mwanamama
Member
- Feb 6, 2008
- 61
- 0
Ndugu wana Jamii naomba Msaada wenu,Nimekutana na baadhi ya watu wana T-shirts za JF,nimejaribu kuwauliza wamepata wapi na jibu lao ni kwamba T-shirts hizo zinagawiwa bure kwa Members wa JF.Nilishindwa kuendeleza Mjadala huo kwa sababu sehemu tuliyokuwepo,haikuwa muafaka kwa mazungumzo hayo.Nimejaribu kuwasiliana na baadhi ya members wengine humu,nao kama mimi hawajui lolote kuhusu T-shirts hizo.Kama kuna yeyote ana Ufahamu kuhusu T-shirts hizo ninaomba maelekezo,nataka kuwa na T-shirt hizo,hata kama kwa kununua niko Tayari.Kwa mtazamo wangu ingekuwa vyema kama suala hilo lingewekwa wazi hapa Barazani,kuliko kupeana hizo T-shirts kwa njia za uvunguni/kificho.
Tumekuwa # 1 kupigia kelele Ufisadi,sisi wenyewe suala dogo tu la T-shirts linatushinda,na tunapeana T-shirts kwa kuangalia majina,na kuna member kaniambia kuwa T-shirts zinapatikana bure, kwa sijui Premium members, sasa kama tunaanza kugawanywa hivyo,itatufanya wanyonge tujisikie JF sio Uwanja wetu,kama T-shirts tu, tunaangaliana kwa status,itakuwaje tukipata Madaraka ya Umma,si ndio wale wanyonge/Masikini Wakulima na Wafanyakazi hatutowajali na kukumbatia wafanyabiashara (wenye nazo).Nilifikiri kuwa JF ni Uwanja wa kujenga Jamii iliyo sawa na huru bila kujali Uwezo wa mtu,bali kuujali Utanzania wake na mawazo yake juu ya kuikomboa Nchi yetu inayoangamizwa na Uongozi Mbovu? Naanza kupata wasiwasi kuwa "Tunayoandika/Zungumza hapa hatutoyatenda tukipata Madaraka".Siupendi kabisa Msemo wa Kaka yangu nyani Ngabu,(Waafrika ndivyo Tulivyo"),lakini mara nyingine nauona kama kwamba una ukweli,naomba kuhitimisha kwa kuomba radhi kama maneno yangu yamewakwaza wengine,lakini naomba majibu hapa hapa Ubaoni.Tafadhali Moderators naomba muiweke hii thread mahali appropriate kama ikibidi