Zimebaki siku ngapi tuhamie Dodoma?

Siku Magufuli akipiga mnada ile Ikulu ya magogoni. Mnijulishe nitume wawakilishi wangu.
 
Nimekuwa nawza hivi ile ahadi ya kuhamia Dodoma bado ipo kama namkumbuka ilikuwa ni DEC mwaka huuu hebu tukumbushame maaana naona wazungu wa WB wanakuja magogoni badala ya huku kwetu kwa kina lusinde
Mh akienda likizo ya xmass chato akirudi anaishia Dodoma na ndo anakuwa kahamia jumla.
 
Watu kama wewe sidhani kama mmeshawahi kufanikisha chochote maishani au hata tu kama una malengo yoyote zaidi ya Majungu, fitina na Unafiki!
Swali la msingi lilikua ni lini hivyo ulipaswa kusema ni siku fulani, tarehe fulani na saa fulani
 
Jengo la Ikulu ya Dar litumika kama makumbusho ama litakuwa Ikulu ndogo inayoizidi nguvu Ikulu ya Chamwino?
 
Utawala huu wa wahuni na waongo waongo sana, Waziri Mkuu muda wote yuko Dar es salaam na Makamu wa Rais naye kila siku yuko Dar es salaam na hawa tuliambiwa wamehamisha ofisi zao Dodoma!

Huyu mtawala naye alisema mwezi ujao anatuachia jiji letu sijui kama ataondoka maana simsikii tena akileta mbwembwe za kuhama
KINA MTU MMOJA YUPO DODOMA KIGOGO KAMA SIO KINGUNGE " JIWE AKITOKA MADARAKANI HAKUNA MTU ATABAKI DODOMA" WATARUDI BONGO
 
Tunamalizia finishing na kupiga rangi,kanla ya mwaka mpya tutakuwa huko....
 
Wazo la kahamisha mji mkuu kwenda katikati ya nchi aliyekuwa rais wa Nigeria wakati huo General Yakubu Gowon alilitoa kwa Nyerere alipofanya ziara hapa kwenye 1973.

Aliporejea nyumbani na kuwasilisha hoja hiyo kwa baraza la kijeshi lililokuwa likitawala Nigeria, wakalipitisha mara moja na wakaanza kulifanyia kazi, ndani ya miaka 15 wakawa wamehamisha makao makuu toka Lagos kwenda Abuja.

Sisi toka Nyerere aanzishe huu mpango, nafikiri ilikuwa ni mwaka 1970 hadi leo imekuwa ni "Chorus" tu tunaimba kiasi kwamba gharama zimekuwa hazishikiki kiasi kwamba sasa tunalazimishwa kuhama kwa kutoa kafara mipango mingine muhimu zaidi na bila hata kuangalia Economic Benefits za mpango wenyewe.

Hoja za kiusalama alizokuwa akitumia Nyerere kama sababu za kuchagiza huu uhamaji kwa dunia ya sasa hazina mantiki kwani leo mtu anawezakuwa amekalia kigoda kule Las Vegas, Nevada na akatuma tu Drone ikaja ikawaangamiza na kurejea salama huko. Hizi ndizo zile tunazoita "Misplaced Priorities and Misuse of State Resources".
 
Kwa kweli Dodoma wangejitahidi wajenge na kupanda miti kwanza upepo ndio utawatoa nduki
 
Back
Top Bottom