Zimwi la ufisadi bado linamwandama Rais Mstaafu Ben Mkapa?

kingrumanyika

Member
Dec 30, 2011
12
0
Sikupata fursa ya kusikiliza kwa kirefu interview yake na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano mmoja huko Arusha, juu ya ushirikiano kupitia mpango wa EPA kama sikosei. Lakini mwishoni kabisa, sehemu ambayo nilibahatika kumsikiliza kupitia ITV, bwana mkubwa huyo ambaye pamoja na mafanikio yake akilinganishwa na huyu aliyepo sasa, bado amekuwa akiandamwa na kashfa za ufisadi ama kwa kushiriki moja kwa moja au kinyume chake, amesikika akisema kuwa eti Watanzania wamekuwa wakiwaonea Watanzania wenzao wanaoamua kuwekeza hapa nchini kwa kuanzisha viwanda.

Anasema kuwa kila wanapojikakamua na kuamua kuanzisha viwanda hapa nchini, tumekuwa tukiwaonea wivu na kuwakwamisha kwa kuwaita mafisadi. Hakusubiri kufafanua kauli hiyo, akaondoka, akiwaacha wanahabari wamepigwa bumbuwazi! Ingawa tunaweza kupata right quotation kutoka katika magazeti ya leo!

Hii si mara ya kwanza, Ben amesikika akitoa maoni yake mahali kisha anagusia ufisadi akionesha namna anavyochukizwa na vita hiyo iliyoanzishwa pale Mwembeyanga mwaka 2007. Tangu wakati huo amekuwa kitajawa kuhusika katika kashfa kadhaa moja kwa moja, tena kw akutumia kofia ya urais au kwa kuzembea kufanya maamuzi akiwa madarakani.

Kweli zimwi likujualo, halikuli ukakwisha. Zimwi la Ufisadi linamfahamu vyema Mkapa, kama ilivyoelezewa vyema kwenye list of shame ya akina Dkt. Slaa na wenzake, pale Mwembeyanga, Dar es Salaam.
 
Tutamsema SANA mzee Mkapa ila akitoka madarakani Baba Riz1 nakwambia yatakofumuka tutatamani MKAPA atangazwe mtakatifu kwa kumlinganisha na huyu!!!
 
Na hili zimwi litamwandama mpaka anaingia kaburini na akichelewa atasimama kizimbani kujibu tuhuma hizi
 
Back
Top Bottom