#COVID19 Zimbabwe: Wafanyakazi wote wa Serikali watakiwa kupata chanjo, la sivyo wajiuzulu

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
Wafanyakazi wa Serikali nchini Zimbabwe wametakiwa kupata chanjo ya COVID-19, vinginevyo wametakiwa kujiuzulu.

Waziri wa Katiba wa Nchi hiyo, Ziyambi Ziyambi amekiambia kituo cha Redio cha Kibinafsi nchini humo, ZiFM Stereo, kuwa Wafanyakazi wa Umma wana wajibu wa kuwalinda wengine dhidi ya maambukizi kwa kupata chanjo ya corona.

“Hatuwalazimishi watu kupata chanjo, lakini kama wewe ni mfanyakazi wa serikali, kwa ajili ya ulinzi wako na wa wenzako, kapate chanjo.

Kama unataka kufurahia haki zako, ambazo zinatambuliwa kikatiba, basi unaweza kujiuzulu. Utafika wakati hatutamtaka mwalimu ambaye hajapata chanjo,” alisisitiza Ziyambi.

Serikali ya Zimbabwe imeajiri zaidi ya watu 200,000, kundi kubwa zaidi likiwa walimu.

Visa 125,671 vya corona vimekwisharekodiwa nchini humo, huku vifo vikifikia watu 4,493. Taifa hilo limetoa chanjo kwa watu milioni 2.7 mpaka sasa.

Chanzo: Reuters
 
Ingekuwa waliochanjwa hawawezi kuambukizwa,Wala kufa na Corona hapo sawa. Madikiteta kulazimisha watu wao chanjo imekuwa ni njia ya kujisafisha kwa mabeberu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom