Zinapatikana Wapi JF T-shirts?

Status
Not open for further replies.

mwanamama

Member
Feb 6, 2008
61
0
Ndugu wana Jamii naomba Msaada wenu,Nimekutana na baadhi ya watu wana T-shirts za JF,nimejaribu kuwauliza wamepata wapi na jibu lao ni kwamba T-shirts hizo zinagawiwa bure kwa Members wa JF.Nilishindwa kuendeleza Mjadala huo kwa sababu sehemu tuliyokuwepo,haikuwa muafaka kwa mazungumzo hayo.Nimejaribu kuwasiliana na baadhi ya members wengine humu,nao kama mimi hawajui lolote kuhusu T-shirts hizo.Kama kuna yeyote ana Ufahamu kuhusu T-shirts hizo ninaomba maelekezo,nataka kuwa na T-shirt hizo,hata kama kwa kununua niko Tayari.Kwa mtazamo wangu ingekuwa vyema kama suala hilo lingewekwa wazi hapa Barazani,kuliko kupeana hizo T-shirts kwa njia za uvunguni/kificho.

Tumekuwa # 1 kupigia kelele Ufisadi,sisi wenyewe suala dogo tu la T-shirts linatushinda,na tunapeana T-shirts kwa kuangalia majina,na kuna member kaniambia kuwa T-shirts zinapatikana bure, kwa sijui Premium members, sasa kama tunaanza kugawanywa hivyo,itatufanya wanyonge tujisikie JF sio Uwanja wetu,kama T-shirts tu, tunaangaliana kwa status,itakuwaje tukipata Madaraka ya Umma,si ndio wale wanyonge/Masikini Wakulima na Wafanyakazi hatutowajali na kukumbatia wafanyabiashara (wenye nazo).Nilifikiri kuwa JF ni Uwanja wa kujenga Jamii iliyo sawa na huru bila kujali Uwezo wa mtu,bali kuujali Utanzania wake na mawazo yake juu ya kuikomboa Nchi yetu inayoangamizwa na Uongozi Mbovu? Naanza kupata wasiwasi kuwa "Tunayoandika/Zungumza hapa hatutoyatenda tukipata Madaraka".Siupendi kabisa Msemo wa Kaka yangu nyani Ngabu,(Waafrika ndivyo Tulivyo"),lakini mara nyingine nauona kama kwamba una ukweli,naomba kuhitimisha kwa kuomba radhi kama maneno yangu yamewakwaza wengine,lakini naomba majibu hapa hapa Ubaoni.Tafadhali Moderators naomba muiweke hii thread mahali appropriate kama ikibidi
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,327
2,000
sasa hata kama mtu alikuwa na mpango wa kukupa si ataghairi.. badala ya kuuliza ulivyofanya badala yake umekuja na kukandia! Hizo tshirt ulizoziona zinasema JamboForums au JamiiForums...?
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,992
2,000
Mwanakijiji,
Hizo T-shirts zinasema JAMBOFORUMS!

Hizo Tshirts zilikuwa ziuzwe kwa kila mwanachama popote pale alipo duniani. Kutokana na sababu zilizo nje ya wamiliki wa JF ilibidi jina libadilishwe toka Jambo Forums na kuwa Jamii Forums na wakati huo order ya kutengeneza Tshirts za Jambo Forums imeshatolewa. Hivyo wamiliki wakaona ni bora fulana hizo wazigawe bure kwa baadhi ya wanachama ambao wamechangia kwa hali na mali kuwepo hewani kwa JF. Nadhani nimekusaidia kujibu swali lako.
 

Mwazange

JF-Expert Member
Nov 16, 2007
1,056
1,225
Mama nina imani Bubu ataka Kusema jibu lake litakuwa limekutosheleza. Nimebaki na fulana chache mkononi, nyingine nitakwenda nazo Columbus kama tulivyoahidiana, lakini nidondoshee anuani yako ya wapi kwa kuiondosha kwenye PM, nitakuletea nawewe.
Ingekuwa uungwana kama ungenitafuta kiustaarabu kwenye PM kuliko kunianika hapa jamvini kunishtaki.
Inshaallah basi nina imani utakuwa umenielewa.
 

green29

JF-Expert Member
Jul 4, 2007
311
225
sasa hata kama mtu alikuwa na mpango wa kukupa si ataghairi.. badala ya kuuliza ulivyofanya badala yake umekuja na kukandia! Hizo tshirt ulizoziona zinasema JamboForums au JamiiForums...?

Mzee MKJ I wish ungeweka quotation mark kwenye hili jibu, mbona TONE inafanana sana na kumuenzi mjasiriamali wa Seaview/Lushoto/Lupaso?! kwi kwi kwi
 

Field Marshall ES

JF-Expert Member
Apr 27, 2006
12,657
0
Hizo Tshirts zilikuwa ziuzwe kwa kila mwanachama popote pale alipo duniani. Kutokana na sababu zilizo nje ya wamiliki wa JF ilibidi jina libadilishwe toka Jambo Forums na kuwa Jamii Forums na wakati huo order ya kutengeneza Tshirts za Jambo Forums imeshatolewa. Hivyo wamiliki wakaona ni bora fulana hizo wazigawe bure kwa baadhi ya wanachama ambao wamechangia kwa hali na mali kuwepo hewani kwa JF. Nadhani nimekusaidia kujibu swali lako.
__________________

Saafi sana mkuu Bubu, hakuna la kuongeza hapo.
 

Mwazange

JF-Expert Member
Nov 16, 2007
1,056
1,225
Kama kuna yeyote ana Ufahamu kuhusu T-shirts hizo ninaomba maelekezo,nataka kuwa na T-shirt hizo,hata kama kwa kununua niko Tayari.Kwa mtazamo wangu ingekuwa vyema kama suala hilo lingewekwa wazi hapa Barazani,kuliko kupeana hizo T-shirts kwa njia za uvunguni/kificho.
Kuna taratibu kadhaa zinakamilishwa za kiutawala, 'usiniulize ni zipi' then watakaponiambia kuwa tayari, then tutakuwa tayari kufyatua za jina jipya...till then wote tuko kwenye sidelines tunasubiri kipenga.
 

Kuhani

JF-Expert Member
Apr 2, 2008
2,944
1,195
Kuna taratibu kadhaa zinakamilishwa na kiutawala, 'usiniulize ni zipi' then watakaponiambia kuwa tayari, then tutakuwa tayari kufyatua za jina jipya...till then wote tuko kwenye sidelines tunasubiri kipenga.

Sitakuuliza ni zipi!

Hizo T-shirt mpya zitapatikana kwa utaratibu gani?
 

Mwazange

JF-Expert Member
Nov 16, 2007
1,056
1,225
Sitakuuliza ni zipi!

Hizo T-shirt mpya zitapatikana kwa utaratibu gani?

Muheshimiwa mambo bado yako jikoni, yakikamilika nitayabandika hapahapa ubaoni, jinsi gani ya kupatikana na kadhalika, pindi utawala ukinielekeza...till then mimi pia nasubiria tu.
Na pia unaweza ukaninong'oneza (PM) ni size gani na wapi pa kuidropu ya jina la zamani kama utapendelea....
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom