Hisia na hamasa za Maandamano nchini: Mapokeo, Mitazamo na Uhalisia (Viongozi na Wananchi)

Neiwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2012
728
633
Kumekuwa na hamasa hamasa ya maandamano kwa kupitia Mitandao ya Kijamii, haswa kupitia Instagram na Telegram. Hamasa hii imeamsha hisia za kila aina kwa wale ambao wanafuatilia kwa karibu.

Hamasa hii imezaa makundi matatu:

Kundi la kwanza: Wale wanaoamini haya maandamano yana tija na yatafanikiwa.

Kundi la pili:
Wale wanaoamini maandamano haya yana tija ila hayatafanikiwa.

Kundi la tatu:
Wale ambao wanaamini haya maandamano hayana tija na wala hayatafanikiwa.​

Kwa wale wasiojua, taarifa za awali za kutaka kufanywa maandamano ni Bi. Mange Kimambi ambaye baada ya kumshambulia kwa posts kadhaa Rais Magufuli kupitia mtandao wa Instagram, aliamua kuwa sasa inatakiwa kuandamana akidai kuwa Upinzani nchini Tanzania hauna nguvu wala mipango thabiti inayoeleweka kuweza kuutoa au kuushinda uongozi uliopo aidha kwa haki (uchaguzi) au kwa kupindua.

Bado ni mapema sana kuzungumzia nini kinatarajiwa kutokea hapa karibuni, ikiwa bado ni Mwezi na nusu toka sasa hadi tarehe iliyopangwa maandamano hayo.

La msingi kuliko yote ni kwamba ni wazi Serikali imeyasikia na tumesikia viongozi mbali mbali wakitoa matamko au kuzungumzia juu ya hamasa hizo za maandamano. Mrejesho huo wa viongozo mbali mbali ikiwemo na rais wa nchi, inafanya kuibuka kwa mijala kwa upana zaidi kama vile, kukuzwa kwa maandamano haya, kukuzwa kwa jina la Mange Kimbambi na kumfanya awe relevant zaidi, kutopokelewa na kutenda sahihi tokana na hamasa hizo, na masuala mengine kede kede.

Kwa wale ambao hawajabahatika kusikia baadhi ya kauli za viongozi unaweza soma hapa chini:-

CP Nsato Marijani (Mkuu wa Operation na mafunzo):

Kuna kikundi ambacho kimetumia mtandao wa Telegram kuhamasisha maandamano nchi nzima kinyume cha sheria na kutaka kwenda ikulu na kufanya hayo wanayotaka kufanya. Naomba nirudie kusema kwamba lolote linalotaka kufanyika katika nchi hii, sisi kama jesi la Polisi tunawaasa wananchi walifanye kwa mjibu wa sheria. Swala la kufanya maandamano ukiwa na nia ya kuiondoa serikali ni uhaini. Hatua kali zitachukuliwadhidi ya watu watakaovunja sheria na tusije kulaumiwa kwa lolote

Rais John Pombe Magufuli:

"Wapo watu wameshindwa kufanya siasa za kweli wangependa kila siku tuwe barabarani tunaandamana, watu wao wanahamia huku wao wanataka wabaki wanaandamana kule nimeshasema ngoja waandamane wataniona, kama kuna baba zao wanawatuma basi watakwenda kuwasilimulia vizuri, niliapa kwa Katiba kwamba nchi hii lazima iwe ya amani na tunataka tujenge uchumi wa kweli ili Watanzania watajirike na hali ya Watanzania imeanza kwenda vizuri mwanzo ni mgumu lakini nataka niwaambie watanzania tupo kwenye wakati mzuri tuvumiliane ili tufike sehemu Tanzania iwe nchi ya asali"

Msome Rais Magufuli: Rais Magufuli: Ole wake atakayeandamana, kama kuna baba zao wanawatuma, watakwenda kuwasimulia vizuri

Paul Makonda (Mkuu wa Mkoa wa Dar):

