Bahati furaha
JF-Expert Member
- Jul 11, 2012
- 3,030
- 1,384
Baada ya kisa cha nabii mmoja kutoka nchini Afrika Kusini kuzua hofu juu ya afya ya waumini wake baada ya picha kusambaa akiwapulizia dawa ya kuulia wadudu, kisa kingine kimeibuka nchini Zimbabwe ambapo Nabii huwauzia waumini wake matango wakati wa ibada.
Kisa hicho cha nabii kutoka Zimbabwe, Walter Magaya kinaeleza kuwa matango hayo yanadaiwa kuwa yana upako hivyo yataweza kuwasaidia wale wote watakao tumia.
Watu mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii walionyeshwa kusikitishwa na viongozi hawa wa dini ambao kila siku wamekuwa wakifanya mambo ya kushangaza.
Wakati huo huo, Nabii huyo alipohojiwa alisema kuwa yeye hakuyaleta matango hayo kanisani hapo kwa ajili ya kuwauzia waumini wake, bali ni kuwaonyesha ni kwa kiasi gani yeye ni mkulima mashuhuri. Alisema kuwa anafuga kuku, nguruwe ana bwawa la samaki na pia hulima hivvyo matango hayo ni kuwapa waumini sehemu ya mafanikio yangu.