Zingatia mambo haya unapokuwa kwenye intaneti

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Apr 28, 2020
445
754
zingatia haya unapokuwa kuwa kwenye intaneti

Ni kweli kwamba mitandao ya simu kwenye intaneti ni ulimwengu mpya ambao una kila kitu endapo unajua mahali pa kuangalia na kutumia vizuri.

lakini sio kila kilichopo kwenye intaneti lazima ukifungue au ukitumie ni muhimu baadhi ya vitu uachane nayo kabisa unapokuwa unataka kutumia intaneti kwenye simu au kompyuta yako.

Mambo hayo ni muhimu Sana kuwa nayo mbali Kama unataka kuwa salama mitandaoni

Usitumie Password ya aina moja
Password ni sehemu ya moja wapo kwani huduma nyingi zinazotolewa mitandaoni zinatolewa baada ya mtu au watu kujisajili kupitia simu yako. hivyo ni muhimu kuzingatia Usitumie password ya aina moja unapotaka kujiunga mahal fulan kwa ajili ya huduma fulani.

epuka sana kutumia majina yako, tarehe ya kuzaliwa , au abcd1234, 123456 kwani ni rahisi mtu kukuingilia kwenye kifaa chako. kama una kichwa kigumu cha kuhifadh password zako basi unaweza kuhifadh kwenye kompyuta yako au hata kwenye notepad yako.

Usitumie WIFI ambayo isiyokuwa na Password
Ni kweli kuwa hakuna kitu chochote Cha bure kisicho kuwa na gharama wengi wetu hupendelea kutumia WiFi ya bure baadhi ya huduma ambayo hutolewa na mtu au watu kwa ajili ya kuongeza biashara mvuto na kupata wateja wengi.

lakini Ila ni vyema kuwa muangalifu na WiFi hizo maana WiFi nyingi za namba hizo hutumika vibaya kuchukua data za muhimu kutoka kwenye simu au kifaa chako au wakati mwingine hutumiwa kuweka virus (kirusi) ambacho kinaweza kufanya mambo ambayo usingependa yakukute.

Usiamini watu usio wajua #mitandaoni
Nakuambia Tena Usiamini watu kupitia mitandaoni hapa kwetu Tanzania nadhani kila mtu analo SoMo la usiwaamini watu usio wajua mitandaoni

lakini kutokana na utandawazi ni ngumu Sana kumjua mwema au muovu Nani maana wote Wana sura moja.

Kutokana na Hilo ni vyema Sana kuwa muangalifu hasa huku mitandaoni na Usiamini yoyote usiyemjua.

don't fall for fake post & link
watu hupenda san vitu vya bure utasikia unataka kupata Gb56 watumiae watu kumi kisha ujisajili my friends Airtel , voda , tigo halotel au mtandao wowote hule hawawezi kukupata tu vitu vya bure heti GB 56 Akuna kitu kama hicho jihadhari na post kama hizo kwenye simu yako

Usipende kununua vitu hovyo Online shop
tunajua mitandao imekua sasa lakini jihadhari sana kununua vitu online kuwa muangalifu kabla ujaagiza kitu mtandaoni utaibiwa jamani. muhimu kabla ujaagiza hakikisha unaangalia review ya hiyo kitu kama online inauzwaje.

pia watu wangap wamenunua na hata kupitia maoni ya watu sio unapenda kununua vitu hovyo online utaibiwa

Vipi umejifunza nini kwenye makala yetu hii tuachie Maoni yako sasa ? ,


Pia usisahau kutembelea pagw yetu ya Instagram kujifunza zaidi
 
Back
Top Bottom