Zi'nlala

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,607
1,840
Wapemba wawili walikuwa wanatembea barabarani kule Mtwara, kwa ghafla mmoja akagongwa na gari akafa, hapo hapo. Polisi walipo fika eneo la ajali wakamuuliza yule mpemba mwingine kama ifuatavyo:

POLISI: Unaikumbuka namba ya gari lililomgonga marehemu?

MPEMBA: Ami n'zikumbuka mieee, gari enyewe ni kuukuu hivi inkisha namba zake ni saba mbili zinlala na saba mbili zinsimama.

Polisi wakawa wamepigwa na mshangao wasimuelewe, kumbe masikini mpemba wa watu alikuwa anamaanisha LL77 namba za Malawi


*** *** ***​

Mpemba mmoja alikuwa akivusha watu kwa kutumia mtumbwi pale kivuko cha kigamboni, mbaya zaidi mtumbwi wake ulikuwa umejaza abiria kiasi ambacho hata pa kukanyaka hakuna. Sasa kwa bahati mbaya walipokuwa katikati ya maji wakati wa kupiga makasia upodo ukamteleza ukazama abiria wakawa wanapiga makelele sana.
kuna ambao walikuwa wanalia "mama weee...! wengine bandu mweeee...! wengine Mtumee... wengine Yesu wanguuu... basi kila mtu na kilio chake... Sasa yule mpemba kwa hasira na kwa mshangao akawajibu...

"Pana cha Yesu na Ntume... hapa!! Na upodo unzamaa!!? kama wankuja wote wataket wapiii....?!!
 
Back
Top Bottom