Zinduna Talk Show: Leo mjengoni nipo na Platozoomn~~~!

Zinduna

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
2,378
3,379
avatar67909_13.gif

platozoom akiwa katika pozi

Sublakheri wapenzi wasomaji wa JF, kwa wale ndugu zangu wakristo nasema Bwana Yesu asifiwe sana.

Haya tena leo mjengoni nipo na ndugu yetu, jamaa yetu na rafiki yetu platozoom. Mahojiano yangu na platozoom yatasawiri zaidi kwenye maisha yake binafsi na kazi zake za mapema.

Line za ku-post Comments ziko wazi, Mwana JF yeyote anaweza kutumia fursa hii kumuuliza platozoom swali lolote na yeye bila shaka atayajibu maswali yenu kwa kadiri atakavyopata muda.

Kwa kuanza ninayo maswali kumi na sita ambayo ningependa kumuuliza platozoom:

1. Je umezaliwa awamu ipi ya utawala katika nchi yetu?

2. Hebu nipe kwa kifupi historia kuhusu maisha yako ya shule, yaani ni changamoto gani ambazo ulikabiliana nazo na leo hii ukiangalia ulipotoka unajiona kama shujaa.
3. Hebu nipe historia yako ya hapa JF kwa kifupi, yaani ulifahamuje kuhusu JF, ulijiunga lini na ni nini kilikusukuma hadi ukajiunga na JF?
4. Je Ulifahamuje kuhusu tendo la kujamiiana? Yaani ni nani alikufundisha kwamba hiyo kitu downthere ina matumizi mengine mbali na yale ya kutabawali?
5. Je Umewahi Kutendwa?
6. Je umeoa? Kama umeoa, Je una watoto wangapi, na kama hujaoa, ina maana huna hata kabinti ka kuchombeza?
7. Je umewahi kupitisha usiku na kahaba?
8. Je ulipojivinjari na kahaba uliona tofauti yoyote na unachokipata kutoka kwa Mke/Mpenzi wako?
9. Je umetahiriwa, kama umetahiriwa, ulitahiriwa ukiwa na umri gani, na je ulitahiriwa kwa ganzi au kavu kavu kama wamasai?
10. Je ni tukio gani liliwahi kukuhuzunisha sana?
11. Je ni tukio gani liliwahi kukufurahisha sana?
12. Je unapenda kuvaa nguo za aina gani?
13. Ukipata fursa ya kupata staftahi na King'asti, Je ungapenda kujadili jambo gani na yeye?
14. Je ni mwana JF gani unavutiwa na post zake, yaani ukiona jina lake tu kama ame-post thread unashawishika kuifungua ili kujua kilichomo?
15. Je ni jambo gani umewahi kulifanya kwa faida ya nchi yako na ambalo hata ukifa litabaki kama kumbukumbu kwa vizazi vijavyo?
16. Una ushauri gani kuhusu hiki kipindi cha Zinduna Talk Show…….

Haya nakaribisha maswali yenu wadau na hivi punde Bwana platozoom atakuja kuyajibu maswali yenu.

Karibuni sana

MABADILIKO:

Wiki ijayo Zinduna Talk Show atakuwepo The Boss na host atakuwa ni lara 1.
Madame B, atakuwepo mjengoni wiki inayofuata

Nawasilisha
 
Last edited by a moderator:
Swali la kizushi. Ukiambiwa u"spend" night na Zinduna utakubali au utakataa na kwanini? Kama utakubali, unatarajia nini? Ku"enjoy" au "boring!?".
 
Last edited by a moderator:
Ukipata nafasi ya kuwa PRESIDENT WA TZ KWA MUDA wa mwaka mmoja utafanyaje? je kati ya ccm na chadema wapi upendo wako umeegemea?
 
Habari zenyu Wana-JF ...Ndiye mimi umsolopagazi Platozoom. Kwanza nashuru kwa kukaribishwa kwenye kipindi cha Zinduna Talk Show. Na bila shaka moyo unassuzika kwa sababu ninaweza kuona laptop yake kwa uzuri zaidi! Naanza kujibu maswali ya Zinduna kama hivi:

1. Je umezaliwa awamu ipi ya utawala katika nchi yetu?

Nimezaliwa katika awamu ya Kwanza ya utawala.

2. Hebu nipe kwa kifupi historia kuhusu maisha yako ya shule, yaani ni changamoto gani ambazo ulikabiliana nazo na leo hii ukiangalia ulipotoka unajiona kama shujaa.

Ebanaa eeh, mara ya kwanza kupelekwa nkwa ajili ya kuandikishwa ticha mmoja alinikataa kwa madai bado mdogo, enzi hizo unazungusha mkono wa kulia kwenye sikio la la upande wa wa kushoto.

Kuna nyakati nyingi shuleni sikuwa na viatu, na haikuwa shida sana kwa sababu karibia robo tatu hawakuwa navyo. Hakuna kilichoharibika kwa sababu hakukuwa na ‘class’ za walionazo na wasio nazo.
Changamoto kubwa zaidi ni uwezo wa wazazi ambao ulikuwa wa kupanda na kushuka lakini sikuwahi kuiba wala kudhulumu. Nashukuru nilizaliwa Wilaya na mtaa wa wababe na wavuta bangi lakini sikuwahi kuitia mdomoni japo harufu yake nilivuta!!

3. Hebu nipe historia yako ya hapa JF kwa kifupi, yaani ulifahamuje kuhusu JF, ulijiunga lini na ni nini kilikusukuma hadi ukajiunga na JF?

Mimi ni msomaji mzuri wa magazeti tokea nikiwa mdogo bila kusahau vitabu vya Willy Gamba (Njama, kikosi cha kisasi n.k), magazeti (Mfanyakazi, Uhuru n Hoja) kwa hiyo ilikuwa rahisi kwangu kupata taarifa za Jamii forums na kwa sababu ya udadisi nikawa nasoma posts za watu tokea 2006 japo nilijiunga rasmi February mwaka huu.

Inaendelea..............
 
4. Je Ulifahamuje kuhusu tendo la kujamiiana? Yaani ni nani alikufundisha kwamba hiyo kitu downthere ina matumizi mengine mbali na yale ya kutabawali?

Yaani unauliza rangi ya mkaa? bila shaka nilifahamu kwanza kupitia mchezo wa kujificha na kibaba baba ila haikuwa tamu hivyo. Baadaye nikiwa balehe binti mmoja akanionjesha ndio hapo nikajua kuumbe asali si lazima uipate kwenye mzinga tu !!

Halafu kutabawali ni nini?

5. Je Umewahi Kutendwa?

Yah, aisee nilitendwa na binti flani hivi niliyempenda sana lakini baada ya miaka flani akarudi kama tongwa aliyekosa kitoweo!

6. Je umeoa? Kama umeoa, Je una watoto wangapi, na kama hujaoa, ina maana huna hata kabinti ka kuchombeza?

Sijaoa bana bado natunga sheria. Halafu kwa nini uite "kabinti?" nina mpenzi na kuhusu kuchombeza mimi hataa huwa anakuja na kutandika kitanda na kuondoka!!!
Bado milango ipo wazi lakini

7. Je umewahi kupitisha usiku na kahaba?

Maswali mengine yanahitaji tafakuri ya kina. Ngoja niingie maktaba kwanza ili nije na majibu ya kiprotokali.lakini Bishanga anaweza kujibu hili swali kwa niaba yangu

8. Je ulipojivinjari na kahaba uliona tofauti yoyote na unachokipata kutoka kwa Mke/Mpenzi wako?

Not applicable!

9. Je umetahiriwa, kama umetahiriwa, ulitahiriwa ukiwa na umri gani, na je ulitahiriwa kwa ganzi au kavu kavu kama wamasai?

Ilikuwa kwa ganzi bana nikiwa na 12yrs.

10. Je ni tukio gani liliwahi kukuhuzunisha sana?

Kwa nyakati tofauti nimehuzunika kwa kuwapoteza Wazazi wangu….lakini kubwa zaidi alipofariki kaka yangu. Acha tu.
 
Swali la kizushi. Ukiambiwa u"spend" night na Zinduna utakubali au utakataa na kwanini? Kama utakubali, unatarajia nini? Ku"enjoy" au "boring!?".

Mbona unauliza swali la kitoto kabisa....nani anaweza kukataa ofa kama hiyo...we vipi wewe!!
 
Haya endelea kutiririka mwanawane

BTW - KUTABAWALI ni kitendo cha kujisaidia haja ndogo aka KUKOJOA MKOJO
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom