Zimbabwe: Matajiri wasioweza kueleza chanzo cha utajiri wao mali zao kuchukuliwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
2,373
2,000
Mamlaka ya Zimbabwe imesema watu ambao hawawezi kuelezea utajiri wao ulitoka wapi mali zao ziko katika hatari ya kuchukuliwa hata ikiwa mahakama itawaondolea madai ya kuhusika na ufisadi.

Mwenyekiti wa tume ya kupambana na ufisadi Zimbabwe, jaji Loyce Matanda-Moyo, amesema oparesheni mpya nchini humo ni kuchunguza maisha ya matajiri.

Nchi hiyo inakabiliana na mdodoro wa kiuchumi katika kiindi cha mwongo mmoja sasa.

Raia wamekuwa na hasira juu ya huduma mbovu zinazotolewa huku ufisadi ukiendelea kukithiri.

"Huu ni uchunguzi wa maisha ya baadhi ya watu matajiri. Watahitajika kutoa stakabadhi zao kuonesha bidhaa na huduma wanazatoa na zitahitajika kwendana na thamani ya mali walionao. Pia tutaangalia ikiwa watu hawa au biashara zao walikuwa wanalipa ushuru." Justice Matanda-Moyo told Zimbabwe's Sunday News.

Katika oparesheni hiyo, tume hiyo inatumia madaraka iliyopata kuanzia Julai 2019 ya kutaka kuelezewa jinsi watu walivyopata utajiri wao kulingana na kile kinachofahamika kama utajiri usioweza kuelezeka.

Watu wanaochuguzwa wanaweza kwenda katika mahakama ya juu kuelezea utajiri wao lakini iwapo hawatafanya hivyo moja kwa moja mali zao zinachukuliwa.

Zimbabwe sio nchi ya kwanza kuchukua hatua kama hiyo kutaka watu kuelezea vile walivyopata utajiri wao. Ireland na Uingereza zote zilibadilisha sheria zao na kuanzisha sheria ya mali isiyoweza kuelezeka kule ilikotoka 2017.

Shirika la Kimataifa la Kupambana na Ufisadi Transparency International, hivi karibuni lilitaja vifaa vya kimatibabu kukabiliana na virusi vya corona vilivyoagizwa na Zimbambwe kama wenye mashaka.

Shirika hilo lilisema kuwa bei za vifaa vya matibabu ziliongezwa na kuashiria uwezekano wa ufisadi unaoendelea nchini humo.

Aidha, Jumamosi, Waziri wa Afya Obadiah Moyo alishtakiwa kwa makosa ya kutumia vibaya mamlaka yake yenye kuhusishwa na kandarasi ya uagizaji wa bidhaa hizo.

Anatarajiwa kufika tena mahakamani Julai.

BBC Swahili
 

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
5,001
2,000
Watu wengi wameshadhulumiwa kwa mpango huo, hapa nchini wangapi walilizwa na kulia kutokana na ishu kama hio, mambo kama haya kwa Africa yataenda zaidi kisiasa nasio uhalisia ulivyo, chuki na wivu pia havitoachwa nyuma, waafrika wengi sana tuna ile kwa nn flani anapata
Sio kwamba angalau wanafanya kitu sahihi!!?
 

Bambushka

JF-Expert Member
Jan 9, 2020
1,049
2,000
Haa haa matajiri wote ZANU-PF...Ni sawa tu na Bongo, tume vibogoyo hazina meno...mali za wabunge sijui vigogo mawaziri ma RC hakuna ni blah blah to fool the audience...viini macho tupu!

Wazee wa vijisenti hawahojiwi!

Everyday is Saturday.......................... :cool:
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom