Zingatia mchoro huu wa njia ya daraja la Kigamboni usipotee

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,545
22,050
Habari zenu humu;

Kutokana na watu kuendelea kupotea, nimeona nishiriki nanyi kuweka mchoro huu wa njia endapo ukahitaji kufika kigamboni kupitia daraja hili jipya la Mwl. Nyerere.

NJIA ZA DARAJA LA KIGAMBONI0011.jpg


Pia serikali kupitia mamlaka husika washughulikie changamoto zifuatazo ili kuepusha ajali zinazoweza kujitokeza;

CHANGAMOTO:

- Utumiapo daraja hili kuna changamoto zifuatazo zishughulikiwe.

a. Ni vyema kwenda taratibu hususani unapokaribia kuingia (yaani sehemu inayounganisha U-turn ya kurudi Kigamboni na ile itokayo Uhasibu/TAZARA (ufikapo sehemu hiyo kuwa makini sana vinginevyo utageuka kafara). Nashauri sehemu hii serikali iweke taa maalum za kuongozea au tuta kwa watokao Kigamboni kwenda bandari na wanao u-turn wasimame ili wasigongane na watokao Uhasibu/TAZARA na kuingia moja kwa moja darajani.

b. Unapotokea Kigamboni pindi unavuka daraja la reli na kugundua umekosea njia ukabana kushoto, yaani kama lengo lako ni kwenda Uhasibu/TAZARA , ya kupasa uka U-turn urudi tena kigamboni ukaanze upya, ili ukae katikati kulia na si kushoto.

Note; Kuhama ghafla toka kushoto kwenda kulia ufikapo eneo hili kunaweza kusababisha bonge la ajali kwa kugongwa au kumwingilia aliye kwenye channel yake.

c. Pindi unapovuka kwenda Kigamboni VIJIBWENI CENTER Hakuna barabara inayowapeleka vijibweni center, wanalazimika kwenda moja kwa moja hadi mwisho wa lami na ku u-turn kurudi ili kuelekea vijibweni center.

NASHAURI, barabara moja kulia (KARIBU NA TRANSFOMA YA UMEME) baada ya tuta unapotoka kwenye check point, waweke taa itobolewe kulia kuingia vijibweni center ambayo kwani ni barabara mhimu sana kwasababu huko mbele inaenda hadi Kibada, baada ya kupita yard ya mama ANNA MKAPA inaenda kuungana na barabara nyingine itokayo kisiwani HOSPITALI YA JIJI/makaburini kwenda hadi Kibada kupitia shule ya Mizimbini secondary

d. Kwa watembea kwa miguu daraja ni lefu takribani mita 600, kwa mida ya usiku si salama kutokana na wakabaji wanaoweza kutumia pikipiki kukukaba na kukimbia, nashauri serikali waweke walinzi dolia, kila mita 100, kila upande, achilia mbali kituo cha police kilichopo, hii itasaidia kuimalisha ulinzi wa raia na miundombinu iliyopo.

e. Wenye magari, si vyema kupaki pembezoni mwa daraja na kuwasha hazard ili upige picha, hili linaweza kusababisha ajali kwa watumiaji wengine, ni vyema kwenda mpaka upande wa kigamboni kwani kuna sehemu nzuri na salama kwa parking.

....EPUKA KUWA KAFARA WA DARAJA LA KIGAMBONI, ENDESHA KWA USALAMA….

Unaweza uka share ujumbe huu ili kutoa elimu kwa wadau wengine ili kutoa maelekezo sahihi, Kupeana elimu ni wajibu wetu sote.

Imeandaliwa na mpenda maendeleo Dmkali.

KWA MAELEZO YA KINA ZAIDI JUU MATUMIZI SAHIHI, BOFYA LINK HII; Zijue hatari na changamoto za daraja la Kigamboni kabla hujalitumia
 
Safi mkuu, hako ka interchange ulikochora hapo ni mfano wa vingi vinavyotakiwa kuwepo kupunguza foleni hata maeneo mengi, sio lazima kuwa na complicated structures, na sidhan kama hiyo ni gharama sana, kwa vile Magu ana rungu saiv hebu aangalie namna ya kuweka interchange kama hizo simple tu unapandisha tuta nadhani wataalamu wa hayo mambo mnajua.
 
Ahsante mdau kwa juhudi zako binafsi za kutuletea huo mchoro. Hivi TANROADS wameshindwa kabisa kuona umuhimu wa kuandaa mchoro wa kitaalamu zaidi na kuusambaza kwa njia kama hizi za mtandao n.k.ili kuelewesha watumiaji wa hilo daraja?
 
Pongezi ndugu kwa kujitolea kuwatahadharisha watumiaji wa daraja la kigamboni.Ni kazi kubwa inayotakiwa kufanywa na kikosi cha polisi cha usalama barabarani.
 
Ahsante mdau kwa juhudi zako binafsi za kutuletea huo mchoro. Hivi TANROADS wameshindwa kabisa kuona umuhimu wa kuandaa mchoro wa kitaalamu zaidi na kuusambaza kwa njia kama hizi za mtandao n.k.ili kuelewesha watumiaji wa hilo daraja?
si unajuwa mambo ya serikali yetu, Labda kuna gharama kubwa kuuandaa mchoro, yamkini inatakiwa milion 100 zinaandaliwa ili uchorwe
 
Wataalamu wa Tanroads wangekuja na proposals za simple interchange kama hizi kwenye maeneo ya makutano yenye jams nyingi na makadirio ya gharama zake ambazo najua sio nyingi, kwa kweli ningekuwa namba moja kupledge tuchangie fedha nje ya kodi tunayolipa. Nchi kama Botswana, Swaziland structure kama hizo ziko nyingi sana. Ni wakati sasa wakina Mfugale waache kuvaa masuti waje na proposal rahisi jinsi ya kuacha bara bara kuu kuingia bara bara za mitaani.
 
Back
Top Bottom