"Kuna kakundi hapa kanahangaika kweli usiku na mchana wengine wanahangaika kutumia mitandao ya kijamii kutukana viongozi, kuhamasisha sijui wanaita nini sijui maandamano nawapa pole sana, watafanya labda mimi nikiondoka nikiwa siyo Mkuu wa Mkoa kwenye huu Mkoa hiyo mipango mipango yao watafanya labda mimi nikiwa sipo lakini amani ya mkoa wa Dar es Salaam ni muhimu sana"

IGP Simon Sirro (Mkuu wa Jeshi la Polisi):

"Wote tunajua kwamba maandamano Katiba imetamka na sheria za vyama vya siasa imetamka kwamba maandamano ni haki kwa raia lakini kuna utaratibu wa maandamano, sasa kuna maandamano ambayo ni halali na ambayo si halali. Maandamano ambayo si halali maanake yanaashilia uvunjifu wa amani ni maandamano ambayo yanaelekea kutenda uhalifu sasa kama ni maandamano yanakuja kwa njia ya uhalifu na jeshi la polisi lipo kwa ajili ya kuzuia uhalifu maanake ni lazima tuhakikishe maandamano hayo hayafanyiki hivyo ni lazima juhudi ifanyike kabla ya hayo maandamano kufanyika"

Zaidi IGP anasema....

"Maandamano yakifanyika ambayo si halali uwezo wa kuudhibiti tunao sasa natoa tu salamu kwa wale ambao wanafikiri wataweza kufanya maandamano ambayo si halali ya kutaka kuleta vurugu ndani ya nchi ambao ni watu wachache wenye maanake ni lazima watapamba na jeshi la polisi ambalo linasimamia usalama wa nchi hii, lakini niwambie na wale vijana wadogo na wazazi, wazazi wajitahidi sana kulea watoto zao wajaribu kuwaambia watoto zao wasiingie kwenye kuvunja sheria kwani unaweza kuvunja sheria kirahisi ila madhara yake ni makubwa. Unaweza kuingia kwenye maandamano ambayo si ya halali halafu ukileta shida kubwa kwako na familia yako. Wanacheza na hiyo mitandao sijui tumefika mia moja, mia mbili siju elfu moja wajaze wanachosema lakini nasema nafasi hiyo hawataipata"

Msome zaidi IGP Sirro: IGP Sirro: Ole wake atakayeandamana bila kufuata sheria

Kamanda Lazaro Mambosasa:

"Kuna watu ambao wanaendelea kuhamasisha wananchi kuvunja sheria. Wanataka wajiandae kwa maandamano, tarehe wanazoendelea kutaja. lakini wanafanya hivyo wao wakiwa wamekaa sehemu salama. Wanataka kuwaingiza watanzania wengine kwenye shida,"

Msome Mambosasa: Polisi yawakamata wawili kwa mauaji ya Kiongozi wa CHADEMA. Kamanda Mambosasa akataza maandamano ya mitandaoni

Mkuu wa Majeshi (CDF), Jenerali Venance Mabeyo naye akasema: Jenerali Mabeyo(JWTZ): Kuna Viashiria vinavyotishia Usalama wa Nchi. Hatua zinachukuliwa kudhibiti hali hiyo

Uhalisia wa Hamasa hizi za Maandamano:

Kila mmoja ana lake la kusema, lile analoliamini na wengi wanakuwa wanasimamia mawazo yao hayo kwa vigezo mbalimbali....

Naomba kufahamu toka kwenu wana JamiiForums, ni nini uhalisia (tokana na mtazamo wenu) juu ya hamasa hii ya maandamano na namna inavyochukuliwa na viongozi wa juu pamoja na wananchi huko mitaani?

Maoni ya wananchi (Kwa hisani ya Kwanza TV)



Nawasilisha!
 
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema anaandika katika ukurasa wake wa twitter

"Mange sio Chama cha Siasa/Taasisi amewafanya Viongozi wote kuongea, Rais, IGP, Marijani, Mambosasa na wewe Waziri .Taasisi nyingine zitakapoamua kuunga mkono maandamano haya bila shaka kauli zenu nyingine mtazitoa mkiwa The Hague. Hakuna silaha yenye uwezo wa kuishinda haki.

 
Chadema haikubaliki Tanzania ?? Uchaguzi wa uraisi ukipata, ccm Kura 8milioni, chadema Kura 6milioni how can you say chadema haikubaliki ?? ....kama uwezo wakufikili Ndio huu...!! Kweli we are "shit hole"
Sasa wewe kwa kupima kura za sisiemu na za chadema ambazo wewe mwenyewe umeweka hapo unaona nani anakubalika?? Wewe kweli kazi ipo!

Note: Na chadema yenye ukawa ilipata kura mil 5, sita labda za kwako. Za chadema hapo ni kama 2.1 hivi.
 
Nimeamini nguvu ya keyboard ni kubwa sana aiseee.

Amiri Jeshi mkuu, Waziri wa Mammbo ya Ndani, Mkuu wa Majeshi wa nchi na Wakuu wa Jesi la Polisi wote wanahaha kuzima kile alichokiandika mwanamke mmoja akiwa nyuma ya keyboard yake.
Akitekwa mtu akiuawa kimya,sasa mwanamke anawaendesha kama gari bovu,na wanaofia uungwaji mkono wa watanzania kutokana na madhambi yao,biblia inasema hakuna amani kwa wabaya asema Mungu wangu
 
Mwenyekiti wa UDP, John Cheyo amesema mabaraza ya vyama vya siasa yakitumika kikamilifu yanaweza kuondoa malalamiko ya wananchi na viongozi wa upinzani.

Amesema hayo leo Machi 11,2018 akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu vuguvugu la maandamano yaliyopangwa kufanyika Aprili 26,2018 yanayoratibiwa kupitia mitandao ya kijamii.

Cheyo amesema maandamano hayo ni uchochezi na uvunjifu wa amani na kwamba, mambo yanayolalamikiwa yangeweza kutatuliwa kupitia mabaraza hayo.

"Tusitake kufika hatua ya kuandamana barabarani ili kudai haki, Katiba mpya, Tume huru ya uchaguzi. Tukifikia huko amani iliyopo Tanzania tutashindwa kuipata tena na wananchi watakosa nchi nyingine yenye amani ya kukimbilia," amesema.

Cheyo amesema kama tatizo ni fedha kwa ajili ya mabaraza hayo kukutana, Rais John Magufuli anapaswa kutoa fedha kuyawezesha kufanya vikao.
"Siungi mkono hoja za kudai kuwepo mikutano ya hadhara hata kama ni kwa ajili ya kuongeza wanachama kama wanavyodai wengine, naamini kwa sasa mitando ya kijamii ina nguvu kuliko kitu chochote nchini," amesema Cheyo.

Amesema kabla ya kudai haki ya kuandamana, zipo nyingine wananchi wapaswa kuzipa kipaumbele zikiwemo haki ya kuishi, kupata maji safi na salama, elimu na afya.

"Hatuwezi kufika mahali tuseme nchi hii imepotea na hakuna demokrasia kisa tumekosa haki ya kuandamana, haki ya kufanya mikutano ya hadhara. Kila mtu alishuhudia mikutano ya kampeni za uchaguzi wa ubunge wa marudio katika majimbo ya Kinondoni na Siha ilivyogeuka sehemu ya kutukanana," amesema Cheyo.

"Kama kitu mnachokidai kiliweza kusababisha watu kugombana na askari hadi mauaji yakatokea hicho kitu hakitusaidii kama nchi," amesema.

Cheyo amesema yanayodaiwa kwa nguvu hayana faida na manufaa ya kila siku kwa sababu watu wanahitaji kupata wakati wa kulima na kuvuna.

"Hiyo mikutano iliyoshupaliwa sasa na kuhitajika kwa nguvu zote si kweli kwamba kila siku watakuwa barabarani kuhutubia wananchi, fedha tutatafuta saa ngapi, tutalima saa ngapi, hivyo ni vyema tutambue kila kitu kinachofanyika kupitia mambo ya siasa kisiwe kisingizio cha kusema nchi haina amani, haina uhuru," amesema Cheyo.

Amesema viongozi wa dini wanapaswa kuwa kiunganishi cha wananchi na viongozi wa vyama vya siasa na si kufanya kinyume cha hilo.
 
Nimemuona Cheyo akizungumza hayo nimecheka kwelikweli. Analazimisha kwamba vyama vingine visipate wanachama wapya kwakuwa chakwake kimepoteza muelekeo na sasa amekuwa mateka wa ccm. Yeye ni ccm na anachofanya ni kulinda maslahi ya ccm ili amalizie uzee wake vizuri. Cheyo angejua kwamba sasa hivi hakuna muda wa kumsikiliza mnafiki yoyote. Alikuwa wapi kukemea ule uhuni uliokuwa unafanywa na ccm wakati wa uchaguzi wa marudio? Hakuona wala kusikia box la kura lililotolewa kituoni na kurudishwa tena? Kama alikaa kimya basi awaache wengine wahoji.
 
Cheyo muda wako umeshapita. Tuachie sisi tufanye changes wajukuu zako waje kufraia inchi ya asali.

Maandamano yakifanyika wajukuu zako hawatapigwa risasi hovyo kama akwilini polis watakuwa na discipline.

So keep your mouth shut and let your ears listen and your eyes watch 26/04/2018
 
Huyu mzee naye mnafiki
Hizi si enzi za TANU mzee Hii ni generation nyingine kabisa hapo ndipo mnapokosea
Kubembelezana kumeisha
Waacheni vijana wafanye yao

Maandamano ndio mnatoka nyenyenyenye watu wanapigwa risasi wanatekwa wanateswa mnakaaa kimya hebu tupisheni tutengeneza Tz ya watoto wetu na wajukuu zetu ninyi mlishindwa kutupatia hayo kaeni mtulie msitupangie
Wazee wengine wana maudhi kaaa!
 
Shida iliyopo ni mtu mmoja kupiga marufuku wengine wasifanye siasa wakati yeye anafanya siasa mfano kuzindua barabara mara mbili, mwendo kasi mara mbili, na pia kujifanya yeye ni Mungu mtu kwamba hakosei yote tisa jamaa ni mhutu sasa ndo mana ni katili sana
 
Kwani hayo maandamano yanaandaliwa na taasisi gani?

Kwani waandaaji wa hayo maandamano wamewazuia akina Cheyo kuendelea na mipango yao?

Hivi mikutano ya kisiasa ni kwa mujibu wa sheria ya vyama vingi? Au ni hisani? Kama ni kwa mujibu wa sheria ya vyama vingi basi Cheyo ni absolete
 
Hivi bado najiuliza kuhusu baadhi ya viongozi tena ambao wana nguvu sana CHADEMA sijasikia wakizungumza chochote juu ya matukio haya

1. Kwenye uchaguzi wa Kinondoni na matokeo take

2. Tukio la kuuwawa mwanafunzi na baadhi ya madiwani wa chairman

3. Kuhusu hili suala la maandamano na kumorality wafuasi juu ya hill

4. Matukio ya kutekwa na kupotea kwa baadhi ya watu

5. Muenendo wa kisiasa nchini iwe kwa kukemea,kupinga,na kutoa ushauri
 
Utaft wangu binafsi unaonyesha 80% ya watanzania wote hawatak ubabe wa serikali ya jpm na wapo tayari kwa maandamano!
Kinachosababisha ni ukatili na umaskini unaongezeka kwa kasi kila kukicha!
 
Nilijua tu wange kaa kimya mgekuja na",....hawana lolote hao wanamgwaya 'marekani' Mange Kimambi!"
=====
Sasa mmetahadharishwa...tieni mguu barabarani. Waziri wa mambo ya Ndani ni Dr. Mwigulu Nchemba na rais ni Dr. Joseph Magufuli.
 
Back
Top Bottom