Zimbabwe: Rais Mnangagwa apitisha Sheria inayowaruhusu wasichana wajawazito kuendelea na masomo

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
242
500
Mwanafunzi Mjamzito.jpg

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesaini sheria inayozuia shule za serikali kuwatenga wasichana ambao ni wajawazito kuhudhuria masomo.

Chini ya marekebisho hayo ya Sheria, walimu pia hawaruhusiwi tena kuwachapa viboko wanafunzi. Sheria mpya pia inasema kwamba hakuna mwanafunzi atakayetengwa shuleni kwa kutokulipa karo ya shule.

Kabla ya marekebisho ya sheria, viongozi wa shule walikuwa na uwezo wa kumfukuza msichana kwa kupata ujauzito lakini kumwacha mvulana anayehusika na ujauzito huo. Kitendo hicho kilionekana kama ubaguzi dhidi ya mtoto wa kike.

Wasomi na wadau wa elimu wameyakaribisha marekebisho hayo na kuyataja kuwa ni maendeleo makubwa. Naye Waziri wa Elimu ya Msingi na Sekondari Kaini Mathema alisema amefurahi kwamba Rais amesaini sheria hiyo mpya.

=========

Harare. Zimbabwe President Emmerson Mnangagwa has signed a law barring government schools from excluding girls who fall pregnant from attending lessons.

Teachers are also no longer allowed to cane pupils, under amendments to the Education Act which became law on Saturday.

The new law also says that no pupil shall be excluded from school for non-payment of school fees.

Prior to the amendments of the law, school authorities could expel a girl for falling pregnant but spare the boy responsible for the same pregnancy, which was seen as discriminatory against the girl child.

The educationists welcomed the amendments as progressive. Primary and Secondary Education Minister Cain Mathema said he was excited that the President had signed the new law.

"The President has just signed the law and we will fully enforce the provisions for the furtherance of education in the country. We believe the Act is a progressive legislation," he said.

Zimbabwe Teachers Association (Zimta) chief executive officer Sifiso Ndlovu said they fully supported the provisions of the Act as it was consistent with modern society. He said corporal punishment engendered a violent society and it was refreshing that it was removed while the outlawing of the exclusion of pregnant pupils helped in the furtherance of the rights of the girl child.

"As Zimta, we fully participated in the crafting of that law. Most of what we raised has been included. We abhor the use of corporal punishment because it is an old-fashioned tool of instilling discipline," he said.

"It has the effect of engendering a violent society. We also support any measure meant to safeguard the interests and rights of the girl child. One such provision is outlawing the exclusion of those that fall pregnant. This is what other societies have embraced and we fully support the provision," said Ndlovu.

Progressive Teachers Union of Zimbabwe secretary-general Raymond Majongwe said while the law would protect the rights of girls, there were fears that some people could take advantage of that. He also said there should be more consultation on the issue of corporal punishment as pupils could engage in illicit behavior knowing that they would not be punished.

"There should have been more consultation on these measures, especially on corporal punishment. Pupils and students may end up abusing drugs knowing they will not be punished," he said.

In terms of the Act, any disciplinary policy shall not permit any treatment which does not respect the human dignity of a pupil. School authorities are now required to draw up a disciplinary policy in accordance with standards set out in regulations prescribed by the minister.

The new law also allows the minister to fix school fees taking into consideration the location and status of a given school.

Source: Daily Nation
 
Sethshalom

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
436
1,000
Huko Tanganyika ndio kwanza wanataka watoto wachapwe hadi wazirai
Yes tena wachapwe zaidi, vitoto vingi vya siku hizi havina akili hata ya kuchota maji mtoni. Vinaona maigizo ya kwenye runinga na kuhisi ndio uhalisia wa maisha. Kuna mahala nimeona kitoto cha miaka 18 cha form 3 kikiomba ushauri wa kuacha shule ili kiolewe na chenzake cha 23. Eti sasa hivi hata darasani hakielewi chochote ni kusinzia tu kikiwaza kitoto chenzake cha 23 kikihofia eti kikiendelea kusoma mpaka form four kitakuta chenzake kimeshaoa mwingine. Sasa watoto hao si wakupigwa tu ,tena fimbo kama mvua ili usingizi uishe
 
Ambokile Amanzi

JF-Expert Member
Dec 12, 2018
611
1,000
Yes tena wachapwe zaidi, vitoto vingi vya siku hizi havina akili hata ya kuchota maji mtoni. Vinaona maigizo ya kwenye runinga na kuhisi ndio uhalisia wa maisha. Kuna mahala nimeona kitoto cha miaka 18 cha form 3 kikiomba ushauri wa kuacha shule ili kiolewe na chenzake cha 23. Eti sasa hivi hata darasani hakielewi chochote ni kusinzia tu kikiwaza kitoto chenzake cha 23 kikihofia eti kikiendelea kusoma mpaka form four kitakuta chenzake kimeshaoa mwingine
Nonsense!
 
Tarakwa

JF-Expert Member
Apr 19, 2017
576
1,000
Emerson Mnangagwa amepiga hatua kubwa kuelekeza taifa kwenye ndoa ya jinsia moja
 
zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,124
2,000
Ha ha ha wamefungulia mbuzi mlango, hivyo vitoto vya kike vitabeba mimba mpaka aibu. Watatuletea mrejesho miaka 5 ijayo. Yale ya UK teenagers wa 12-16ulaya ndio inaongoza kwenye teenagers pregnancy
Tatizo la mimba ni mfumo sio mtu, jamii nzima imeharibika ko sio sawa kuzuia wanafunzi kusoma kisa mimba ni afadhali wapewe adhabu ya faini au kurudia madarasa ila sio kunyimwa kusoma.

Ndio maana takwimu zinaonyesha walio kwenye ndoa ndio wanaongeza maambukizi ya Ukimwi kuliko ambao ni mabachelor. Kwahiyo ni tatizo la jamii nzima tusifanue cherry picking

Nampongeza Munangagwa kwa hili. Elimu ni haki ya kila raia awe mzinzi au mtakatifu.
 
zitto junior

JF-Expert Member
Oct 7, 2013
12,124
2,000
Yes tena wachapwe zaidi, vitoto vingi vya siku hizi havina akili hata ya kuchota maji mtoni. Vinaona maigizo ya kwenye runinga na kuhisi ndio uhalisia wa maisha. Kuna mahala nimeona kitoto cha miaka 18 cha form 3 kikiomba ushauri wa kuacha shule ili kiolewe na chenzake cha 23. Eti sasa hivi hata darasani hakielewi chochote ni kusinzia tu kikiwaza kitoto chenzake cha 23 kikihofia eti kikiendelea kusoma mpaka form four kitakuta chenzake kimeshaoa mwingine. Sasa watoto hao si wakupigwa tu ,tena fimbo kama mvua ili usingizi uishe
Mimi sikuwahi kuchapwa toka nmeingia sekondari na tokea hapo perfomance yangu ilikua nzuri zaidi.

Mambo ya darasani ni makuzi tu na saikolojia sio viboko. Otherwise tulipewa adhabu kulima, Kufyeka nyasi, kujaza maji n.k yaani adhabu za kuongezea skills na endurance. But kuona mtu anashabikia viboko kma viboko karne ya 21 inashangaza kidogo.
 
Ambokile Amanzi

JF-Expert Member
Dec 12, 2018
611
1,000
Tatizo la mimba ni mfumo sio mtu, jamii nzima imeharibika ko sio sawa kuzuia wanafunzi kusoma kisa mimba ni afadhali wapewe adhabu ya faini au kurudia madarasa ila sio kunyimwa kusoma.

Ndio maana takwimu zinaonyesha walio kwenye ndoa ndio wanaongeza maambukizi ya Ukimwi kuliko ambao ni mabachelor. Kwahiyo ni tatizo la jamii nzima tusifanue cherry picking

Nampongeza Munangagwa kwa hili. Elimu ni haki ya kila raia awe mzinzi au mtakatifu.
Halafu hawa hawa mabazazi si ndio huwa wanafurahia kuwatafuna watoto wadogo wa shule?

Leo imekuwa nongwa wahanga wa ubazazi wao kupewa nafasi ya kusoma?

Ati oooh watapewa mimba!!! Kwani hizo mimba anayewapa ni nani kama sio hawa hawa mabazazi butu?
 
Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,345
2,000
Naomba kuelimishwa:

1. Kwa Tanzania, binti akipata ujauzito, huondolewa kwenye shule ya msingi au sekondari serikali au ya binafsi yenye sheria ya shule kuzuia masuala ya mahusiano ya kingono shuleni. Mwanafunzi huyo bado ana ruhusa ya kusoma shule binafsi, au mifumo mingine ya elimu ya umma, kama vile ufundi au ufundi-sanifu. Kama sikosei, kwa nchi ya Marekani, kinara wa kupembejea haki za kidemokrasia, binti apataye ujauzito hulazimika kutohitimu "high school" na badala yake kuhitimu "GED". Je, uelewa huu ni wa uhalisia?

2. Kwa sheria hii mpya, wanategemea matukio ya ujauzito yataongezeka au kupungua miongoni mwa wanafunzi? Mimba za utotoni zikiongezeka huko Zimbabwe, watakaozipata watashauriwa waolewe au watashauriwa wawe 'Single Mothers'?
 
Capastor

Member
Jul 15, 2019
72
125

+imependa maelezo yako yapo kwa logic mzee

Kama marekan inazuia je Tanzania ni nani

Jama hiz sheria znavyoletwa tuztafakar kwa kina na tuanglie wao wanatekeleza vp isiwe tu wanaztunga huko af cc tutekeleze, ikumbukwe sisi ni taifa huru lenye haki ya kujitegemea kimaamuz na sio kuendeshwa kama wanavyotaka wao
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom