Uchaguzi 2020 Zimebaki wiki nne kampeni zianze, CHADEMA na ACT-Wazalendo mna nini cha kutuambia?

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
8,708
5,711
Sio siri wala sio kificho ni kuwa ule mchakato wa vyama ambavyo nia yao kubwa ni kukamata dola wataanza kutongoza wananchi ili wakubalike kwa wanachi utaanza hivi karibuni.

Lakini swali kubwa la msingi ni kuwa vya vyama vya upinzani vilivyojaa unafiki na kukosa uzalendo kama Chadema na Act wazalendo mna nini cha kuja kutuambia sisi watanzania hoehae?

Kwamba watanzania wana hali ngumu ya maisha? Kwamba ajira ni ngumu? Kwamba hakuna mzunguko wa pesa huku serikali ya Ccm inafanya miradi mikubwa kama JNHPP?

Nataka niwahakikishie kuwa CCM ni chama makini na kinajua nini maana ya kutengenza ajira,nini maana ya kuwa na mzunguko wa pesa ambao una manufaa ya kiuchumi kwa taifa letu.

Kwanza mnatakiwa mtapokuja na hoja kama hizi mtambue kuwa watanzania sio wajinga! Tunajua hiki kipindi kigumu ni kwa ajili ya manufaa ya taifa letu. Ubadhirifu na ufisadi ulisababisha kuwe na mzunguko mkubwa wa pesa ambao ulifanya hata watu wajisahau kuwa kufanya kazi ni upuuzi bali kuna shortcut za kuwin maisha.

Pia mnatakiwa mtambue kuwa hata nchi zilizoendelea hakuna serikali ambayo imeajiri raia wake wenye sifa za kuajiriwa kwa 100% na hapa mnatakiwa mjue kuwa Tanzania ya mwaka 1990 sio ya leo. Maana unaweza kuwa na degree ukauza uji mtaani maana sio rahisi serikali kuajiri kila msomi au mtu mwenye weledi.

Nimewazungumzia CHADEMA na Act Wazalendo sababu ni vyama vya kinafiki na vibaraka wa mabeberu na havina nia njema na taifa la Tanzania. Kampeni zinaanza soon,ngoja tusikie mtatuambia kitu gani?

Mimi ni Chagu wa Malunde nipo Kakola kahama nikishuhudia jinsi Twiga minerals ikisafirisha makinia ambayo zaidi ya miaka mitatu yalizuiwa na sasa Tanzania inanufaika kwa 16% shares and 50% Economic benefit.
 
Sasa si ndo usubiri hizo wiki nne uwahoji hili swali.

Mkuu jifunze kuhusanisha matukio na nyakati.
 
Usitegemee maajabu, kudhihirisha udhaifu wao mpaka sasa hawana wagombea uraisi, ilani zao bado-wanasubiri CCM watoe wakopi, wagombea ubunge na madiwani hawana-wanasubiria watakao katwa na CCM
 
Back
Top Bottom