Zimbabwe Mambo MAGUMU!

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
24,751
22,003
Zimbabwe: Mambo magumu!

2008-07-25 17:24:53
Na Harare, Zimbabwe


Mfumuko wa bei unaotajwa na Serikali ya Zimbabwe kuwa umefikia asilimia Milioni 2.2 unaendelea kuwafanya wananchi wa Zimbabwe kuishi katika hali ngumu zaidi katika historia ya nchi hiyo ambapo sasa, bei ya vitu karibu vyote ipo katika hesabu za mabilioni, matrilioni na kuendelea.

Aidha, mambo magumu nchini humo yamewafanya hata wananchi kuikejeli Serikali kuwa wao ndio pekee duniani walio na mapesa ya kiwango cha ubilionea, lakini wanaoishi katika maisha ya dhiki zaidi.

Kwa mujibu wa taariza za kiuchumi nchini humo kwa sasa zilizotolewa na vyombo mbalimbali vya habari na kuthibitishwa na Serikali hiyo, ni kwamba sasa, dola moja ya Kimarekani ni sawa na Dola Bilioni 120 za Zimbabwe.

Imeelezwa kuwa kutokana na hali hiyo ya kuporomoka kwa kiwango cha juu kwa pesa ya Zimbabwe, bei ya bidhaa zote ziko katika kiwango cha mabilioni, ikiwa ni pamoja na yai moja la kuku kuuzwa kwa dola Bilioni 35.

Ili kupambana na mfumuko huo usio wa kawaida, Jumatatu iliyopita, Serikali ya Rais Robert Mugabe iliidhinisha utumiaji wa noti mpya yenye thamani, ya dola za Zimbabwe bilioni 100, ambazo kwa sasa ni chini ya thamani ya dola moja ya Kimarekani.

Hata hivyo, hatua hiyo imekuja ikiwa ni miezi sita tu tangu walipoanza kuchapisha noti mpya ya milioni 10 iliyotolewa Januari mwaka huu, ikifuatiwa na noti ya milioni 50 iliyotolewa Aprili na mwezi wa tano walipoidhinisha noti mpya ya milioni 100 na nyingine ya milioni 250, zikifuatiwa na noti ndogo za bilioni tano, 25 na 50.

Raia mmoja wa Zimbabwe amenukuliwa na gazeti moja nchini humo akidai kuwa hata noti hiyo mpya ya dola yao Bilioni 100, hivi sasa haiwezi kugharamia hata nusu ya nauli yake ya kuelekea kazini asubuhi kwa siku moja.

Amedai kuwa kwa mahitaji ya siku ya nauli, yeye huhitaji zaidi ya dola bilioni 500, na kudai kuwa \"mkate mdogo zaidi wa hamburger wa round roll, kwa sasa unauzwa dola bilioni 40\".

``Tunda moja wiki moja iliyopita lilikuwa likiuzwa kwa dola moja ya Marekani, ambayo ni sawa na bilioni 120, lakini kwa sasa imepanda na kufikia dola 2 ambayo ni sawa na bilioni 140,`` amekaririwa mkazi mmoja wa Jijini Harare nchini humo.

Aidha, mkate mmoja sasa unanunuliwa kwa dola ya Zimbabwe bilioni 100, kilo moja ya nyama inanunuliwa kwa dola ya Zimbabwe bilioni 450, wakati lita moja ya maziwa inauzwa kwa dola bilioni 200.

Ernest Nyandoro, 43, mfanyakazi wa kiwanda cha matofali amesema fedha inayotolewa na benki haitoshi kwa kuwa unaweza kutoa dola bilioni 500 na hiyo inaweza kutumika kwa nauli ya kuwapeleka na kuwarudisha watoto shule na kuwanunulia chakula tu.

Naye Gavana wa Benki kuu nchini humo, Bw. Gideon Gono, amesema kwa sasa benki yake inaangalia uwezekano wa kuweka mipaka zaidi katika kutoa fedha.

Aidha mshahara wa mtu wa kati nao umeongezeka na kufikia dola za Zimbabwe trilioni moja na inahisiwa muda si mrefu itaongezeka na kufikia trilioni tano au zaidi, maana pesa zote hizo hazitoshi kwa walau mlo wa mwezi mmoja.

Wakati huohuo, mtaalam mmoja wa viwango vya ubadilishanaji pesa nchini, amefafanua kuwa pesa za Zimbabwe ukizilinganisha na zile za Kibongo, utagundua kuwa hivi sasa, usafiri wa mabasi ya Jijini Harare hugharimu zaidi ya dola Bilioni 40 kwa safari, kwa mlinganisho wa dola moja ya Kimarekani na Shilingi 1,200 za Kibongo kwa viwango vya sasa.

``Ukichukulia nauli ya daladala ya Jijini Dar kuwa Sh.300, kwa Zimbabwe ni sawa na dola zao Bilioni 40 na zaidi,`` imeelezwa.

Aidha, kwa mchanganuo huo wa thamani za fedha za Zimbabwe na Tanzania, kwa kipimo cha dola ya Kimarekani, inaelezwa kuwa bei ya dawa za Panadol za Sh.100 ya Kibongo huweza kuuzwa kwa zaidi ya Dola Bilioni Tisa za Zimbabwe.

Aidha, kwa mchanganuo huo, inaelezwa kuwa bei ya bia inayouzwa kwa Sh. 1,200 za Kitanzania ambazo ni sawa na dola moja ya Kimarekani, kwa Zimbabwe ni sawa na dola zao Bilioni 120, soda inayouzwa kwa sh.400 nchini, kwa Zimbabwe ni zaidi ya dola zao Bilioni 39.
  • SOURCE: Alasiri
 
Waandishi wa habari kwa kweli wanatuangusha sana.
Kwani hawatoi habari zenye kumake sense hata kidogo.
Sasa hayo mahesabu na uchambuzi hapo juu ni wazi kuwa yana utata...Kwasababu inavyoonyesha...Maisha ya wazimbabwe yanaweza kuwa better zaidi ya maisha ya wabongo licha ya inflation hiyo.
 
Zimbabweans are dying faster na hadharani wakati huku kwingine mafisadi anatuua taratibu na QUIETLY!!
 
Waandishi wa habari kwa kweli wanatuangusha sana.
Kwani hawatoi habari zenye kumake sense hata kidogo.
Sasa hayo mahesabu na uchambuzi hapo juu ni wazi kuwa yana utata...Kwasababu inavyoonyesha...Maisha ya wazimbabwe yanaweza kuwa better zaidi ya maisha ya wabongo licha ya inflation hiyo.
Karibu tena jamvini. Pole kwa kukaa keko:)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom