ZIMBABWE: Tanzania imejifunza nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ZIMBABWE: Tanzania imejifunza nini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by changamoto, Sep 16, 2008.

 1. c

  changamoto Member

  #1
  Sep 16, 2008
  Joined: Aug 26, 2008
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  KWA KUWA tuko mbali hatujui kwa hakika maafa yaliyowafika Wazimbabwe katika kipindi cha miaka mifupi tu kutokana na kuwepo kwa chama kimoja kinachodhani kimepewa ahadi na Muumba kutawala milele.


  Jamii yoyote inayokipa kikundi chochote katika jamii kuwa na nguvu na uwezo zaidi kuliko makundi mengine katika jamii kinafanya hivyo kwa hasara yake chenyewe.

  Nadharia ya 'power' katika jamii inataka mgawanyo wake uwe kwa uwiano mzuri ambao hauruhusu labda wanasiasa wa mrengo fulani kunyanyasa watu wengine au wafanyabiashara fulani kuwa na nguvu za kutisha katika jamii au mangimeza fulani kuibia nchi bila watu wengine kujua kwa sababu tu taifa limeshindwa kuwa na wakaguzi wanaojua ujanja wa wajanja kama wao katika kujinufaisha kutokana na keki ya taifa iliyo meza ya ndani au wachimbaji madini fulani kunywa chote kinachopatikana na kuwaacha wananchi hoi.

  Tuiangalia ' theory of power' kwa kuitazama Zimbabwe kwa karibu zaidi na kuona ni hatua gani amabzo sisi kama Watanzania na wazawa wa nchi hii tunaweza kukifanya ili yaliyojitokeza huko yasije yakazuka hapa baada ya miaka michache.
   
Loading...