Zipi sababu za kukufanya Ufikiri kuwa Magufuli anafaa au hafai kuendelea kuongoza taifa hili kwa ngwe ya pili 2020-2025?

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,657
30,034
Kama kawaida yet u watanzania kila baada ya miaka 5 ufanyika uchaguzi mkuu wa Urais,Ubunge na Udiwani,

Mwaka 2015 umefanyika uchaguzi uliomuacha Magufuli kileleni kwa kura 8,000,000 za waliojitokeza kupiga kura Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya uchaguzi,

Yapo mambo ambayo aliahidi na kufanya vema, lakin yapo mambo ambayo mpaka sasa kuna sintofahamu,

Kwa mengine ameyaweza

1.MIUNDOMBONU
tumeshuhudia ujenzi ukiendelea kila kona kama vile
A.Ujenzi wa Barabara
B.Ukarabati wa Vivuko
C.Ujenzi wa Mabweni na viwezeshi vya elimu nchini

2.USAFIRI
A.Ununuzi wa ndege
B.Ujenzi wa reli ya standard gauge
C.Ujenzi wa Meli ziwa Victoria
D.Upanuzi wa viwanja vya ndege

3.RUSHWA
Hapa kuna maoni tofauti kutoka kwa wadau mbali mbali kuwa ni hadaa tu ya kutulaghai hakuna suala lolote limefanyika,

4.ELIMU
Elimu bila malipo kuanzia chini mpaka sekondari

Maeneo ambayo Kafanya vibaya sana

1.RUSHWA
Bado rushwa ipo nchini hakuna uhuru wa kuhoji mapato na matumizi ndani ya baadhi ya Taasisi,
Hata zile zinazusanywa kutoka Kwa wahujumu uchumi hatujaelezwa zinaenda sehem gani na zitafanya nini

2.MAAMUZI YA JAZBA
Kuna maamuzi rais wetu anafanya mpaka unaweza kujiuliza hivi huyu kawazaje mpaka haya yanatamkwa?

3.UONEVU
KUTISHIA WAWEKEZAJI
4.UKIUKWAJI WAHAKI ZA BINADAMU
5.UMINYWAJI WA DEMOKRASIA NA UHURU WA HABARI
6.UPOTEAJI WA WATU WAKOSOAJI

Naendelea............
 
Nchi za wenzetu hazimpima kiongozi kwa kujenga vitu kama miundombinu pekee, bali humpima kwa kuheshimu utu wa watu wake,demokrasia,uhuru wa watu kutoa maoni,kuheshimu katiba na sheria za nchi husika na kigezo kingine kikubwa kikiwa ni peformance ya kiongozi katika maswala kama uchumi,na ajira,

Ni kweli pia ukishindwa kuboresha miundombinu huku unakusanya kodi, watakupiga chini,ila hata ukijenga miundombinu na ukafeli katika hayo maeneo niliyotaja,bado tu watakupiga chini.
 
Kuna sababu moja kuu.Magufuli anathamini vitu kuliko watu.Magufuli anathamini watu wake anaowataka(mbaguzi)Lakin ana chuki kwa wenzake wasiomsapoti hivyo hafai kuwa kiongozi.Pili suala la ajira ni ni tatizo sugu zaidi,Yeyote aliyesoma na hana ajira basi akimpa kura magufuli basi kidogo kichwani zitakuwa hamnazo kwa sababu serikali ya kikwete iliajiri hadi watu hewa na kuwalipa mishahara lakin huyu mbweha hata kuajiri robo hakuna.

Vipo vingi ukianza kutaja vizuri ni vichache kuliko vibaya.
 
Jiwe Hafai kwa sababu zifuatazo:

1. Ni katili (uvunjaji wa nyumba za watu, kumuonea na kuendelea kumnyanyasa Lissu)

2.Haheshimu katiba (anachagua portion za kuheshimu zile zinazompendeza yeye, zile zisizompendeza basi anazikanyagakanyaga

3.Hana vision njema ya kiuchumi(Miradi yake ya ndege ni white elephant)

4.Anaua taasisi za checks and balance (Anakanyaga bunge na mahakama)

5. Hatendi haki

6. Haheshimu uhuru wa watu na faragha zao(Kudukua watu na kutamka wazi kuwa anawadukua)

7. Haheshimu Ilani ya chama (Kuna vitu vilivyomo kwenye ilani ya chama lakini kavipiga chini kuwa eti hakuviahidi mfano ni katiba mpya)

8. Yuko biased, hayuko consistent (Kafukuza watumishi vyeti feki lakini wale aliowateua yeye mwenyewe hakuendesha zoezi hilo dhidi yao hata kama pengine baadhi yao wana vyeti feki)

9.Maamuzi yake ya papo kwa papo hayana faida kwa Taifa (mfano kuhamia Dodoma, Kutwaa kinguvu korosho za walulima na kuwasababishia adha kubwa ya kutolipwa kwamwaka mzima)

10. Ni one man show (anataka atolee mwongozo wa kiutendaki kwa vitu ambavyo vimo hata katika mamlaka ya wakuu wa wilaya etc)

11. Akishaharibu sehemu ni bingwa wa kuhamishia lawama kwa watendaji wengine, na wengine kuwakemea kemea mbele ya kadamnasi ili ajisafishe yeye kwa makosa yake mwenyewe (mfano kugukuza watu kwa ishu za korosho wakati yeye ndo aliharibu toka mwanzo)

Kiufupi Jiwe Hafai kuwa hata katibu kata

Twende na Membe 2020, huyu amepikwa kiuongozi akapikika kwelikweli, ana exposure kubwa
 
Magufuli he is the best President ever...Ukweli lazima tuuseme Kwa sasa hakuna mbadala wa Magufuli Kwa miaka mingine mitano....huyu mzee kalitendea mema sana Taifa letu.....Yeye si Malaika akakosa Mapungufu lakini mpaka sasa ana Mazuri mengi mno kwa Nchi yetu kulinganisha na mabaya tunayoaminishwa na baadhi ya watu ambao nao ni wachafu kupindukia
Leo too watu wanaona Membe ni mbadala wa Magufuli Kwa lipi Jema alilolifanya kwa Nchi hii wakati akiwa Waziri na Mbunge????
Halafu Watanzania tunatakiwa kujihadhali mno na hawa wanaopingana na Rais wetu Kwa sasa hawa si wao bali wanatumiwa na baadhi ya wabaya wetu walioguswa maslahi yao ya kifisadi waliokuwa wanafaidika nayo awamu zilizo pita....
Mfano hivi Kia akili ndogo mnafikiri Tundu Lissu huko Kwa hao Wazungu wanashindwa Nini kumfadhili kipesa au kumhakikishia njia yoyote Ile ashinde Urais na yeye kuwalipa ahsante Kwa kuwauzia Rasilimali zetu.....(Na ndio màana Leo too Membe,Zitto na Lissu ni marafiki Kwa kuunganishwa na majizi ya baadae ya Nchi yetu)
Magufuli angekuwa Hapendwi kama tunavyoaminisha ma Magenge ya ajabu humu mitandaoni mbona watu tungekuwa Tumeishaingia barabarani......Ukimya wa Watanzania ni Kwa sababu tunaona kweli anaitendea Nchi yetu mambo mazuri mno
 
Kwahiyo aendelee kuongoza
Kiongozi hupimwa kwa mizania ya mazuri vs mabaya afanyayo kwa wananchi wake.
Kusema ukweli kabisa, Rais Magufuli ana mazuri mengi kuliko mabaya.

Kama binadamu anapaswa kuendelea kuishi kwa misingi ya utu na heshima kwa watu anaowaongoza.

Ni kiongozi sahihi kwa kipindi hiki tulichonacho ambapo mambo ya Serikali na Nchi yalikuwa yanaenda ili mradi siku zinaenda.

Amefanya kwa uwezo wake, Mwenyezi Mungu aendelee kumwongoza ili awaheshimu wananchi wote bila kuwabagua na aheshimu utu wao ikiwemo haki ya kuikosoa Serikali inapokengeuka.

Hata Nyerere alikuwa na madhaifu, lakini mizania ya mazuri ilikuwa juu ndio maana kiujumula bado anahesabika kuwa alikuwa mzuri.
 
Hafai, hafai, na sababu kuu ni moja tu. Kwakuwa yupo sisiem.

Shida zote za nchi chanzo ni fisiem.

Ndio maana Leo JPM anapata tabu sana linapokuja suala la uchaguzi na upigaji wa kura. Yaani uwanja ukiwa huru JPM na chama chake hawachomoki, yaani JPM ana mambo take mazuri lkn gari analotumia limechakaa, lkn angekuwa upimzani naamini kwenye chaguzi ingekuw ni kama kumsukuma mlevi.
 
Back
Top Bottom