Zinduna
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 2,378
- 3,379
platozoom akiwa katika pozi
Sublakheri wapenzi wasomaji wa JF, kwa wale ndugu zangu wakristo nasema Bwana Yesu asifiwe sana.
Haya tena leo mjengoni nipo na ndugu yetu, jamaa yetu na rafiki yetu platozoom. Mahojiano yangu na platozoom yatasawiri zaidi kwenye maisha yake binafsi na kazi zake za mapema.
Line za ku-post Comments ziko wazi, Mwana JF yeyote anaweza kutumia fursa hii kumuuliza platozoom swali lolote na yeye bila shaka atayajibu maswali yenu kwa kadiri atakavyopata muda.
Kwa kuanza ninayo maswali kumi na sita ambayo ningependa kumuuliza platozoom:
1. Je umezaliwa awamu ipi ya utawala katika nchi yetu?
2. Hebu nipe kwa kifupi historia kuhusu maisha yako ya shule, yaani ni changamoto gani ambazo ulikabiliana nazo na leo hii ukiangalia ulipotoka unajiona kama shujaa.
3. Hebu nipe historia yako ya hapa JF kwa kifupi, yaani ulifahamuje kuhusu JF, ulijiunga lini na ni nini kilikusukuma hadi ukajiunga na JF?
4. Je Ulifahamuje kuhusu tendo la kujamiiana? Yaani ni nani alikufundisha kwamba hiyo kitu downthere ina matumizi mengine mbali na yale ya kutabawali?
5. Je Umewahi Kutendwa?
6. Je umeoa? Kama umeoa, Je una watoto wangapi, na kama hujaoa, ina maana huna hata kabinti ka kuchombeza?
7. Je umewahi kupitisha usiku na kahaba?
8. Je ulipojivinjari na kahaba uliona tofauti yoyote na unachokipata kutoka kwa Mke/Mpenzi wako?
9. Je umetahiriwa, kama umetahiriwa, ulitahiriwa ukiwa na umri gani, na je ulitahiriwa kwa ganzi au kavu kavu kama wamasai?
10. Je ni tukio gani liliwahi kukuhuzunisha sana?
11. Je ni tukio gani liliwahi kukufurahisha sana?
12. Je unapenda kuvaa nguo za aina gani?
13. Ukipata fursa ya kupata staftahi na King'asti, Je ungapenda kujadili jambo gani na yeye?
14. Je ni mwana JF gani unavutiwa na post zake, yaani ukiona jina lake tu kama ame-post thread unashawishika kuifungua ili kujua kilichomo?
15. Je ni jambo gani umewahi kulifanya kwa faida ya nchi yako na ambalo hata ukifa litabaki kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo?
16. Una ushauri gani kuhusu hiki kipindi cha Zinduna Talk Show…….
Haya nakaribisha maswali yenu wadau na hivi punde Bwana platozoom atakuja kuyajibu maswali yenu.
Karibuni sana
MABADILIKO:
Wiki ijayo Zinduna Talk Show atakuwepo The Boss na host atakuwa ni lara 1.
Madame B, atakuwepo mjengoni wiki inayofuata
Nawasilisha
Last edited by a moderator: