Zinduna talk show wiki ijayo mjengoni atakuwepo mama kipenzi BADILI TABIA~~~~~!

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,378
3,379
avatar45959_18.gif

BADILI TABIA

Ni matumaini yangu kwamba kwa wale ndugu zangu waislamu wameanza mfungo wa mwezi mtukufu salama kabisa.

Baada ya kupata nafuu naamini inshaallah wiki ijayo Jumamosi ya tarehe 28, Julai 2012 kipindi hili cha Zinduna talk show kitarejea kama kawaida na nimeona nianze na mtu muhimu sana hapa JF, Mama yangu wa hiyari BADILI TABIA.

Naomba kwa hisani yako mama uthibitishe uwepo wako katika kipindi hicho muhimu hapo juma lijalo naamini itakuwa ni fursa nzuri kwa wana JF kukufahamu vizuri na labda watapata pia fursa ya kujifunza mengi kupitia uzoefu wako katika mapenzi na mahusiano ya kijamii.

Pia ningependa kuwashukuru Smile na Erickb52 kwa kujitolea kuendesha kipindi hiki wakati nilipokuwa mgonjwa, naamini humu kuna vipaji vingi sana na sasa najua kuwa, kumbe hata nitakapokuwa na udhuru wapo wadau wa kusongesha Zinduna talk show kama kawa.

Nawatakia siku njema na ninaomba wiki ijayo tuwe pamoja katika kumkaribisha mama yetu BADILI TABIA

ONYO: Kipindi hakipo leo kwa hiyo msianze kumsakama mualikwa na maswali, subirini wiki ijayo ndio mje hapa na maswali yenu.
 
Last edited by a moderator:
kwenye hii show kuna ratiba ama mtu analipia kwanza?

Inategemea sana na uwepo wa mtu, mwanzoni nilikuwa nawasiliana na mwalikwa kwa PM, lakini sasa nitakuwa naweka jina la mwalikwa wa wiki inayofuata katika kila talk show ili mwalikwa huyo aweze kuthibitisha uwepo wake siku hiyo aliyoalikwa.
Kwa kuwa zimepita wiki mbili bila mimi kuwepo online, ndio maana nimetumia fursa hii kutoa mwaliko rasmi kwa mama yetu BADILI TABIA, na kama akishindwa kuthibitisha, basi nitachagua mtu mwingine.
 
Last edited by a moderator:
Ungetoa Agenda kwanza nadhani tungejifua vilivyo kwa ajili ya Live Show.....manake nimetingwa vibaya na mambo yanayoendelea sasa hivi nchini...Lol
Agenda maswali hayatofautiani sana, soma talk show za nyuma, lakini pia kila mtu anaruhusiwa kuuliza swali lolote.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom