani humo katika "msikiti fulani mpya" pia wanahusika na wizi kwenye majumba ya watu ya vitu mbalimbali. Tunadhani hii ni katika haarakati za kupata fedha kwa ajili ya kuendeleza harakati zao hizo. Mama yangu mzazi ambaye ni mzee amekubwa na zahma ya kuvunjiwa nyumba na kuibiwa!

Tunaomba serikali na jeshi la polisi wafanye uchunguzi. Kwa vile maeneo yanayokumbwa na balaa hili yapo Kaskazini mwa Wilaya ya Lushoto na mpakani na nchi ya Kenya, tunaoiomba serikali na Jeshi la Polisi wawe makini katika uchunguzi wao kwa vile inawezekana matukio haya ni maandalizi ya harakati pana zaidi za ugaidi.

Duuuh , poleni sana watu wa tanga ..lkn serikal iko makini sana kuzuia wapinzani kufanya siasa ili serikali ije huko tanga , waambie chadema wanafanya mikutano njoni muwazuie labda mnaweza pata msaada kwa njia hiyo.
 
Msikiti c ni Nyumba ya Ibada jamanii, cjui km kuna dini inahubiri MTU kuua MTU mngine. Na km IPO basi itafika tuu cku TUTAJUA MUNGU WA KWELI NI YUPI.

Poleni sana watu wa Lushoto kwa hili janga. Kuna watu wanatumia misikiti ili kuficha maovu yao.

Wanajifanya ni waumini wazuri na wanalala misikitini kumbe ni wahalifu wakubwa.

Mwanzoni misikiti imekuwa ikihifadhi waumini hasa wasafiri waliokosa sehemu za kujistiri.

Hii imekuwa nia njema na imewasadia watu wengi kuadhirika. Ndugu zangu waislamu hii dunia imebadilika, sio kila muarabu ni shekhe.

Hili jambo la kulala misikitini linatakiwa liangaliwe upya, kwa kuwa watu wasio waaminifu wameanza kuitumia hii fursa kwa nia ovu.
 
Nimepokea kwa masikitiko kutoka kwa ndugu zangu walioko Wilayani Lushoto kwamba hali ya usalama Wilayani humo,hasa Lushoto ya Kaskazini ni tete sana.Wote tutakumbuka matukio ya Tanga kule Amboni na Magamba.Inaelekea huu ni muendelezo wa matukio yale.

Taarifa nilizo nazo kutoka Lushoto ni kwamba yapo mauaji ya watu wapatao kumi na sita yaliyofanywa maeneo ya Shume kwenye kijiji cha Gologolo baada ya miili ya watu hao kukatwa viungo na hatimaye kutelekezwa.Zipo pia isolated incidences za wauaji hao kukata viungo vya wananchi maeneo mbalimbali na hatimaye kuitelekeza msituni.

Watu hao wanaoaminika kuwa makao yao makuu yapo maeneo ya Kata ya Rangwi
Wilayani humo katika "msikiti fulani mpya" pia wanahusika na wizi kwenye majumba ya watu wa vitu mbalimbali.Tunadhani hii ni katika haarakati za kupata fedha kwa ajili ya kuendeleza harakati zao hizo.Mama yangu mzazi ambaye ni mzee amekubwa na zahma hii!

Kwa vile maeneo yanayokumbwa na balaa hili yapo Kaskazini mwa Wilaya ya Lushoto na mpakani na nchi ya Kenya, tunaoiomba serikali na Jeshi la Polisi wawe makini katika uchunguzi wao kwa vile inawezekana matukio haya ni maandalizi ya harakati pana zaidi za ugaidi!

Mama yako mzazi amekatwa viungo gani mbona huvitaji? Tatizo ni huo msikiti mpya au tatizo ni nini? Propaganda zakijinga na chuki zimekuzidi, huku kuna panya road wangemkamata huyo mama yako angekojoa huku amesimama
 
Nitoe ushauri kwa serikali,huu ni wakati wa kumimina makachero wengi ndani ya misikiti na makanisa.Huenda haya makundi ya kihalifu hata ya Dar yanamkusanyia mtu mtaji wa ugaidi baadae.
 
Mama yako mzazi amekatwa viungo gani mbona huvitaji? Tatizo ni huo msikiti mpya au tatizo ni nini? Propaganda zakijinga na chuki zimekuzidi, huku kuna panya road wangemkamata huyo mama yako angekojoa huku amesimama
Asante kwa kunitukana.Hata kosa langu silioni.Wewe si muungwana hata kidogo.Nimekusamehe bure.Nadhani wanaohusika hata hivyo wamepata taarifa.
 
Kama hali ya chama iko vizuri , hatutahangaika .

Mama yako mzazi amekatwa viungo gani mbona huvitaji? Tatizo ni huo msikiti mpya au tatizo ni nini? Propaganda zakijinga na chuki zimekuzidi, huku kuna panya road wangemkamata huyo mama yako angekojoa huku amesimama

punguzeni mihemko... pengne ni alshabab wametamalaki eneo husika.
 
Asante kwa kunitukana.Hata kosa langu silioni.Wewe si muungwana hata kidogo.Nimekusamehe bure.Nadhani wanaohusika hata hivyo wamepata taarifa.
Duuuhhh weye uliyemtukana huyu Bwana jitokeze hadharani umuombe msamaha..huko Ushoto ni atai kwei kwei watakulaza juu ya mti...shauri yako
 
Duuuhhh weye uliyemtukana huyu Bwana jitokeze hadharani umuombe msamaha..huko Ushoto ni atai kwei kwei watakulaza juu ya mti...shauri yako
Hapana mimi sio mchawi,nimemsamehe bure kama nilivyosema.
 
Duuuhhh weye uliyemtukana huyu Bwana jitokeze hadharani umuombe msamaha..huko Ushoto ni atai kwei kwei watakulaza juu ya mti...shauri yako
Inaonekana na wewe ubongo umejaa tope. Watu wanajadili mambo ya msingi wewe unaleta mzaha.
 
Back
Top Bottom