ZIMBABWE: Mke wa Rais Mugabe amtaka mumewe kumtangaza mrithi wake

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
_97104837_mugabenwife.jpg

Rais wa Zimabwe ametakiwa na mkewe kumtaja ''mrithi'' wake ili kupunguza migawanyiko kuhusu mtu atakayemrithi.

''Rais hafai kuwa mwoga kumchagua mrithi wake na neno alke litakuwa la mwisho'',alisema bi Grace Mugabe.

Bwana Mugabe ndio kiongozi mzee zaidi na chama chake cha ZANU PF kimemchagua kuwania urais kwa mara nyengine mwaka ujao.

Lakini makundi pinzani yamekuwa yakiwania urais ili kuimarisha uwezo wao huku kukiwa na wasiwasi kuhusu hali yake ya kiafya.

Chanzo: BBC Swahili
 
Ha ha ha! Ashaona kiza mbele. Kashastuka hatma yake aliyezoea kula na kunywa mezani pa mfalme, ufalme unafikia ukomo hivyo. Ama kweli ukimtegemea mwanadamu siku yaja utadhalilika.

Eti "neno lake litakuwa la mwisho"! Wameshageuza Zimbabwe mali yao! Nchi ya kifalme ile? Haina Katiba na taratibu za kuchagua viongozi? Ulevi wa madaraka tena madaraka ya kubebwa mbaya sana.
 
hapo mzee yuko ndoto ya ngapi sijui?washaona zimbabwe ni kama mji wao wanajiamulia tu.
 
Ha ha ha! Ashaona kiza mbele. Kashastuka hatma yake aliyezoea kula na kunywa mezani pa mfalme, ufalme unafikia ukomo hivyo. Ama kweli ukimtegemea mwanadamu siku yaja utadhalilika.

Eti "neno lake litakuwa la mwisho"! Wameshageuza Zimbabwe mali yao! Nchi ya kifalme ile? Haina Katiba na taratibu za kuchagua viongozi? Ulevi wa madaraka tena madaraka ya kubebwa mbaya sana.
Anaogopa?hujiulizi kwanin amesema Rais asiwe mwoga kutangaza na kuwa atakachotangaza Rais ndio final?

Usijeshangaa huyo chaguo ambaye Mzee Mugabe anaogopa kumtaja na anashinikizwa na mke wake kumtaja ni mwenyewe mkewe, Grace Mugabe.
 
Huyu mzee mwakani wakati wa uchaguzi kama atakuwepo atakuwa amechoka sana.
 
Anaogopa?hujiulizi kwanin amesema Rais asiwe mwoga kutangaza na kuwa atakachotangaza Rais ndio final?

Usijeshangaa huyo chaguo ambaye Mzee Mugabe anaogopa kumtaja na anashinikizwa na mke wake kumtaja ni mwenyewe mkewe, Grace Mugabe.
Duh! Hilo nalo neno. Kumbe anajibashiria "ufalme". Sikuwa nimegundua hilo.
 
Back
Top Bottom