Zingatia yafuatayo ili uweze kufanikisha maisha kupitia siasa

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
Mada tajwa hapo juu yahusika.

Wengi wetu tumekuwa tukitamani sana kuwa na maisha mazuri kupitia siasa huku ukizingatia kwamba ukiwa mwanasiasa bora halafu ukapata 'zali' ,unakuwa na maisha mazuri within no more time.Kwa kifupi tu,siasa ndo kazi pekee yenye maslahi marefu ndani ya muda mfupi.Siasa haiangalii elimu, siasa ni game kama mchezo wa karata.

Kuna watu wamekuwa mpaka wanaenda kwa waganga wa kienyeji kuchanja chale sehemu wanazozijua wao,ilimradi tu wayashinde maisha kupitia siasa. Leo nawaletea nyenzo(tips) muhimu za kuwa mwanasiasa mzuri na bora:-

1. Jiunge na chama cha siasa chenye mwelekeo chanya (mfano CCM);

2. Shiriki vyema kwenye hafla, mikutano, makongamano, matamasha ya kisiasa huku ukiwa upande wako (mfano CCM);

3. Shiriki vyema kwenye chaguzi zote kuanzia mtaa mpk taifa ndani ya chama chako (CCM);

4. Tangaza nia kwenye nafasi za uongozi huku ukianzia chini kabisa;

5. Shiriki hafla mbalimbali za kitaifa zinazohudhuriwa na viongozi wakuu wa Serikali na chama mfano sherehe za Uhuru, Muungano, CCM, Mei Mosi, Wafanyakazi, Nanenane, Wakulima nk. Huku ukivalia mavazi ya chama chako (cha CCM);

6. Kuwa na confidence ya kusimama majukwaani mbele za watu na viongozi. Usiogope kuchekwa;

7. Kuwa karibu (jenga fitina) na viongozi wakuu wa chama na Serikali ;

8. Jitahidi kunyenyekea wakubwa , kuwatembelea majumbani mwao, maofisini mwao mara kwa mara huku ukiwa umevalia vazi la chama chako (cha CCM);

9. Neno 'mheshimiwa' ni la muhimu sana unapokutana n wakubwa;

10. Kula la kipofu

11. Muombe Mungu atakusaidia


Mungu ibariki Tanzania
 
Hii inawafaa kina Barbarosa, muda wote, faizafoxy, jingalao, stroke, Lizabon na takataka zingine Kama hizo
 
Hivi kati ya Tundu Lissu(CHADEMA) na Fred Mpendazoe(CCM) nani aliyefanikiwa kisiasa?
 
Ujinga na ushetan tuu huo, bora kufa ukiwa umesimama kuliko kuishi umepiga magoti
 
Hii ime work sana kwa bashite yani sahvi anajilia vyake kiroho safi..ila nakumbuka JMK aliwahi kusema usipo kubali kuliwa huli..nadhani hii ni njia mbadala ya kufanikisha malego..bravo bashite..
 
Back
Top Bottom