#COVID19 Zingatia usafi wa barakoa wakati wa kujikunga na Covid-19

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
Uvaaji wa barakoa ni miongoni mwa tahadhari muhimu inayosisitizwa katika kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi vya Corona.

Wataalamu wa Afya wanahimiza usafi wa mara kwa mara katika barakoa inayotumika kujikinga dhidi ya maambukizi ya Corona.

Inaeleza kuwa barakoa huweza kuchafuka kutokana na kutumika kwa muda fulani, kudondoka au kwa kupiga chafya na kukohoa.

Hivyo, ikitokea barakoa imechafuka kwa namna yoyote unashauriwa kuibadilisha na kuvaa nyingine ambayo ni safi sambamba na kusafisha vyema mikono yako.

Aidha, inaelezwa kuwa kwa barakoa ambazo zimetengenezwa kwa ajili ya kutumika mara moja zitupwe baada ya kutumika au kuchafuka wakati zile ambazo zinaweza kutumika zaidi ya mara moja zisafishwe na maji ya moto zinapochafuka.
===

Put on a new, clean mask as soon as possible and wash your hands
If you are wearing a mask: You can cough or sneeze into your mask. Put on a new, clean mask as soon as possible and wash your hands.

Always cover your mouth and nose with a tissue when you cough or sneeze, or use the inside of your elbow and do not spit.
Throw used tissues in the trash.

Immediately wash your hands with soap and water for at least 20 seconds. If soap and water are not readily available, clean your hands with a hand sanitizer that contains at least 60% alcohol.

How to clean mask
Reusable masks should be washed whenever it gets dirty or at least daily. If you have a disposable face mask, throw it away after wearing it once. Always and wash your hands after handling or touching a used mask.

CDC
 
Je, uvaaji wa barakoa si kwamba unaunyima mwili fursa ya kutengeneza kinga yake ya asili, kiasi siku ukiacha kuvaa unakuwa hatarini kupata hata maambukizi mengine ya kawaida?
 
JamiiTalk ni ID kubwa sana hapa. Makosa madogo kwenye heading yana'washawasha' wasomaji. i.e. kujikunga!
===
Kuhusu barakoa mbali na mambo mengine mazuri uliyoeleza. Kwa uzoefu wangu wa kuitumia nashauri watumiaji wa zana hii kuwa wasidhubutu kupanda jengo refu ama mlima mkali kwa mguu wakiwa wamezivaa zana hizi. Watazirahi/zirai. Mimi nilikoswakoswa kuzirai.
 
Back
Top Bottom