Zimebaki saa chache historia mpya kuandikwa EATV Awards


MZK

MZK

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2012
Messages
214
Likes
274
Points
80
MZK

MZK

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2012
214 274 80
Mashabiki wa sanaa nchini na Afrika Mashariki leo Jumamosi ya Desemba 10 watapata kujua wasanii wa muziki na filamu watakaoibuka washindi wa tuzo kubwa kuwahi kufanyika nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla za EATV Awards 2016.

Wasanii hao ambao pia wapo wa kutoka Kenya na Uganda, wataandika historia sambamba na tukio kubwa kwenye tasnia ya sanaa Afrika Mashariki EATV Awards.

Hii ndiyo orodha kamili ya wasanii watakao 'perform' na kuandika historia siku hiyo.

  1. Darassa kutoka Tanzania
  2. Bill Nass kutoka Tanzania
  3. Maurice Kirya kutoka Uganda
  4. Wahu kutoka Kenya
  5. Lady Jaydee kutoka Tanzania
  6. Barnaba kutoka Tanzania
  7. Vanessa Mdee kutoka Tanzania
  8. Shetta kutoka Tanzania
  9. Alikiba kutoka Tanzania
Licha ya wasanii wa muziki pia kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo dance kutoka kwa vijana walioshika nafasi tatu za juu katika mashindano ya Dance100 2016 yanayoendeshwa na EATV.

Wasanii hao wameahidi kuangusha show ya nguvu kwa watakaohudhuria tukio hilo, na kuwataka watu wajitokeze kwa wingi kushuhudia wakiangusha mzigo wa nguvu jukwaani 

Forum statistics

Threads 1,274,326
Members 490,664
Posts 30,508,486