Zimbabwe yafanya mkutano wa kilele wa tembo kujadili usimamizi wa tembo

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,000
1,019
Mkutano wa kilele wa tembo umefunguliwa jana Jumatatu katika mbuga ya wanyamapori ya taifa ya Hwange nchini Zimbabwe, ambapo nchi zinazoshiriki zimetaka kufikia makubaliano kuhusu usimamizi wa tembo na hifadhi ya wanyamapori.

Mkutano huo utakaoendelea hadi Mei 26 utakuwa jukwaa la kujadili mzigo wa ongezeko la kupita kiasi la tembo na athari zinazotokana na marufuku dhidi ya biashara ya kimataifa kuhusu pembe za ndovu.

Mbali na hayo nchi zinazoshiriki zinataka kufikia makubaliano ya pamoja kabla ya mkutano wa 19 wa pande mbalimbali za Makubaliano ya Biashara ya Kimataifa kuhusu Spishi zilizo Hatarini CITES.

Nchi za magharibi na wanaharakati wa haki za wanyama siku zote wanapinga biashara za pembe za ndovu, huku wakiona kuwa ongezeko la uwindaji haramu linatishia maisha ya tembo wa Afrika. Lakini walinzi wa wanyamapori wa Zimbabwe wanaendelea kutetea kuwa mauzo ya pembe za ndovu zenye thamani ya dola milioni 600 za kimarekani zinazohifadhiwa nchini humo yatasaidia kufadhili juhudi za kuhifadhi wanyamapori.
 
Shukrani kwa taarifa
Mmmhhh. Ila wakati mwingne wazungu Wana akili sana. Yaan wana uchungu na wanyama pori kuliko sisi tulio nao hapa. Mfano mzur ujeruman hutoa mamilion ya pesa kila mwaka kulinda hifadhi yetu Serengeti. Huku kinana na kund lake wakitorosha twiga na kuua tembo kila kukicha. Na wamepitisha sheria Kali za kulinda Hawa wanyama
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom