Zimbabwe: Mke wa Mugabe aitwa Mahakamani kwa tuhuma za kumzika Mumewe kinyume na utaratibu wa Kimila

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,848
2,000
Mahakama ya Kitamaduni nchini Zimbabwe yamtaka Mke wa rais wa zamani wa Zimbabwe, Grace Mugabe kufika mahakamani hapo kwa tuhuma za kufanya mazishi “yasiyofaa” ya hayati Rais Robert Mugabe.

Grace Mugabe anatuhumiwa kwa kuenda kinyume na utamaduni wa jamii yao kwa kumzika mume wake katika boma la familia badala ya kumzika sehemu iliyochaguliwa na jamaa zake na mama yake.

Katika waraka kutoka kwa Chifu Zvimba, ambaye ni mkuu wa kitamaduni wa nyumbani kwa kina Mugabe amesema Grace anatakiwa kuufukua mwili wa hayati Rais Mugabe ili uzikwe tena kulingana na utamaduni wa watu wa Zvimba.

Pia ameagizwa kulipa faini ya ng’ombe na mbuzi kwa kukiuka utamaduni. Mugabe alifariki mwaka 2019 katika hospitali moja nchini Singapore akiwa na umri wa miaka 95.

Familia yake iliamua afanyiwe mazishi ya faragha kijijini kwao Kutama wilaya ya Zvimba- karibu kilomita 90 sawa na (maili 55) magharibi mwa mji mkuu wa Harare, baada ya mvutano wa wiki kadhaa na serikali.

Patrick Zhuwao, mpwa wa marehemu rais alisema kwamba Mugabe alizikwa kulingana na ombi lake, uamuzi ambao unastahili kuheshimiwa. Pia hakuna mzozo ndani ya familia akiongeza kwamba suala hilo lipo nje ya mamlaka ya chifu.


Mtanzania
 

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
25,222
2,000
Haya ndo malipo ya udikteta ,unazikwa Kama mbwa au maiti kutembezwa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom