Zingatia haya yatakusaidia katika maisha yako..

Status
Not open for further replies.

Mahmood

JF-Expert Member
Feb 9, 2008
7,909
2,477
Kitu kizuri na chenye manufaa duniani ni kuilea nafsi iwe yenye kuridhika na kushukuru, na kuwa na nia safi.

Na hakuna kitu chema chenye kuleta faida kama kuwasamehe WENZAKO wote wenye kukukosea na wenye kukuchukia!

Lakin kuna jambo jingine bora zaidi hata Mtume
(S.A.W.) aliwahi kumuusia mmoja kati ya swahaba wake zaidi ya mara 3,
na kila mara alirudia akisistiza:

"USIKASIRIKE!"
"USIKASIRIKE!"
"USIKASIRIKE!"

Kwani hasira huzaa Chuki,
Chuki huzaa maudhi,
Maudhi huzaa kisirani, na
Kisirani huondosha nuru njema maishani na
huondosha mapenzi, maelewano, utulivu, na amani.

Tuazimie kutenda mema na Mungu Atatujaalia tawfiq,

In Sha Allah
 
Hakika Mungu Mkubwa.

Jamaa haendi msikitini lakini anahoji mahubiri ya msikitini, uzuri ni kwaba ujumbe umemfikia.
 
Inaonesha humu ndani kuna watu hawajui ugaidi ni nini na chanzo chake ni nn na wapi? poleni sana mungu atupe uwezo wa kutumia akili zetu
 
Ujumbe mzuri,kwa waungwana wanaoona kuwa JF ni sehemu ya kupata mawazo mapya watajifunza vitu.
 
Haya ndio yanayo huburiwa katika nyumba za ibada.

Ndio maana Waislamu na Wakristo wanaishi pamoja na kwa usalama hapa Tanzania, mshukuru Mungu (acha fikra mbaya).

Sawa mkuu.

Tuombe Mungu sheikh Ponda na wenzake wawe na fikra kama zako.
 
kuna sababu za kumfanya mtu akasirike,naweza kusema huwa inatokea ghafla agharabu kusema hapa nakasirika au pale sikasiriki,huenda ukasema hivyo lakini ikitokea hali halisi huenda ukakasirika,kwa mfano,imetokea tu umegundua mke wako anabwana pembeni,hapa pia utasemaje,kwa asili haiji hasira automaticaly?labda cha kuongeza kwamba kukasirika hakukwepeki ila kinachotakiwa ni kutulia kwanza unapohisi umekasirika yaani usitoe maamuzi ukiwa una hasira,ila hasira haizuiliki.hata hivyo umejitahidi kutuletea kitu tofauti kidogo...
 
ukweli utabaki palepale.....!!! na moyo wa mtu ni sanduku....!!!

Ondoa fikra mbaya mkuu, kama huamini livunje hilo sanduku ili uone kilichomo ndani. Kuwa na moyo safi kwa mwenzio mtendee yaliyo mema kwani yatamfanya aone aibu hivyo kumfanya aondoe nia ovu kwako.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom