ZIMBABWE: Nabii awauzia waumini matango, adai yana upako

Bahati furaha

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
3,028
1,383
Baada ya kisa cha nabii mmoja kutoka nchini Afrika Kusini kuzua hofu juu ya afya ya waumini wake baada ya picha kusambaa akiwapulizia dawa ya kuulia wadudu, kisa kingine kimeibuka nchini Zimbabwe ambapo Nabii huwauzia waumini wake matango wakati wa ibada.

Kisa hicho cha nabii kutoka Zimbabwe, Walter Magaya kinaeleza kuwa matango hayo yanadaiwa kuwa yana upako hivyo yataweza kuwasaidia wale wote watakao tumia.

unnamed-22.jpg

Watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii walionyeshwa kusikitishwa na viongozi hawa wa dini ambao kila siku wamekuwa wakifanya mambo ya kushangaza.

Wakati huo huo, Nabii huyo alipohojiwa alisema kuwa yeye hakuyaleta matango hayo kanisani hapo kwa ajili ya kuwauzia waumini wake, bali ni kuwaonyesha ni kwa kiasi gani yeye ni mkulima mashuhuri. Alisema kuwa anafuga kuku, nguruwe ana bwawa la samaki na pia hulima hivvyo matango hayo ni kuwapa waumini sehemu ya mafanikio yangu.
 
Mbona nnaona waumini wa kike tu na matango! Kasheshe!

Haya makanisa na hawa wachungaji ni majnga, ashaakum si matusi, nilitumiwa picha ya mchungaji mmoja amewafuramisha waumini wake anawalamba makalio.
 
Anawauzia au anawagawia hayo matango? Maana habari hapo chini mchungaji anadai anataka awaonyeshe waumini yeye ni mkulima mwenyebidii.

Watu wa dini wanashangaza sana. Kuanzia wachungaji hadi waumini.

Inaonekana watu wanapenda Mambo rahisi pia vichwani watu wako empty kabisa aiseee. Yani watu wamefungwa akili zao hawaoni hawasikii, wao wanafuata mkumbo tu.

Inasikitisha wanawake ndiyo wahanga wakuu. Angalia picha mamia ya akina mama na akina dada wameinua matango juu wanaimani kubwa watapokea miracles.
 
Sio Binadamu tumekosa akili, sema Watu weusi hasa nyie wanawake mmekosa akili.

Kanisa zima limejaa wanawake.

Na usiombe uoe Mke mlokole halafu wewe sio mlokole utajuta.

Wajinga ndio waliwao, Waumini wa Lusekelo ni mfano tosha.
 
Kuna tofauti gani kati ya hao waumini wanaoyaamini hayo Matango na wale wanaoamini hadithi za kusadikika za kichawi na kishirikina humu?
 
Tupunguze kushangaa majirani zetu, kabla ya kutafakari matendo yetu.
1480506876869.jpg
1480506890445.jpg
kama serikali ya jamuhuri ilithubuthu kufanya hivi loliondo, nini matango Zimbabwe?
 
Ukiwa na tatizo utafanya chochote uambiwacho ndg yangu.

Wapo watu na akili zao wamenyweshwa mikojo yao wenyewe wakiambiwa ni dawa.

Msiwapuuze, wanahitaji msaada.
 
Mbona nnaona waumini wa kike tu na matango! Kasheshe!

Haya makanisa na hawa wachungaji ni majnga, ashaakum si matusi, nilitumiwa picha ya mchungaji mmoja amewafuramisha waumini wake anawalamba makalio.
Ni Kweli dunia imefikia mwisho na utapeli mkubwa ni kupitia makanisa ya kiroho.
 
Ni Kweli dunia imefikia mwisho na utapeli mkubwa ni kupitia makanisa ya kiroho.

Akuna cha dunia imefika mwisho bana labda uko afrika kwetu ndo kufike mwisho ayo mambo yako uko tu mbona mabara mengine ayo mazingaumbwe ya dini ayapo!! Mm nitaendelea kuamini tu kuna mungu wa africa na mungu wa ulaya Asia na marekani
Maana kwa akili ya kawaida tu awezi kua mungu mmoja atufanye waafrica ivyo na wazungu ivi
 
Mkuu naona umesahau ISIL & IS ,hao wapo duniani na wanajengeka kila siku!!!!
 
Kwa kuwa tango ni zao muhimu kwa afya ya binadamu, mchugaji ongeza mgao kwa faida ya afya yao
 
Anawauzia au anawagawia hayo matango? Maana habari hapo chini mchungaji anadai anataka awaonyeshe waumini yeye ni mkulima mwenyebidii.

Watu wa dini wanashangaza sana. Kuanzia wachungaji hadi waumini.

Inaonekana watu wanapenda Mambo rahisi pia vichwani watu wako empty kabisa aiseee. Yani watu wamefungwa akili zao hawaoni hawasikii, wao wanafuata mkumbo tu.

Inasikitisha wanawake ndiyo wahanga wakuu. Angalia picha mamia ya akina mama na akina dada wameinua matango juu wanaimani kubwa watapokea miracles.
Refer yule jamaa alietukana halafu bado nyomi ipo church kwake!!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom