Zinedine Zidane mwarabu aliyetukumbusha mkasa wa Daudi na Goliath

Huyo mwarabu namheshimu mno kamanda, personally sijaona wa kumfikia huyo mwarabu miaka ile...final 1998 watu walipigwa kanzu, chenga nyingi mpaka walipoteana :D:D Gaucho na De lima jasho liliwatoka walitamani mpira uishe haraka, aise hawatamsahau huyu mwamba wa Algers...Mungu ambariki mno na ampe umri mrefu...

France 3-0 Brazil
 
Kwenye biblia kuna kisa cha mtoto mchunga mbuzi Daudi wa Israel, wakati huo kila mtu anamuogopa Goliath mwenye nguvu kama Hawafu, Daudi hakutumia nguvu kubwa bali akili ndogo sana kumuangusha Goliath

Ili kushinda vita ni lazima ujue muda gani upambane, muda gani ujifiche na muda gani ukimbie, bila shaka unamkumbuka Zidane kwenye ubora wake, alikua ni Goliath wa soka, lakini mtoto mdogo tu Marco Materrazi alitumia akili ndogo kumshinda

Katikati ya ubora na ufundi mkubwa na kuibeba Ufaransa mgongoni mwake, ila Zidane akaja kuwa adui mkubwa na kusemwa sana na Wafaransa, Zizzou alimuuliza Materrazi "Unahitaji jezi yangu?" ila Materrazi alimjibu "Namtaka Dada yako", hapo Zizzou aligeuka kuwa Mwarabu halisi, akala umeme fainali world cup 2006 pale German

Yupo wapi yule Daudi aliemwangusha Binadamu aliesimama kwenye ukumbi mmoja pale Basel Uswizi, 2003 akibeba tuzo ya mchezaji bora wa dunia, alikua ni General wa soka na Maestro uzawa wa Algeria, haikuwa tuzo yake ya mara ya kwanza au ya pili bali ni ya tatu

Pengine labda Daudi hakujua kuwa alimuangusha Goliath, aliefanya makubwa kwenye tuzo kabla ya ujio wa Ronaldo na Messi, labda amesahau kuwa baada ya kichwa cha Angelos Charisteas kilichowatoa France robo fainali ya Euro 2004, Zizzou alitangaza kustaafu

Lakini tangazo lake lilikataliwa na Wafaransa wote, Kocha Raymond Domenech na wanasiasa nguli kama Nicolaus Sarkozy, kila mtu alitaka arejee uwanjani, akakubali kuvaa upya viatu vyake, kuvaa upya kitambaa chake na jezi yake namba 10 ya Les Blues, kwa ajili ya kombe la dunia 2006

Alirejea wakati ambao timu ilimuhitaji zaidi, wakahitaji pass zake, swashbuckling, tantalizing football na Panenka zake, aliibeba timu mgongoni mwake mpaka zile fainali pale Ujeruman, hakuna aliejua kuwa mwisho wake utakua mbaya zaidi ya ule wa 2004

Nakumbuka pia Goliath alitangaza kustaafu soka la klabu Mei 7 pale Bernabeu, uwanja ulijaa nembo ya 'Zidane 5', alipiga goli lake la mwisho kwenye ile sare ya 3-3 dhidi ya Villareal mbele ya Alfredo di Stefano, ilikua cross ya Beckham, baadae alirejea kuwaaga na machozi yakimtoka sana
Zizuu sio mwarabu
 
Back
Top Bottom