Zinaa Ya Maadili na Uzalendo Dhidi Ya Majipu Yanayotumbuliwa

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
1,168
1,071
Toka zoezi la utumbuaji wa vipere,Majipu yalio mgongoni,miguuni,tumboni,kifuani n.k lianzishwe na viongozi wa awamu ya tano chini His Excellency JPM kumekuwapo na mabadiriko chanya na hasi kwenye jamii lengwa na faidika na utumbuaji husika.

Mathalani kwa wananchi wa kawaida ambao ndio mabosi wa wachaguliwa na wateule wengi wamepongeza sana zoezi zima na kumwaga sifa kedekede kwa viongozi wetu na yamkini kuwaombea dua kimoyo moyo ktk mchakato husika.

Uozo ,uchafu na ukosefu wa matibabu sahihi kwa miaka mingi uliosababishwa na utendaji dhaifu,ukosefu wa kinga uzalendo ,upungufu wa kinga usimamiaji thabiti na utekelezaji wa majukumu pasipo dawa maadiri hivyo kuathiri utoaji huduma za msingi kwa umma na kuwa chanzo cha majibu kuota ktk mwili Tanzania.

Zipo athari kadhaa zitokanazo na kuathiriwa kiufahamu na kiutendaji kwa idara/taasisi zenye kuonekana na dalili za majipu kuota katika miili,nafsi na roho.Wapo ambao walikerwa sana na uozo,uchafu wa majipu lakini hawakuwa na namna isipokuwa kushiriki kwa shingo upande uzalimu wa zinaa ya wizi,ufisadi na matumizi mabaya ya dhamana ya vyeo vyao ...lakini wapo ambao warishiriki kwa dhati kutengeneza mifumo ya ufisadi na unyang'anyi wa mali za umma..

Maumivu ya mtumbuliwa jibu yanaweza kuhisiwa kwa karibu hata na majirani,marafiki,ndugu wa mtumbuliwaji..wapo wanaoziba macho yao wasione usaa,wapo wanaoziba maskio wasisikie kilio na yowe za anaetumbuliwa...lakini wapo wanaopata hata kiu maji, haja ndogo au kubwa pindi waonapo au kusikia zoezi likifanyika.


 
Back
Top Bottom