Zingatia mambo haya ukiwa gerezani

Mkuu mimi nilifikiri ukifungwa unaondolewa uhuru wako na unatakiwa kupewa mahitaji yote ya msingi kama binadamu isipokuwa ule uhuru wako wa kuchangamana na watu wengine, je, ni sahihi wafungwa kufanya kazi wakiwa gerezani endapo hukumu zao hazikueleza kwamba wanapewa kifungo na kufanyishwa kazi, ziwe nyepesi au kazi ngumu. Mwenye uzoefu wa mataifa mengine anaweza kutupatia pia....
 
Gerezani ikifika saa 10 jion inatakiwa muwe tayari mmeshalala na ukiwa huna ramani utakula had maji ya ukoko
Asubuhi utapangwa kwenye genge la kilimo alaf majembe yote unabebeshwa wewe, mkifika mbugani kila mmoja anatakiwa achukue jembe lake kimbembe inakua kila jembe zuri ukigusa kila mtu anakwambi ni la kwake

Mwisho unabaki na jembe bovu kinoma, mnaenda kukatiwa maeneo ya kulima hapo ndo utatamani ardhi ipasuke uingie ndan maana dunia inakua siyo sehem salama tena maana una jembe bovu alaf shamba ukiliangalia huon mwsho wake na unatakiwa ulime mistari kadhaa hadi mwsho wa shamba na wala siyo ombi ni amri ukifanya mchezo utachezea fimbo nyingi sana na hakuna wa kuja kukutea utalima tu kama kufa we kufa ndugu zako watarudishiwa nguo
 
Ongeza nyama kwa wale wafungwa wanaogeuzwa wanawake hii ni kweli
Gerezan huwez kugeuzwa mwanamke labda tu wewe mwenyewe uwe shoga ukifika utoe kwa hiyari kutokana na ushoga wako au upende maisha ya kitonga kwa kujitoa utu wako ila hakuna wa kukulazimisha na ni bonge la msala askari magereza wakigundua ww pamoja na mwezako mnaokulana patachimbika hapo ndan mtailewa vizuri Nini maana ya show show
 
Niliwai kufanya kazi kwenye gereza moja uko nyanda za juu kusini kuhusu Mambo ya kilimo aisee nilijifunza mengi ikiwemo

✓ mfungwa anapo ongea na bwana jela (askali magereza) inabid achuchumae chini

✓ watu wengi wanafungwa kutokana na kiburi au jeuri ( wafungwa wote nilio fanya nao kazi nilikuwa nawahoji kwa nn upo hapa lkn baada yakunijibu nilijua bila kiburi na jeuri uyu jamaa asinge kuwepo hapa)

✓ usijaribu kuomba sigara kwa mfungwa mwenzio wakati imezimwa maana huwa wanatabia ya kuchanganya na mihadarati so ikiwa on apo unaweza kugongea lkn akikwambia subilia nikuletee kataa

✓ Bwana jela anaweza kuchagua nyampala kwa muda wowote ule na kwa sababu yoyote ile kwaiyo ukiwa na nidhamu unaweza kuwa Nyampala pia Nyampala inabidi avae mkanda kiunoni kama utambuzi

✓ wale wafungwa wanyonge walikuwa wanaitwa Wajoli

Mwisho akuna kitu kizuli kama uhuru Mkuu so ukiwa urahiani ebu tumia uhuru wako vizuri maana kule sio poa kama unaroho nyepesi ata Bwana jela uwezi kuishi maana utaona unaenda kinyume na maandiko matakatifu

Tuombeane uzima na mwisho mwema maana nafsi ya mwanadamu inahitaji maombi
 
Kama unadhani jela ni shule mpeleke mwanao, sio kuzuri hata kidogo

Hakuna kitu muhimu kwa binadamu kama uhuru, ndugu zangu tuishi na watu vizuri tuepukeni migongano na ugomvi usio na maana hasa wale wenzangu na mimi wenye hasira za karibu na kupanic fasta.. wizi, udokozi na makosa madogo madogo ya kisheria tujiepushe nayo

Mkuu habari ya siku nyingi!? Skuizi umeachia front seat kwa vijana sio!?
 
Sana mwanaume hili nimelijua toka nimefikisha miaka14 kuhangaikaaa
Nimewahi mtembelea mshkaji alipigwa miaka 5,aisee vile nilimkuta nililia sn sn.Ni mwezi tu alikuwa amekaa lakini hali niliyomkuta nayo inasikitisha.



Wanaume tumeumbwa mateso
Ee
 
Maweni naona ndio gereza gumu sana kutokana na location yake ilipo utapiga sana kokoto kwenye jua pale wafugwa wengi pale wametoka magereza ya karanga(kilimanjaro) na kisongo(arusha) hawa ni wa vifungo virefu na wale wa pale tanga kule shuruba ni nzito sana wafungwa wa kunyongwa wapo pia pale wengii tyu (condemn) maweni hata askari magereza ni wakali sana upekuzi ni kila muda na vipigo ukienda kule mwezi utapauka na kua mweusi tiii kutokana na joto,kazi,mrundikano wakuu gereza la maweni ndio gereza naloliogopa kuliko yote tanzania likifuatiwa na gereza la songwe na gereza lililopo ruvuma!
Kwa maelezo haya ni dhahiri Magufuli yupo motoni, maana pamoja na dhahama zote hizi yeye alikuwa anaona hazitoshi aliwasema Askari magereza wawatese kwelikweli wafungwa.

Sijawahi kuona Mtanzania katili kama huyo mwendakuzimu.
 
Linapokuja sawa lolote baya akili ya mwanadamu imekuwa ikilisusa bila kutegemea, ni rahisi sana kususia habari za kifo mtandaoni na kutafuta vichekesho au habari za kufurahisha, Sio bahati mbaya ila ni maumbile asili ya mwanadamu.

Lakini hoja uliyoleta mkuu ni nzuri kwa mwanadamu yeyote ambaye bado hajafikwa na umauti. Sikuwahi hata siku moja kuwaza kwamba mimi mwenyewe ipo siku ntakanyaga rumande achana na gerezani, lakini nilipelekwa rumande. Hii ilinifanya niamini kitendo cha mimi kuwa mwanaume na harakati zangu za utafutaji basi lolote linawezekana.

Binafsi nikushukru, kwa kutoa hizi "basics" ntajitahidi kuwa raia mwema, lakini wakati wa upotofu basi zitumike aidha kwangu au ndugu nitakayemshauri pia.
Chief hapa duniani kabla haujafa hauna assurance yoyote. Kitu pekee ambacho kipo certain ni kifo tu. Haya mengine yanakuja na kupita so mtu asidhani kuwa haya yaliyoandikwa hapa hayamhusu. Ni njia yetu wote.
 
Nilitumwa kikazi gereza fulani, aiseeee kumbe kule pasikie tu, jamani nyie lile limlango lione tu ila ukiingia kutoka ni ngumu.

Basi nilivyofika nikajitambulisha nimetumwa na mamlaka fulani kumuona mfungwa fulani nikaonyesha docs anazotakiwa kusaini.

Sikupata usumbufu wowote askari walinipokea vizuri.nilikalishwa sehemu baada ya muda wakamleta nikaongea nae ila mbele ya askari.

Niliongea nae akaomba hizo documents nimpelekee mtu fulani baada ya yeyekusaini na wakagonga mhuri wa magereza kuwa kapokea.

Nafasi aloipata ni kupitia hiyo document nilopeleka ataweza pata hata wakili waongee tho nafasi ya kumsaidia ilikuwa ni ndogo.

Machache niliyoyaona ndani ni kusafi sana maua kila kitu mazingira kwa nje ni safi.

Wafungwa ambao walikuwa hawajavaa sale niliona wakiwa katika vazi zao na wasafi tu.

Nilichogundua kule kuna nidhamu ya hali ya juu.kila kitu ni utaratibu.

Wakati nikiwa pale mlangoni kwa ndani maafande walinzi walinambia mtu anapoingizwa pale kwa mara ya kwanza uamini kuwa atatoka soon ila sio kweli, kuingia ni rahisi ila kutoka sio unavyodhani.

Kwa ulinzi ule inabidi kuwa mpole ukiwaza kutoroka lazima uumie. Kwanza unaanzaje kutoroka kwa fensi ile? Fensi ndefu vile kama barabara?
Nilijifunza tuishi kwa kuwa makini ukiona mtu anataka kukuletea msala jiweke pembeni.mambo ya ugonvi, kuzurumu watu na mambo mengine mabaya tuepukane nayo.
Umeongea point sana dawa ni kuwaavoid watu wanaoweza kukupeleka uko
 
Miaka mitatu iliyopita nilifahamiana na ndugu mmoja wa mwenye nyumba wangu kigamboni, jamaa alikua ana muonekano wa kihuni na kiteja. Nilikuja kufahamu kua jamaa alikaa gerezani kwa zaidi ya miaka 7 kwa kesi ya mauaji yeye pamoja na wenzake.

Jamaa alikua anatembea kama mlemavu, hyo ilitokea kipindi akiwa jela baada ya kuvunjwa mguu na askari magereza, anasema kisa cha kuvunjwa mguu ilikua ni fujo walizoanzisha gerezani. Jamaa anasema kama kuna kitu cha kuogopa sana kwa mfungwa ni fujo na utovu wa nidhamu gerezani.

Miezi mitatu kabla ya kufariki aliwahi kukutana na yule askari aliyemvunja mguu mitaa ya posta yalipokuepo makao makuu ya jeshi la magereza. Jamaa anasema alionana uso kwa uso na poti alishangaa kumuona jamaa yupo nje kwa msamaha wa Rais.
Alipomkumbusha kisa cha kumvunja mguu poti alijibu "nilikua kazini nikitimiza majukumu". Kuna msemo unasema 'ugali mtamu lakini sio wa jela.
 
Back
Top Bottom